Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,804
- 1,871
Asiyesikia la mkuu huvunjika guu na asiyeweza kujifunza kutokana na makosa yaliyopita mathalan hawezi kujifunza lolote huko mbeleni. Misemo hii si ya kuipuuzia hasa katika mwenendo wetu wa siasa wa awamu hii.
Nimemsikia Zitto akimsafisha Membe na kumtofautisha na Lowassa na kuwahakikishia wananchi kutokuwa na wasi wasi na huyu Mbobezi. Kwa mara ya kwanza Mahesabu na akili nyingi za Zitto zitaonekana kuwa ndogo kuliko zile za chama Tawala. Kwani kama kweli Membe anaugomvi na chama tawala hata waandishi wa habari asingeruhusiwa kukutana nao. Na kimsingi angewekwa kizuizini au tusingemuona kabisa. Historia imeonyesha hivyo!
Kwanini Membe ni Hatari?
Hivyo upinzani wanaweza kumkubalia kuwa mwanachama wa kawaida lakini asipewe kugombea hata ubunge au uenyekiti wa jimbo. Hizo ndio habari za mjini ukipenda Breaking News!

- Membe ni mtu aliyekulia ndani ya chombo nyeti toka akiwa na miaka 23, hivyo anaielewa Tanzania na chama kuliko Lowassa. Katika nchi yeyote ile watu kama hao hawaachwi wakaropokaropoka ovyo kama si kwa maslahi ya watawala.
- Kama kweli chama tawala wangetaka kumfukuza Membe uwanachama wangeshaitisha kikao cha halmashauri kuu na kumfukuza Membe Rasmi na kumpatia barua ya kufukuzwa kwake. Kwanini hawafanyi hivyo? Ni kwasababu ya kuunyambulisha mjadala na kumfanya Membe awe kivutio zaidi kwa wapinzani.
- Kuwapata watu waasi ndani ya chama tawala
- Kuuangalia kasi ya upinzani kama wamestuka kwa yale ya Lowassa au bado wapo gizani. Kwa vile bado wanachukua data.
Hivyo upinzani wanaweza kumkubalia kuwa mwanachama wa kawaida lakini asipewe kugombea hata ubunge au uenyekiti wa jimbo. Hizo ndio habari za mjini ukipenda Breaking News!