Angalizo kwa wanunuzi wa Colgate

Angalizo kwa wanunuzi wa Colgate

Tupe mtazamo wa boksi la original bro',pia hizo original zipo maduka yapi hapa mjini,ndio maana wengi wetu vinywa vinatoa harufu isiyo rafiki kwa jirani zetu,siku njema na ubarikiwe kwa elimu nzuri
 
Bora Bib yangu alinfundsha matumiz ya mkaa kupigia mswaki
 
Habarini.

Leo nimeona nishare nanyi jambo muhimu sana kuhusu afya ya kinywa.

Naamini sisi sote huwa tunapiga mswaki kama tunavyo elekezwa na madaktari wa kutibu magonjwa ya kinywa.

Na katika kusafisha kinywa moja ya vitu tunatumia ni miswaki imara na dawa bora ya meno. Kwa wale mlioishi miaka ya nyuma kuanzia sabini mtaungana nami juu ya ukweli kwamba kabla hata ya madawa mengine ya meno haya ya sasa kama whitedent, sensodyme, forever na nyinginezo, alikuwapo dawa moja mwamba ambaye hadi leo hanaga mpinzani wa uhakika. Huyu si mwingine bali ni dawa Colgate.


Hii dawa imekuwapo kwa vizazi ikitetea ubora wake katika kuwa na standard inayotakiwa ya dawa bora ya meno. Kwa hapa afrika, dawa hii yenye hadhi ya kimataifa na yenye soko dunia nzima inatengenezwa hapo South Afrika na kampuni ya Colgate Palmolive.

Ila nasikitika asilimia 90% ya colgate zilizopo madukani ni mzigo kutoka kwa watengenezaji fake ambao hawana kibali kamili cha kutengeneza colgate yenye ubora ule wa kimataifa. Kwa kifupi, Colgate nyingi zilizopo hapa madukani ni feki na ninasikitika sana hata sisi wateja au watumiaji wa brand hii murua tumeshindwa kuchukua hatua na kupiga vita uvamizi huu wa ubora kwa kukubali hizi sumu feki zisambae madukani bila kueleimisha uma wa watanzania juu ya ubora halisi wa Colgate original ambayo imetufanya leo hadi umri huu tuwe na meno imara ambayo hayajaharibiwa na wadudu na kutupa usalama murua ambao unatuwezesha hata kuongea na mpenzi wako mkitizamana usoni kinywa kikiwa swafi kabisa.


Naomba tuelimishane hapa kuwa kuna viashiria ambavyo huonyesha hii dawa si yenyewe.

1. Kwanza, Colgate original huwa na boksi lenye mlango ambao unaweza kufungua na kisha kuifunga yaani haujawekewa gundi.

Colgate feki ipo tofauti, boksi lake milango yake imesilibwa na gundi kabisa, ukichana ni umenunua na si ya kurudisha kwenye shelfu tena.

Nadhani wanafanya hivi ili kuzuia wale wanaoifahamu kama mimi kuibaini kabla hawajainunua. Mfano mimi nikilamba tu pale pale dukani na kuinusa naiweza kuibaini hii ni Colgate feki ila wasio zijua vema wananunua na kuwatajirisha hawa wezi wetu wanaotuuzia dawa feki.

So, kumbuka, linapokuja swala la boksi ya dawa ya Colgate, usijeukathubutu kununua yenye boksi ambalo mlango wake upo sealed na gundi na hauwezi ifungua na kuifunga na kuirejesha katika shelfu ya dukani hapo.


2. Boksi ya Colgate feki ina maelezo sawa kabisa na Colgate original ila tofauti yake ni kwamba hii feki itakosa Barcodes katika package yake.

Hii ina maana imetengenezwa na watu feki ambao hawakufanikiwa kuipitisha katika mikono safi ya watu wa procurement katika kiwanda chenyewe cha huko South Africa. Kama unabisha tafuta boksi isiyo na barcode halafu ukawalalamikie hao Colgate Palmolive kuwa bidhaa ni feki, watakapohitaji uwatumie hiyo bidhaa watagundua kuwa hiyo boksi ya Colgate haijapitia katika mikono ya maofisa ugavi wao katika hicho kiwanda na kusambazwa, maana wenzetu huwa wanazipa bidhaa zao barcode ili iwe rahisi kutrace inventory yao mara kunapotokea uharibifu wowote.

3. Alama ya ubora ya TBS. Hii huwa tunaambiwa kila uchao kuwa tusinunue bidhaa ambazo hazina hii alama....ingawa zipo ambazo huwa anafoji lakini ni chache sana na kuna udhibiti unafanyika hivi sasa katika kuzuia hii changamoto. Ukitazama boksi za Colgate feki huwa inakosa hii alama, na sababu ipo very obvious, kuwa ni bidhaa feki na hatarishi kwa usalama wa afya ya mwanadamu.

Hizi ni miongoni mwa alama chache nilizobaini na nina washauri wale watumiaji wa colgate original hebu tupige vita udhalimu huu lakini pia tuwakondeshe kwa kutokununua maana kwao hii ni biashara na sio swala la kiafya sasa tukiwakomoa watakosa soko na kutafuta bishara nyingine na kuacha upuuzi wao.

