Angalizo: Wanaoitwa interview na utumishi wa umma

Angalizo: Wanaoitwa interview na utumishi wa umma

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,441
Reaction score
38,417
Habari wanajamii!

Mimi ni HoD katika taasisi moja ya serikali, inayojihusisha na utoaji wa elimu ya juu Jijini DSM, huko nyuma tuliwai kuomba ofisi ya Rais Utumishi wa umma, kutangaza nafasi za kazi ambazo zipo wazi hapa ofisini kwetu, nyingi zake zikiwa ni walimu, na chache zilikuwa za watu wa utawala!

Baada ya mchakato wa kutangaza na hatimaye waombaji kuitwa na tume katika APTITUDE TEST, ikaja zamu ya Oral interview na Practical interview kwa upande wa walimu! Mimi nilikuwa memba wa interview panel wa taasisi nikishirikiana na wale maofisa kutoka utumishi!

Cha kusikitisha ni namna watanzania wenzangu wasivokuwa na umakini katika masuala muhimu kama utafutaji wa ajira na hasa interview, ama niseme sijui ni masihara ama uswahili wetu! Makosa mengi yalifanywa na wahojiwa kiasi cha kunitia simanzi mle ndani ya INTERVIEW PANEL, huku nikichoka kwa kujua upuuzi wote ule, wametoka katika vyuo vyenye majina makubwa hapa nchini! Baadhi ya makosa yaliofanywa na waombaji kazi ni haya hapa:


  1. Wengi walikuwa na maelezo marefu sana, tena yasiyo ya msingi ktk swali la kwanza kwa kila muulizwaji. Wote walianza kwa kuulizwa: "Tell us about your historical background" Yaani hapa watu walibwabwaja, aiseeee1 watu wakataja mpaka wanasiasa, wakataja vyama, idadi ya watoto, wengine wakataja hadi mambo ya ndoa, kuna waliotaja hobby zao, yaaani maelezo mengi mpk huruma! walichemka vibaya!
  2. Hii nchi kuna urasimu sana kama uliwahi ama bado unafanya kazi serikalini, na kisha ukaomba kazi sehemu nyingine, serikalini! katika interview ile, sijui ni kutokujua (nimewasamehe) ama ni kupenda sifa, wasailiwa walikuwa na mbwembwe sana wakati wakujibu swali hili! Katika panel niliokuwepo, kati ya wasailiwa 15, 7 walisema wamewahi ama wanafanya kazi serikalini, afisa utumishi kutoka UTUMISHI aliwadisqualify kuendelea na interview wasaliwa wa aina ile, on the spot!
  3. Wengi hawakutii agizo la kwamba kama wapo na kazi ya serikali, wapitishe maombi yao kwa waajiri wao! Hii iliwagharinu ktk ukumbi wa interview!
  4. Ushamba na dharau! kuna walioambiwa watengeneze SLIDES not less than 10 ndani ya 1 hour, kwa topic aipendayo msailiwa, bado watanzania wenzangu, kuna wasailiwa waliandaa slides 3, wengine 2, kuna jamaa na Masters yake nje, aliandaa slide 1 tu, ya Mathematics! Katika dunia ya leo skills za computer ni muhimu sana, unamuelewaje mtu mwenye Masters ambaye hata kuandaa slide 10 ndani ya lisaa 1 hawezi!
  5. UREMBO! Kosa hili lilinishangaza sana. Kuna bidada, msailiwa alikuwa mrembo, na alikuwa na mvuto kusema ukweli. Panel ilikuwa na wanaume wote, watano, sasa sijui yeye alikuwa na akili gani kichwani mwake kuhusu wanaume sisi, wakati woote wa maswali ya oral alikuwa na pozi, sijawahi ona hapa Dsm! Pozi mbele ya interview panel. Alikuwa anafanyiwa usaili wa kuwa assistant tutor, aisee wakati anapresent, tulikoma na swaga zake! mara kashika nywele, mara min kaivuta juu, mara kavua miwani, mara kaivaa! mara ananyata pale mbele, mara hereni zinawasha! mara scarf sijui inalegea, sijui inabana shingo! Tulitamani amalize dakika zake 30, aende zake!
  6. Muda! Kama kawaida yetu! wapo waliochelewa, na walipofahamishwa kuwa wamechelewa wakaanza kwa kuangua vilio!
  7. Mara nyingi, kila mwisho wa interview, msailiwa huulizwa kama ana swali ama maoni kwa panel! wengi hawakuuliza swali wala kutoa maoni yao! Kilinivutia kitu kimoja, wachache waliouliza, walikuwa wanaulizia maslahi na hasa Mshahara! Kwamba mshahara ni Tshs ngapi na kama kuna marupurupu mengine! Sikuweza kuelewa mara 1 kuwa walikuwa wana maana gani (mtanisamehe kama mimi nimewaelewa vibaya) kutaka kujua mshahara, kwa mimi nijuavyo, mshahara wa serikali huwa hauna room ya kubargain, sasa kama alishaapply, akafanya interview ya kwanza, na akaja interview ya pili, swali hili sikuweza kujuwa logic yake hata!

