DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Natoa angalizo hili kwa nia njema kabisa kwa klabu ya Simba SC.
Klabu ya Simba inapoelekea katika mechi ya kesho na kama Mungu atajaalia ikaingia fainali, ijihadhari sana sana na kujiingiza katika mitego ya kisiasa.
Ni jambo moja kuishukuru serikali kwa mchango wake wa hapa na pale katika timu ila mtu wa kwanza anayefanikisha mafanikio ya Simba siyo serikali, siyo viongozi, siyo benchi la ufundi na unaweza kusema hata siyo mchezaji. Mtu wa kwanza ambaye ni chachu ya mafanikio ya Simba ni mashabiki wa Simba. Huyu muilinde sapoti yake kwa wivu mkubwa sana.
Wote tunajua kwamba siasa zetu sasa hivi zipo katika hali tete. Simba ina mashabiki smart sana, wana uwezo wa kung'amua pale kunapoonekana kuna agenda zingine nyuma ya pazia ambazo zinapitishwa kupitia klabu yao. Tusiwakwaze hawa maana mashabiki wana hisia zinazotofautiana sana.
Nawahusia sana viongozi wawe makini sana katika hili. Mkikosea kidogo katika hili mnaweza kupoteza sapoti ya mashabiki na kuja kurekebisha hili itachukua muda mrefu sana na wale ambao walihusika katika upotevu huo watakaa pembeni mpambane na hali zenu.
Nadhani wote mnaosoma bandiko hili ni watu wazima na nimeeleweka vizuri bila kwenda kwenye "specifics". Ni ushauri ninaotoa kwa nia njema ya klabu ya Simba.