Angalizo: Wanaoitwa interview na utumishi wa umma

Angalizo: Wanaoitwa interview na utumishi wa umma

Mkuu hujajitoa ilimradi ukienda interview usiseme kuwa umeajiriwa hadi siku ya mwisho na utapewa ruhusa ya kufata datasheet kwa mwajiri wa sasa.

Mimi nimefanya vile 2012 na nilikuwa nshafutwa payroll ila LAWSON ikanidaka na ikabdi niombe kibali utumishi kimekuja kutoka 2013 mwishoni na sasa nipo job.
Ukiwaambia imekula kwako.

Mkuu naomba mawasiliano yako unipe uzoefu kidogo.
 
Habari wanajamii!

Mimi ni HoD katika taasisi moja ya serikali, inayojihusisha na utoaji wa elimu ya juu Jijini DSM, huko nyuma tuliwai kuomba ofisi ya Rais Utumishi wa umma, kutangaza nafasi za kazi ambazo zipo wazi hapa ofisini kwetu, nyingi zake zikiwa ni walimu, na chache zilikuwa za watu wa utawala!

Baada ya mchakato wa kutangaza na hatimaye waombaji kuitwa na tume katika APTITUDE TEST, ikaja zamu ya Oral interview na Practical interview kwa upande wa walimu! Mimi nilikuwa memba wa interview panel wa taasisi nikishirikiana na wale maofisa kutoka utumishi!

Cha kusikitisha ni namna watanzania wenzangu wasivokuwa na umakini katika masuala muhimu kama utafutaji wa ajira na hasa interview, ama niseme sijui ni masihara ama uswahili wetu! Makosa mengi yalifanywa na wahojiwa kiasi cha kunitia simanzi mle ndani ya INTERVIEW PANEL, huku nikichoka kwa kujua upuuzi wote ule, wametoka katika vyuo vyenye majina makubwa hapa nchini! Baadhi ya makosa yaliofanywa na waombaji kazi ni haya hapa:

  1. Wengi walikuwa na maelezo marefu sana, tena yasiyo ya msingi ktk swali la kwanza kwa kila muulizwaji. Wote walianza kwa kuulizwa: "Tell us about your historical background" Yaani hapa watu walibwabwaja, aiseeee1 watu wakataja mpaka wanasiasa, wakataja vyama, idadi ya watoto, wengine wakataja hadi mambo ya ndoa, kuna waliotaja hobby zao, yaaani maelezo mengi mpk huruma! walichemka vibaya!
  2. Hii nchi kuna urasimu sana kama uliwahi ama bado unafanya kazi serikalini, na kisha ukaomba kazi sehemu nyingine, serikalini! katika interview ile, sijui ni kutokujua (nimewasamehe) ama ni kupenda sifa, wasailiwa walikuwa na mbwembwe sana wakati wakujibu swali hili! Katika panel niliokuwepo, kati ya wasailiwa 15, 7 walisema wamewahi ama wanafanya kazi serikalini, afisa utumishi kutoka UTUMISHI aliwadisqualify kuendelea na interview wasaliwa wa aina ile, on the spot!
  3. Wengi hawakutii agizo la kwamba kama wapo na kazi ya serikali, wapitishe maombi yao kwa waajiri wao! Hii iliwagharinu ktk ukumbi wa interview!
  4. Ushamba na dharau! kuna walioambiwa watengeneze SLIDES not less than 10 ndani ya 1 hour, kwa topic aipendayo msailiwa, bado watanzania wenzangu, kuna wasailiwa waliandaa slides 3, wengine 2, kuna jamaa na Masters yake nje, aliandaa slide 1 tu, ya Mathematics! Katika dunia ya leo skills za computer ni muhimu sana, unamuelewaje mtu mwenye Masters ambaye hata kuandaa slide 10 ndani ya lisaa 1 hawezi!
  5. UREMBO! Kosa hili lilinishangaza sana. Kuna bidada, msailiwa alikuwa mrembo, na alikuwa na mvuto kusema ukweli. Panel ilikuwa na wanaume wote, watano, sasa sijui yeye alikuwa na akili gani kichwani mwake kuhusu wanaume sisi, wakati woote wa maswali ya oral alikuwa na pozi, sijawahi ona hapa Dsm! Pozi mbele ya interview panel. Alikuwa anafanyiwa usaili wa kuwa assistant tutor, aisee wakati anapresent, tulikoma na swaga zake! mara kashika nywele, mara min kaivuta juu, mara kavua miwani, mara kaivaa! mara ananyata pale mbele, mara hereni zinawasha! mara scarf sijui inalegea, sijui inabana shingo! Tulitamani amalize dakika zake 30, aende zake!
  6. Muda! Kama kawaida yetu! wapo waliochelewa, na walipofahamishwa kuwa wamechelewa wakaanza kwa kuangua vilio!
  7. Mara nyingi, kila mwisho wa interview, msailiwa huulizwa kama ana swali ama maoni kwa panel! wengi hawakuuliza swali wala kutoa maoni yao! Kilinivutia kitu kimoja, wachache waliouliza, walikuwa wanaulizia maslahi na hasa Mshahara! Kwamba mshahara ni Tshs ngapi na kama kuna marupurupu mengine! Sikuweza kuelewa mara 1 kuwa walikuwa wana maana gani (mtanisamehe kama mimi nimewaelewa vibaya) kutaka kujua mshahara, kwa mimi nijuavyo, mshahara wa serikali huwa hauna room ya kubargain, sasa kama alishaapply, akafanya interview ya kwanza, na akaja interview ya pili, swali hili sikuweza kujuwa logic yake hata!