WaTanganyika wenzangu na hasa, wale wanaotafuta kazi za serikali, naomba tuwe makini na hizi mambo, maisha ya mtaaani ni magumu, wasio na ajira ni wengi sana, tupunguze masihara na mizaha yetu tuliozoea, tuongeze umakini katika hili!

Mwenye sikio na asikie!
 
Cjakuelewa ulialikwa katika panel ya usaili au manake ajira za serikali haziwi outsourced
 
point number 1 umetuzingizia sisi watafutaji. hakuna anaejibu hivyo siku hizi bwana.
 
mkuu naomba uelezee vitu vinavyohitajika kwenye point namba 1.

wanataka academic and employment history yako mpaka wakati huo wanakufanyia interview, na hapa ndio pale waliowahi ama wanaofanyakazi serikalini, ambao hawakupitisha barua za maombi kwa mwajiri, waliingia mtegoni prakatatumba
 
Last edited by a moderator:
wanataka academic and employment history yako mpaka wakati huo wanakufanyia interview, na hapa ndio pale waliowahi ama wanaofanyakazi serikalini, ambao hawakupitisha barua za maombi kwa mwajiri, waliingia mtegoni prakatatumba

brother, kuna siku hao jamaa wa utumishi waliniuliza ilo swali, tell us about your self, tena waka specify education background and work experience, basi.... katika kujibu, nikawa nasema na responsibilities zangu katika hizo kazi, jamaa wakakataa wakasema tunataka work na edu baasi, sasa mkuu, uwa exactly mnataka tujibuje?
 
Last edited by a moderator:
ulitaka kusema nini?

Sio nilitaka kusema. Nimeandika.

Watu hao hao waliosemwa na mukulu hapo juu kuhusu wanavyochemka katika usaili nao watalalamika kwamba wanafanya usaili mara nyingi lakini kazi hawapati.

Our education is suffering from the "tragedy of the commons" phenomena.
 
uko sahihi mkuu ,kweli maisha mtaani ni magumu sana unapokuwa huna-ajira ..linapotokea jambo la kupata ajira yatubidi tujitaidi kwa juhudi na maarifa yote ili tupate ajira....Haswa kwenye huo mtego wa usaili yatupasa kujiandaa kama unapojianda na mtihani wa UE
 
baadhi ya mambo unayotakiwa uzingatie wakati wa oral interview
1.usivute sigara wakati wa usaili
2.watazeme machoni wasaili
3.tulia...relax
4.usimuite msaili kwa jina la kwanza
5.sema yes siyo yeah"
6. usiwe na miguno ahs" na umms"
7.usiomba msamaha juu ya ukosefu waexperience
8.usitafune jojo
9.toa leseni na vyeti wape
10.uliza maswali baada ya usaili
 
uko sahihi mkuu ,kweli maisha mtaani ni magumu sana unapokuwa huna-ajira ..linapotokea jambo la kupata ajira yatubidi tujitaidi kwa juhudi na maarifa yote ili tupate ajira....Haswa kwenye huo mtego wa usaili yatupasa kujiandaa kama unapojianda na mtihani wa UE

Yaaaah! Hebu fikiria mkuu, yupo jamaa mmoja, alipotakiwa kutoa original certificates, kasema hana, amebeba copie tu! Kisha anabisha na kujitetea kuwa hakuna mahali katika waajiri wanataka original, kwa nini yeye atoe/aonyeshe original! Huyu unamchukuliaje?
 
baadhi ya mambo unayotakiwa uzingatie wakati wa oral interview
1.usivute sigara wakati wa usaili
2.watazeme machoni wasaili
3.tulia...relax
4.usimuite msaili kwa jina la kwanza
5.sema yes siyo yeah"
6. usiwe na miguno ahs" na umms"
7.usiomba msamaha juu ya ukosefu waexperience
8.usitafune jojo
9.toa leseni na vyeti wape
10.uliza maswali baada ya usaili

ahsante kwa nyongeza!
 
asante sana mkuu kwa kutupa elimu murua tena ya bure. hasa ulivyofafanua kwenye kosa namba moja na namba 7. Ubarikiwe
 
Yaaaah! Hebu fikiria mkuu, yupo jamaa mmoja, alipotakiwa kutoa original certificates, kasema hana, amebeba copie tu! Kisha anabisha na kujitetea kuwa hakuna mahali katika waajiri wanataka original, kwa nini yeye atoe/aonyeshe original! Huyu unamchukuliaje?

mtu kama huyo kwa kweli hukuna namna kwa wasaili (interviewer) inabidi kumuweka kando ili wenye shida na ajira wapate nafasi....huwezi kwenda kwenye usaili wowote duniani bila kuwa na original certificate
 
Back
Top Bottom