WanaJF,moja kati ya mambo yanayoitesa CCM leo ni dhana ya kujivua gamba.Nimeshawishika kuwasilisha topic hii baada ya kufikiri sana na nikaona mambo makubwa matatu.
MOJA-Ni namna falsafa ya kujivua gamba ilivyopokelewa ndani na nje ya CCM.Inawezekana mwenyekiti alikuwa na nia njema sana lakini mtu ni yeye na dhamira yake
MBILI-Katibu wa Itikadi na uenezi alipata hisia kwamba walengwa wa falsafa hiyo ni E.Lowasa,A.Chenge na R.Aziz ndio maana alianza kusemasema huku na kule,Hatimae Rostam kuamua kuachia ngazi.Lakini Chenge akasema hajijui kama yeye ni gamba ndani CCM.Huku Lowasa akiitisha mkutano na waandishi akasema HATOVUMILIA KUCHAFULIWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI.
TATU-CCM imekuwa rahisi kumvua gamba Rostam kwa kuwa hakuwa kwenye system ya serikali,yeye ni mfanyabiashara wa kimataifa.Lowasa-waziri mkuu mstaafu.Hivi kweli CCM wanaweza leo kumng'oa eti ni gamba? Chenge-mwanasheria mkuu wa serikali mstaafu,kweli leo ni Gamba?Sina hakika kama watawatosa,kazi kwenu tafakarini.