Hapa chini nitaambatanisha picha ya boksi ya Colgate feki ili muweze kutambua.
Ili iweje kama ata mademu wengi fake
 
Kwisha habari yetu
Ila kwa jinsi waafrika tulivo wagumu tutakufa kwa malaria/kipindupindu sio matokeo ya ubora duni wa Colgate
Bado natafuta....hauwezi amini hizi feki ndizo zimesambaa, nimepita maduka yote kila nikiulizia ile Colgate ya single action nyeupe.....naletewa hizi takataka feki.

Tbs mnakesi ya kujibu kwa kuzembea kuzibaini hizi dawa feki......


Bado natafuta kesho nitajihimu niende maeneo ya mjini kule nikacheki......

Sent from my Infinix HOT 4 using JamiiForums mobile app
 
Naomba urudie kuleta picha nzuri za bandiko lako. Tuwekee picha nzuri zenye kutofautisha picha ya colgate ya bandia na halisi.
Usipotuwekea, basi tutajua wewe ni mamluki wa kuharibu biashara za wenzako. Nadhani wewe ni Whitedent.
Mimi sijawahi ona Colgate inayofunguka bika kuharibu seal yake.
Kama hizi zilizopo na fake! basi wanaozitengeneza ni wazuri sana, tena wala hawahitaji kutumia brandy ya Colgate ni bora waweke brand yao watauza sana sana.
Mimi ni colgate damu tokea utoto.....na nikikuta sehemu wanatumia whitedent basi nitakwenda dukani na kutafuta Colgate yangu.....situmii dawa nyingine isipokuwa Colgate, au nikikosa Colgate basi nitatumia Close up.....

Sent from my Infinix HOT 4 using JamiiForums mobile app
 
Halafu hiyo colgate iko rojo sana kiasi inatia kinyaa kuweka mdomoni. Harufu ile ya colgate hamna. Hii ni chungu. Kuona hivyo mimi hutumia whitedent
 
Naomba urudie kuleta picha nzuri za bandiko lako. Tuwekee picha nzuri zenye kutofautisha picha ya colgate ya bandia na halisi.
Usipotuwekea, basi tutajua wewe ni mamluki wa kuharibu biashara za wenzako. Nadhani wewe ni Whitedent.
Mimi sijawahi ona Colgate inayofunguka bika kuharibu seal yake.
Kama hizi zilizopo na fake! basi wanaozitengeneza ni wazuri sana, tena wala hawahitaji kutumia brandy ya Colgate ni bora waweke brand yao watauza sana sana.
8631d84fd8bd7a5c7a0bd6c572b6dd02.jpg
 
Muongo huyo mamluki
Kuwa serious na maisha ya watu pumbavu wewe. Hivi me nikazane napiga picha makasha ya dawa niliyonunua na kubaini ni feki kwa faida ya nani sasa?!

Mimi hao Colgate hata wananijua kuwa ninaongelea bidhaa yao hapa. Hii sio bidhaa ya anasa/starehe kusema kwamba nikikaa kimya haitaleta madhara, hapa mimi nafanya uzalendo wa kushea na watanzania wenzangu juu ya swala la kiafya na sio ujinga unaouzungumzia wewe shuwaini mkubwa wewe.....
 
Mkuu sio Colgate tu hata Sabuni ya Dove na Nivea pamoja na lotion yake. Kuna jamaa analeta mzigo huo kutoka China bei yake huifanya mia mbili rahisi na halisia. Kuna watu matapeli kweli hapa hata hizi dawa za binaadamu asilimia kubwa wana copy kutoka China.
Hili swala sijajua TBS wanaplay part gani katika kubaini ubora halisi hadi zinatufikia wateja kama hivi?!

Mbali na kwamba ni hatarishi kwa afya lakini pia ni gharama maana kama mimi nimenunua hii dawa ila sitaitumia....
 
Huwa nazinunua kwenye maduka makubwa ya dawa but kwamba ni og au sio og ndio kitu nilikuwa sijui jinsi ya kuangalia hivyo nakushukuru sana mleta mada next tym nitazingatia hizi points ulizotoa hapa,waTanzania wengi sana tunatumia bidhaa fake sema ni vile tu hatujui.
Hii ni hatari sana....
 
Tupe mtazamo wa boksi la original bro',pia hizo original zipo maduka yapi hapa mjini,ndio maana wengi wetu vinywa vinatoa harufu isiyo rafiki kwa jirani zetu,siku njema na ubarikiwe kwa elimu nzuri
Nitapost muda si mrefu aina ya box ya original inatakiwa kuwa.....
 
Wenzetu vijana wa bavicha watapinga. Maana ndio desturi yao na kuitupia lawama serikali. Kwa niaba ya wenzetu kutoka ufipani, Tunashukuru sana kwa msaada.
 
Vipi za thailand malaysia na uarabuni ambazo zimejaa supermarket na hazijawa manufactured South Africa?
 
Back
Top Bottom