WaTanganyika wenzangu na hasa, wale wanaotafuta kazi za serikali, naomba tuwe makini na hizi mambo, maisha ya mtaaani ni magumu, wasio na ajira ni wengi sana, tupunguze masihara na mizaha yetu tuliozoea, tuongeze umakini katika hili!

Mwenye sikio na asikie!

Mkuu sijawahi kufanya interview na hawa jamaa ila naomba kujua, hilo lakuandaa slides. Je unaruhusiwa kua/kutumia reference material, mfano kitabu internet wakati una andaa hizo slide au it should be directly from your head.
 
katika intervie yetu, yule afisa kutoka utumishi wa umma alikuwa anawatoa nje, kisha kuna form, naweza kuita ya scored marks, tulikuwa tunajaza NIL, sehemu zote, kisha ktk comments tulikuwa tunaandika "government employee" huku na yeye msailiwa akiondolewa katika mchakato!

Lakini kuna ambao, walifanya mpaka mwisho wa interview, lakini hiyo comment inawamaliza!

Asante sana kwa huu uzi mkuu umenifumbua mengi, je kama umeajiriwa katika private pia barua inatakiwa ipitie kwa mwajiri?
 
Mkuu sijawahi kufanya interview na hawa jamaa ila naomba kujua, hilo lakuandaa slides. Je unaruhusiwa kua/kutumia reference material, mfano kitabu internet wakati una andaa hizo slide au it should be directly from your head.

Unapoandaa slide unakuwa computer room ambapo hurusiwi kutoka kwa hilo lisaa. Wala huingii na kitu chochote humo. Huo ni mtihani kaka.
 
Asante sana kwa huu uzi mkuu umenifumbua mengi, je kama umeajiriwa katika private pia barua inatakiwa ipitie kwa mwajiri?

Mkuu kwa private haina shida hata kidogo! uko free kusema, utumishi wanajua kuwa watu wng wanakacha private sector kwenda public sector!
 
Unapoandaa slide unakuwa computer room ambapo hurusiwi kutoka kwa hilo lisaa. Wala huingii na kitu chochote humo. Huo ni mtihani kaka.

Kaka utoke nje kufanya nn? slides 10 kwa lisaa 1 ni chache mno!
 
Mkuu sijawahi kufanya interview na hawa jamaa ila naomba kujua, hilo lakuandaa slides. Je unaruhusiwa kua/kutumia reference material, mfano kitabu internet wakati una andaa hizo slide au it should be directly from your head.

Mara nyingi hii practical ya presentation inawahusu tutors na ass. tutors, huwa wanakupa uhuru wa kuchagua topic wee mwenyewe! direct frm ur head!
 
Hongera slim5 kwa kutoa feedback ili watu wajue walipokosea. Ila nilitaka kujua wewe wakati wapata hiyo kazi ulipo, ulibakizwa tu tokea uanafunzi au ulifanyiwa interview ya style hiyo. Na kama leo ungekuwa ndio waitwa interview kama ya sasa kipindi kile cha nyuma, unadhani ungefanya tofauti na hawa waliokuja mbele yako?
 
Last edited by a moderator:
wanataka academic and employment history yako mpaka wakati huo wanakufanyia interview, na hapa ndio pale waliowahi ama wanaofanyakazi serikalini, ambao hawakupitisha barua za maombi kwa mwajiri, waliingia mtegoni prakatatumba

Hili ni sawa kabisa na ishu namba 7 kwenye listi yako

Unaanzaje kuuliza hili swali wakati CV zao mnazo? Unamuitaje kwenye interview mtu ambaye ni muajiriwa wa serikali kama CV yake alituma Kwako na ukaipitia?

Ina maana nyie ni wavivu wa kusoma which means hamkutimiza wajibu wenu.Haina maana kumuuliza mtu kitu ambacho kipo kwenye CV yake,kama lengo kutaka kujua uwezo wa kujieleza basi muulizeni swali linalo husu profession yake ambalo litahitaji yeye ajieleze na Si kuuliza obvious question kama hilo
 
Last edited by a moderator:
Unapoandaa slide unakuwa computer room ambapo hurusiwi kutoka kwa hilo lisaa. Wala huingii na kitu chochote humo. Huo ni mtihani kaka.

Thanks kaka nimekuelewa. Nilitaka kujua yasije kunikuta yakuandaa slide moja.
 
Mara nyingi hii practical ya presentation inawahusu tutors na ass. tutors, huwa wanakupa uhuru wa kuchagua topic wee mwenyewe! direct frm ur head!

Asante mkuu sasa nimeelewa. Kama unajua before its a kind easy.
 
