Angalizo kwa wanunuzi wa Colgate

Angalizo kwa wanunuzi wa Colgate

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,093
Reaction score
22,806
Habarini.

Leo nimeona nishare nanyi jambo muhimu sana kuhusu afya ya kinywa.

Naamini sisi sote huwa tunapiga mswaki kama tunavyo elekezwa na madaktari wa kutibu magonjwa ya kinywa.

Na katika kusafisha kinywa moja ya vitu tunatumia ni miswaki imara na dawa bora ya meno. Kwa wale mlioishi miaka ya nyuma kuanzia sabini mtaungana nami juu ya ukweli kwamba kabla hata ya madawa mengine ya meno haya ya sasa kama whitedent, sensodyme, forever na nyinginezo, alikuwapo dawa moja mwamba ambaye hadi leo hanaga mpinzani wa uhakika. Huyu si mwingine bali ni dawa Colgate.


Hii dawa imekuwapo kwa vizazi ikitetea ubora wake katika kuwa na standard inayotakiwa ya dawa bora ya meno. Kwa hapa afrika, dawa hii yenye hadhi ya kimataifa na yenye soko dunia nzima inatengenezwa hapo South Afrika na kampuni ya Colgate Palmolive.

Ila nasikitika asilimia 90% ya colgate zilizopo madukani ni mzigo kutoka kwa watengenezaji fake ambao hawana kibali kamili cha kutengeneza colgate yenye ubora ule wa kimataifa. Kwa kifupi, Colgate nyingi zilizopo hapa madukani ni feki na ninasikitika sana hata sisi wateja au watumiaji wa brand hii murua tumeshindwa kuchukua hatua na kupiga vita uvamizi huu wa ubora kwa kukubali hizi sumu feki zisambae madukani bila kueleimisha uma wa watanzania juu ya ubora halisi wa Colgate original ambayo imetufanya leo hadi umri huu tuwe na meno imara ambayo hayajaharibiwa na wadudu na kutupa usalama murua ambao unatuwezesha hata kuongea na mpenzi wako mkitizamana usoni kinywa kikiwa swafi kabisa.


Naomba tuelimishane hapa kuwa kuna viashiria ambavyo huonyesha hii dawa si yenyewe.

1. Kwanza, Colgate original huwa na boksi lenye mlango ambao unaweza kufungua na kisha kuifunga yaani haujawekewa gundi.

Colgate feki ipo tofauti, boksi lake milango yake imesilibwa na gundi kabisa, ukichana ni umenunua na si ya kurudisha kwenye shelfu tena.

Nadhani wanafanya hivi ili kuzuia wale wanaoifahamu kama mimi kuibaini kabla hawajainunua. Mfano mimi nikilamba tu pale pale dukani na kuinusa naiweza kuibaini hii ni Colgate feki ila wasio zijua vema wananunua na kuwatajirisha hawa wezi wetu wanaotuuzia dawa feki.

So, kumbuka, linapokuja swala la boksi ya dawa ya Colgate, usijeukathubutu kununua yenye boksi ambalo mlango wake upo sealed na gundi na hauwezi ifungua na kuifunga na kuirejesha katika shelfu ya dukani hapo.


2. Boksi ya Colgate feki ina maelezo sawa kabisa na Colgate original ila tofauti yake ni kwamba hii feki itakosa Barcodes katika package yake.

Hii ina maana imetengenezwa na watu feki ambao hawakufanikiwa kuipitisha katika mikono safi ya watu wa procurement katika kiwanda chenyewe cha huko South Africa. Kama unabisha tafuta boksi isiyo na barcode halafu ukawalalamikie hao Colgate Palmolive kuwa bidhaa ni feki, watakapohitaji uwatumie hiyo bidhaa watagundua kuwa hiyo boksi ya Colgate haijapitia katika mikono ya maofisa ugavi wao katika hicho kiwanda na kusambazwa, maana wenzetu huwa wanazipa bidhaa zao barcode ili iwe rahisi kutrace inventory yao mara kunapotokea uharibifu wowote.

3. Alama ya ubora ya TBS. Hii huwa tunaambiwa kila uchao kuwa tusinunue bidhaa ambazo hazina hii alama....ingawa zipo ambazo huwa anafoji lakini ni chache sana na kuna udhibiti unafanyika hivi sasa katika kuzuia hii changamoto. Ukitazama boksi za Colgate feki huwa inakosa hii alama, na sababu ipo very obvious, kuwa ni bidhaa feki na hatarishi kwa usalama wa afya ya mwanadamu.

Hizi ni miongoni mwa alama chache nilizobaini na nina washauri wale watumiaji wa colgate original hebu tupige vita udhalimu huu lakini pia tuwakondeshe kwa kutokununua maana kwao hii ni biashara na sio swala la kiafya sasa tukiwakomoa watakosa soko na kutafuta bishara nyingine na kuacha upuuzi wao.

Hapa chini nitaambatanisha picha ya boksi ya Colgate feki ili muweze kutambua.
 
a1a9a0312d93456bbab028f5ecce27ed.jpg
 
Tazama gundi katika huo mlango, pia tazama aina ya mlango huo wa boksi hauwezi jifunga bila gundi, colgate original ina mlango ambao unaweza funga na kufungua na kufunga tena.....

Hii ni boksi ya Colgate fake, ukifungua hiyo seal ya gundi ndio mazima lazima uondoke nayo hapo dukani maana ni feki
 
Kwisha habari yetu
Ila kwa jinsi waafrika tulivo wagumu tutakufa kwa malaria/kipindupindu sio matokeo ya ubora duni wa Colgate
 
Kweli Colgate fake haina povu vizuri. Ila ulipata OG utafurahi. Mdomo fresh 24/7
 
Mm siku zote natumia Colgate Herbal, hii ni Nzuri na nyingi hazijachakachuliwa
 
Naomba urudie kuleta picha nzuri za bandiko lako. Tuwekee picha nzuri zenye kutofautisha picha ya colgate ya bandia na halisi.
Usipotuwekea, basi tutajua wewe ni mamluki wa kuharibu biashara za wenzako. Nadhani wewe ni Whitedent.
Mimi sijawahi ona Colgate inayofunguka bika kuharibu seal yake.
Kama hizi zilizopo na fake! basi wanaozitengeneza ni wazuri sana, tena wala hawahitaji kutumia brandy ya Colgate ni bora waweke brand yao watauza sana sana.
 
Mkuu sio Colgate tu hata Sabuni ya Dove na Nivea pamoja na lotion yake. Kuna jamaa analeta mzigo huo kutoka China bei yake huifanya mia mbili rahisi na halisia. Kuna watu matapeli kweli hapa hata hizi dawa za binaadamu asilimia kubwa wana copy kutoka China.
 
Huwa nazinunua kwenye maduka makubwa ya dawa but kwamba ni og au sio og ndio kitu nilikuwa sijui jinsi ya kuangalia hivyo nakushukuru sana mleta mada next tym nitazingatia hizi points ulizotoa hapa,waTanzania wengi sana tunatumia bidhaa fake sema ni vile tu hatujui.
 
Back
Top Bottom