JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 5,012
Watu walio na hali hii huwa wana upungufu wa chembechembe nyekundu kwenye damu mwilini. Hivi ni kumaanisha kuwa miili yao huwa haibebi hewa ya kutosha ya oksigeni. Hali hii inaweza kuwafanya wawe wagonjwa.
Kuna kitu chekundu katika damu kinachotwaa oksigeni katika hwa na kuipeleka kila mahali mwilini. Huwa kemikali ndani ya chembechembe zilizo asili ya kila kitu chenye uhai, kisipoumbika vizuri na kikose kupita ndani ya mishipa ya damu, mishipa inaweza kuziba na kusababisha maumivu makali.
Sickle Cell ni hali inayorithiwa. Mtu huipata kutoka kwa wazazi wake. Kila mtu hupata nusu ya jeni (genes) zake kutoka kwa mzazi wa kiume nusu na kutoka kwa mzazi wa kike. Iwapo wazazi wote (baba na mama) wana jeni ya Sickle Cell, wanaweza kupata mtoto aliye na ugonjwa huu hata kama wao wenyewe hawana.
Sickle Cell hali hii hupatikana sana sana kwa watu wanaotoka sehemu za Afrika ya Kati na Magharibi.
Watu walio hatarini zaidi ya kupata ugonjwa wa Anemia ya Sickle Cell
Wengi walio na hali hii katika damu yao hutoka sehemu za Afrika ya Kati, Amerika ya Kusini na Kati, India ya Kati na nchi za Mediterania kama vile Uhispania, Uturuki, Ugiriki na Italiano.
Kutambua iwapo una ugonjwa huu
Mtu yeyote anaweza kuenda kuangaliwa na daktari kuchunguza iwapo ana ugonjwa huu. Iwapo wewe na mpenzi wako mnapanga kuoana na kuwa wazazi, ni lazima ufanyiwe uchunguzi hasa iwapo mnatoka sehemu ya Afrika ya Kati au mna wazazi wanaotoka kwenye sehemu ambako ugonjwa huu upo. Daktari wako anaweza kukufanyia uchunguzi au akutume kwa daktari mwingine aliye na ujuzi wa kukagua tabia zinazorithiwa za kifamilia.
Iwapo mna mtoto ni muhimu afanyiwe uchunguzi iwapo ana ugonjwa huu au upo ndani ya uzao wake. Ni muhimu kutambua mtoto wako anapoendelea kukua iwapo ana huu ugonjwa.
Muone daktari mara moja kama utaona dalili zifuatazo:
- Homa
- Maumivu ya kifua
- Kupumua haraka haraka
- Uchovu
- Kuvimba kwa tumbo au sehemu za chini yake
- Kupoteza nguvu mara moja na kukosa hisi
- Maumivu ambayo hayataisha hata baada ya kupewa dawa za kupunguza uchungu pale nyumbani
- Kuhisi kujamiana ambako ni kuchungu mno na hakuwachi
- Mabadiliko ya kighafla katika namna unavyoona vitu
ZAIDI:
UGONJWA wa selimundu(sikoseli) ni ugonjwa wa kurithi ambao chimbuko lake ni familia kuwa na mtu anayekuwa na ugonjwa husika.
Ugonjwa huo unaambatana na dalili nyingi zinazotokana na kuvunjika kwa seli na kukwama kwenye mishipa ya damu kutokana na umbile lake.
Mgonjwa asipopata matibabu ya haraka na uangalizi wa karibu wa wahudumu wa afya na walezi wa wagonjwa hawa dalili hizi huchangia kwa kiasi kikubwa kwa waathirika wa ugonjwa huu kulazwa hospitali mara kwa mara na vifo vya utotoni.
Athari za ugonjwa wa sikoseli
Maumivu
Chembe nyekundu za selimundu hushindwa kupitika kwa urahisi katika mishipa midogo ya damu na hivyo kukwama na kuziba mzunguko wa damu. Hali hii husababisha maumivu yenye ukali tofauti.
Maambukizi ya vimelea vya magonjwa:
Wagonjwa wa sikoseli hasa watoto hupata maambukizi ya vimelea vya magonjwa mbalimbali kama vichomi (pneumonia), homa ya uti wa mgongo na homa ya ini.
Upungufu wa damu
Kutokana na chembe nyekundu za sikoseli kuwa na muda mfupi wa kuishi hii humuweka mgonjwa wa sikoseli katika hatari ya kupata upungufu mkubwa wa damu.
Kuvimba kwa mikono na miguu:
Mara nyingi huambatana na homa hali hii husababishwa na chembe nyekundu za sikoseli kukwama na kuziba mzunguko wa damu kwenda kwenye mikono na miguu.