Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,722
Wanabodi,
Huu ni wito wangu kwa wana jf wenzangu, Tuwaepuke "Manabii wa Majanga", Prophets of the doom" ambao kazi yao ni kuwanyooshea vidole wenzao na kuwahukumu pasipo uthibitisho, kila kunapotokea tukio baya, na kuwaombea wenzao majanga ikiwemo kuwaombea vifo, au kuwatabiria kifo.
Unapomuombea janga mwenzako, wewe bila kujua, kumbe ndio unajichumia janga kwako au kwa uwapendao as a karma reaction kwa mabaya uliomuombea au kumtabiria kifo mwenzako kwa kutumia kanuni ya tatu ya Newton law of motion isemayo "for every force, there is an equal and opposite reaction, pulling towards that force", yaani kila jema unalowaza, unalopanga, unalosema na unalotenda kwa wengine, litatengeneza karma nzuri ya mema (positive good karma power) ambayo mema hayo uliowaza, uliopanga, uliosema na uliotenda, yatakurudia wewe na kizazi chako, na kila janga,unalowaza, unalopanga, unalosema, unalotenda kwa wengine, linategeneza a bad karma (karma mbaya) ya majanga (negative bad karma power) hivyo majanga hayo yatakurudia wewe na uzao wako!. Tusiwaombee wenzetu majanga, ili tusijichumie majanga!.
Wito huu ni kufuatia kuongezeka kwa threads ambazo haziliombei mema taifa letu na viongozi wake na nyingine kuwaombea hadi vifo wale tunaowahisi ni wabaya wetu. Kwa dini zote, amri kuu kuliko zote ni upendo, kwa jinsi ile Mungu alivyotupenda sisi hadi.... vivyo hivyo nasi tupendane, hata adui mpende, kama ni adhabu, adui yako ataadhibiwa na Mungu kupitia karma ya matendo yake!.
Kauli huumba, hivyo tusishabikie sana kauli zenye negativity na kujikuta kumbe ni sisi tuna sababisha hizo negatives kwa kuziumba kwa kauli zetu. Badala yake tuwe positive kwenye kila jambo, hata tukihisi jambo fulani sio jema, tutumie kitu kinachoitwa affirmatives kubadili negatives kuwa positives.
Miongoni mwa kauli hizi za hawa Prophets of the doom wa humu jf, ni pamoja na kuwatabiria vifo vya ajabu ajabu wenzao, wakiwemo viongozi wetu!. Tusishangilie majanga yoyote kwa binadamu wenzetu, hata hawa viongozi wetu sio miungu watu hawa ni binadamu tuu kama sisi hivyo hata wakiwa ni watu wabaya kiasi gani, hata wakiwa na mioyo ya kishetani kiasi gani, hata watutendee maovu kiasi gani, sisi tuwaombee tuu mema, tuwaombee mafanikio na kuwaombea afya njema na waishi maisha marefu hapa duniani na sio kuwaombea kifo, halafu kama kuna maovu wameyatenda, sisi tusiwahukumu, tusije tukahukumiwa, kazi ya kuwahukumu kwa matendo yao, tumwachie Mungu mwenyewe ambaye ndiye Hakimu Mkuu, na hukumu yake ni kupitia kitu kinachoitwa karma, ambapo kila mmoja wetu atahukumiwa kwa matendo yake, ukitenda mema, utalipwa mema, ukitenda uovu au ubaya, utalipwa uovu au ubaya!.
Ila maisha yameumbwa na kifo pia kumeumbwa, kila mtu ni lazima atakufa siku yake ikifika tena atakufa kifo kile kile alichopangiwa na Mungu ile siku anazaliwa, hivyo tusimtabirie yoyote kifo, tusimuombee yoyote kifo, uhai na kifo ni chini ya mamlaka ya Mungu pekee na sio sisi binadamu.
Haijalishi mtu atakufaje, ila malaika mtoa roho Israel humpitia kila kiumbe humu duniani mara 7x 70 ( saba mara sabini) kila siku ili kuhakikisha saa yake ikifika, hazidishi hata nukta moja ya sekunde, kifo ni kazi ya Mungu hatuna haja kutabiriana vifo humu na wengine hadi kuombea vifo wengine, kwa kufanya hivyo wengine bila kujijua kuwa kumtabiria mwenzako kifo au mabaya ni kujiombea wewe mwenyewe kifo au mabaya hayo kwa kanuni ya karma ya what goes around, comes around kwa kufuata kanuni ya Newton ya every action, there is equal and opposite reaction.
Haijalishi mtu atakufaje, ila kwa yoyote na vyovyote atakavyokufa, kifo hicho ndicho alichoandikiwa na ndicho kilichopangwa ile siku anazaliwa, kwa sababu kuzaliwa na kifo ni mipango ya Mungu pekee. Hata shetani akipanga mipango miovu vipi, kama Mungu hajaridhia, hata wapange vipi, kamwe hawatafanikiwa, kila binadamu atakufa saa ile tuu aliyoandikiwa na kifo kile tuu alichopangiwa kwa mipango ya Mwenyezi Mungu pekee.
Tupendane, tuombeane mema hata maadui zetu, tuwaombee mema hivyo kutengeneza positive karma effects.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa ...
Wasalaam.
Paskali