Na sehemu ya kuuliza maswali unatakiwa uulize maswali gani?

Hahahaaa kama unataka kukariri hivi(just kidding).

Just to add on what Nyani ngabu mentioned,Kimsingi unatakiwa ujue malengo yako Katika career yako na namna hiyo organization inaweza kukufikisha katika hayo malengo yako while adding value to the organization.

Uliza Maswali ambayo yataonekana una plans za kujiongezea maarifa kwa manufaa ya ofisi Mfano kama wana utaratibu kusomesha elemu ya juu zaidi na training za muda mfupi.

Usiulize swali ambalo litaonyesha kuwa unajali sana masilahi ya kifedha.Pia unaweza kuuliza kiundani namna ya utendaji kazi wa taasisi husika na taratibu zao za promotion

Hayo ndio makubwa mbayo naya fahamu kwa uzoefu wangu mdogo
 
Hili ni sawa kabisa na ishu namba 7 kwenye listi yako

Unaanzaje kuuliza hili swali wakati CV zao mnazo? Unamuitaje kwenye interview mtu ambaye ni muajiriwa wa serikali kama CV yake alituma Kwako na ukaipitia?

Ina maana nyie ni wavivu wa kusoma which means hamkutimiza wajibu wenu.Haina maana kumuuliza mtu kitu ambacho kipo kwenye CV yake,kama lengo kutaka kujua uwezo wa kujieleza basi muulizeni swali linalo husu profession yake ambalo litahitaji yeye ajieleze na Si kuuliza obvious question kama hilo

Kaaa hivo hivo!
 
Hongera slim5 kwa kutoa feedback ili watu wajue walipokosea. Ila nilitaka kujua wewe wakati wapata hiyo kazi ulipo, ulibakizwa tu tokea uanafunzi au ulifanyiwa interview ya style hiyo. Na kama leo ungekuwa ndio waitwa interview kama ya sasa kipindi kile cha nyuma, unadhani ungefanya tofauti na hawa waliokuja mbele yako?

Binafsi huwa najifunza vitu vipya kutoka kwa wanaojua! Sioni shida kuwafuata watu na kuuliza ya yanayontatiza!
mara zote ninazoitwa ktk interview, huwa najiandaa nikijua hiyo ni hatua muhimu sana ktk maisha yng na familia kwa ujumla!
huwa naenda kuwaomba ushauri na uzoefu wa watu ninaowajua ambao wanafanyakazi ktk kada km ybg na wamepitia aina hii ya interview!
huwa na peruzi ktk mitandao kuona kama kuna kitu naweza kuongeza!
tatizo ss watanganyika ni wavivu, ama niseme hatuna umakini ktk mambo ya msingi!
mf:
ktk interview ile, kulikuwa na swali tulitaka Msailiwa aelezee anavoijua taasisi yetu kwa ufupi!
wapo baadhi hawakuweza, yaani hawajui hata vision na mission za org!
kuna mtu alishindwa kurefusha abbr ya jina la chuo chetu!
kwa kifupi, maandalizi muhimu!
 
Last edited by a moderator:
mkuu naomba uelezee vitu vinavyohitajika kwenye point namba 1.

Kwamba we hadi leo huijui background yako
umezaliwa wapi
una umri gani
shule ya msingi umesoma wapi na mwaka gan
sekondari.. High school.. Higher inst...
..Kwamba umewahi fanya kazi wpi.. Kada ipi...
N.k kutegemeana na hstoria yako na kazi uliyoomba
 
Hahahaaa kama unataka kukariri hivi(just kidding).

Just to add on what Nyani ngabu mentioned,Kimsingi unatakiwa ujue malengo yako Katika career yako na namna hiyo organization inaweza kukufikisha katika hayo malengo yako while adding value to the organization.

Uliza Maswali ambayo yataonekana una plans za kujiongezea maarifa kwa manufaa ya ofisi Mfano kama wana utaratibu kusomesha elemu ya juu zaidi na training za muda mfupi.

Usiulize swali ambalo litaonyesha kuwa unajali sana masilahi ya kifedha.Pia unaweza kuuliza kiundani namna ya utendaji kazi wa taasisi husika na taratibu zao za promotion

Hayo ndio makubwa mbayo naya fahamu kwa uzoefu wangu mdogo

Shukrani mkuu
 
Duh nami nimefaidika maana nami nimeomba kazi fulani utumishi kwa mara ya kwanza naamini hii itaongezea ujuzi wa presentation.
 
Haya mambo bwana! Wenye uwezo wa kufaulu vizuri interview na kufanya kazi kwa ufanisi hawaitwi, ila vilaza ndo wanaitwa.
 
Kwamba we hadi leo huijui background yako
umezaliwa wapi
una umri gani
shule ya msingi umesoma wapi na mwaka gan
sekondari.. High school.. Higher inst...
..Kwamba umewahi fanya kazi wpi.. Kada ipi...
N.k kutegemeana na hstoria yako na kazi uliyoomba

Ushaingia chaka wewe, umeambiwa education history na work experience, hizo umezaliwa wapi na umri kawaeleze RITA
 
Back
Top Bottom