Angalizo: Usinunue Chombo Cha moto kama huna fundi wako

SaulGoodman

JF-Expert Member
Nov 12, 2020
351
792
Habari za majukumu wandugu, poleni na hongerani katika majukumu ya kujijenga na kulijenga Taifa. Naomba sasa niende kwenye mada husika.

Mimi ninamiliki usafiri wa gari aina ya Toyota Cami. Sasa Jana kwa bahati mbaya wakati natoka mishemishe naendesha then gafla gari ika "corrupt" na kuzima. Kila nikijaribu kupiga starter wapii kitu haiwaki, basi nikafanya utaratibu nikavutwa mpaka karibu na mitaa ninakoishi kwa fundi garage ambaye nilikua nikimfahamu. Basi kwa kua ilikua usiku na nimechoka akaniambia niiache ilale then kesho nije mapema tushughulikie. Kesho yake yaani Leo mapema nikawahi ofisini kwake, katika kuangalia angalia tatizo akaniambia tatizo ni "valve chaser" imekufa, hivyo inahitajika nyingine. Nikamuuliza ni kiasi gani itagharimu akaniambia sh laki tatu na nusu, daah kwa kweli nilishtuka na kunyong'onyea nikijaribu kumuuliza kuwa haiwez kutengenezwa iyo iliyoharibika ikafaa, Mimi sio mtaalamu wa ufundi wa magari hivyo nilikua nikizungumza hivyo kwa lengo la kutoka hizo gharama ambazo ni nyingi kwangu alafu zimekuja ghafla.

Fundi akasisitiza kua ni lazima ifungwe "valve chaser" nyingine na gharama yake ndo hiyo. Basi karibu na ofisi yake pale Kuna maduka mawili matatu ya spair nikamwambia sawa Wacha nikaulize madukani pale karibu, basi nikaenda bahati mbaya dukan Moja tu ndo lilikua na ile valve chaser na gharama yake ni ileile laki tatu na nusu fundi aliyoniambia. Nikawa nimeshakubali Sina la kufanya, Ila ghafla wazo likanijia, Kuna mwanangu mmoja yeye ni dereva uba nikasema Wacha nimuulize kama atafahamu. Kweli mwanangu akaniambia nimpe kama dk 20 afanye kuchek na watu wake alafu atanirudia. Baada ya dk kama 10 Jamaa yangu akanivutia waya kuniuliza "iyo Cami yako inatumia pressure au umeme?". Eeh mi hata sielew kitu hapo ikabidi nimwambie asubiri kidogo nimuulize fundi Ila wakati huo yeye aniulizie gharama za zote mbili. Kweli mi nikamfata fundi kumuuliza hii gari yangu inatumia umeme au pressure? Fundi akanijibu inatumia umeme. Mda haukupita Jamaa akanitumia sms kuwa "ya umeme laki Moja na ya cable ni laki na nusu".

Baada ya kusoma ile sms nilijikuta nina furaha na hasira kwa wakati mmoja. Basi nikamwambia fundi nimepata sehemu naifahamu bei yake ni nafuu kidogo Wacha niende, fundi akawa mdadisi kujua bei ya huko ninakokwenda Ila nikamkataa kiaina nikamwambia asijali maana naelekea hukohuko town Kuna mishe nachek then nageuka haraka. Sikuona haja ya kuanza kugombana nae kwamba alikua anataka kunipiga pakubwa sababu gharama halisi nilisha zifahamu. Gari ingekua Ina tembea ningeondoka nayo Ila kwavile haikua inatembea basii, niliiacha pale nikaenda kufuata Kifaa nikarudi akafunga nikampa ya ufundi nikaondoka na gari.

Nimekuja kuona ni muhimu sana kutafuta fundi mapema kabla tatizo na gari yako halijatokea. Tena tafuta mwaminifu, na hapo ndo changamoto kumpata maana wengi ni wapigaji haswaa. Tena akijua wewe hufahamu kabisa kuhusu ufundi ndio inakua tatizo kubwa zaidi kwako. Ni ushauri wangu tu.

Unaweza pia tushirikisha kama umewahi pitia changamoto kama yangu, na je uliingizwa mkenge au ulifanikiwa kuchomoka. Na unatumia mpango mkakati upi kuhakikisha halijirudii jambo kama Hilo?

Screenshot_20230412-210259~3.png
 
View attachment 2585723
Hata huyo wa laki moja naye kapiga cha juu kimtelezo , mana mazingira mazuri aliyaseti wa laki tatu na nusu
 
Mleta Mada, ogopa mtu anayeitwa fundi wangu au fundi wa family. Ogopa sana sana hao watu usiwaamini kamwe.

Anyway pole sana sana
Tunawafuata hawa watu tukiwa na Imani kwamba tunapokua wateja wao wa kudumu basi tutapata huduma Bora kwa bei nafuu pamoja na uaminifu
 
Back
Top Bottom