TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

Jaman wale mnaopenda kulewa au kuchelewa kurudi majumbani mwenu kwa sababu za starehe kama hizi muwe mnakuwa na funguo za ziada ili ukirudi unajifungulia mwenyewe kuepusha vifo visivyo vya lazima.

Inachosha sana kuamshwa na mtu aliyetoka kwenye starehe zake ukatishe usingizi wako ili umfungulie
Turudi saa ngapi maana wengine saa 3 tu sim zinaanza pigwa
 
Memba mwenzetu ametangulia mbele ya haki. Pengine nisingejisumbua kuripoti huu msiba lakini mazingira ya kifo chake ni ya kuhuzunisha na yenye mafunzo. Sijui username yake ya JF kwani tulikutana ''casually'' kwenye kilevi mwezi wa tatu mwaka huu tena siku moja tu. Katika maongezi alinijulisha kuwa yeye ni ''active member'' wa JF na anapenda sana kuchangia. Baada ya kilevi (maeneo ya Boko) tulipokuwa tunaondoka akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikaondoka kurudi kwetu Msasani ninakoishi.

Fast forward, wiki kama mbili zilizopita nilirudi tena maeneo tuliyokutana kwenye mishe zangu. Nikaona msiba kwenye boma aliloniambia ni nyumba yake. Kuulizia kulikoni nikaambiwa ni yeye, mwenye nyumba amefariki. ''Eti'' alitoka kwenye kilevi usiku, akagonga geti, mke akagoma katukatu kumfungulia. Akachukua uamuzi wa kuruka ukuta. Kwa bahati mbaya akachomwa na moja ya nondo zilizoko kwenye geti la nyumba (nadhani wengi mnafahamu nondo zinazochongwa kama mkuki na kuwekwa juu ya kuta au geti ili kuzuia vibaka). Kwa bahati mbaya akavuja damu nyingi mpaka akapoteza maisha. RIP member.
RIP Member.
Ulikuwa na mke katili.
 
Yani mm jamani Mume wangu akiwa nje siwezi kupata usingizi silalii mpk nihakikishe nimefungua mlango huwa nawaza mengi kweli. Wacha niufungue halafu ninune tuu. But kuliko kupigwa na majambazi aisee. Na kama mume sio mlevi na hajazoea kuja late siku ikiwa hivyo huwezi pata usingizi. So maybe huyo alizidi lakini huruma lazima ikuingie ukiwaza panya road na usiku una mambo mengi.
Ila hatuwezi hukumu hatujui kilichotokea
R.I.P
Watu wanasahau kuwa mume ni kama mtoto,mtoto hajawahi acha kukosea....yaan mtoto wa mwenzio unamwacha alale nje wewe unakoroma ndani? ....sawa wanawake tuna roho mbaya lakini yatusaidia nn kufanya ivo kwa mtoto wa watu ambaye bado unaendelea kuishi nae....Mi binafsi MTU nikimshindwa tabia naachana nae,eti utaachana na wangapi? Wewe utaua watoto wa watu Mara ngapi?
 
Jaman wale mnaopenda kulewa au kuchelewa kurudi majumbani mwenu kwa sababu za starehe kama hizi muwe mnakuwa na funguo za ziada ili ukirudi unajifungulia mwenyewe kuepusha vifo visivyo vya lazima.

Inachosha sana kuamshwa na mtu aliyetoka kwenye starehe zake ukatishe usingizi wako ili umfungulie
Nimechukia sana kusoma kwamba mke alikataa kumfungulia mume.Alijua mumewe anatumia kilevi.Alishindwa kumchukulia alivyo?Ona sasa!
 
Watu wanasahau kuwa mume ni kama mtoto,mtoto hajawahi acha kukosea....yaan mtoto wa mwenzio unamwacha alale nje wewe unakoroma ndani? ....sawa wanawake tuna roho mbaya lakini yatusaidia nn kufanya ivo kwa mtoto wa watu ambaye bado unaendelea kuishi nae....Mi binafsi MTU nikimshindwa tabia naachana nae,eti utaachana na wangapi? Wewe utaua watoto wa watu Mara ngapi?
Funda mama tufundikee
 
Jaman shogare kama mwanaume ni kama mtoto mbona ww ulinyoosha mikono kipenzi? Sijaongea kwa ubaya mwaya. Ukweli kuna mazingira ambayo yanapelekea mambo kama hayo. Ungemsikiliza Mrs marehem ungeelewa sana
 
Alisemaje?Ni nini kilihalalisha kutomfungulia geti/mlango mwenza wake?
 
Jaman shogare kama mwanaume ni kama mtoto mbona ww ulinyoosha mikono kipenzi? Sijaongea kwa ubaya mwaya. Ukweli kuna mazingira ambayo yanapelekea mambo kama hayo. Ungemsikiliza Mrs marehem ungeelewa sana
Soma point yangu,mume akinishinda tabia naachana nae....NAACHANA NAE....kwann ung'ang'anie mpaka uue.Umeshindwa sepa.
 
Huyu Masanja alikuwa sijui kiongozi wa michezo. Ni kisa cha zamani.
alikuwa Meneja wa uwanja wa Taifa , jamaa alikuwa mzoefu wa ,kuruka ukuta hadi akajiwekea matofali ya kupanda kabisa namkumbua sana huyu braza tulikuwa tunalewa naye sana kimara alikuwa na gari yake Cruza 11 prado short chassis

Mlinzi wa Nyumba ya jirani Emmanuel Damas, akionesha eneo ambalo Charles Masanja alianguka wakati akijaribu kuruka ukuta wa Nyumbani kwake majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo. Baada ya kuanguka, Masanja alifariki muda mfupi baadae wakati akipelekwa Hospitali.
 
alikuwa Meneja wa uwanja wa Taifa , jamaa aliuwa mzoefu wa ,kurua ukuta hadi akajiwekea matofai ya kupanda kabisa namkumbua sana huyu braza tulikuwa tunalewa naye sana kiara alikuwaa na gari yake Cruza 11 prado short chassis

Mlinzi wa Nyumba ya jirani Emmanuel Damas, akionesha eneo ambalo Charles Masanja alianguka wakati akijaribu kuruka ukuta wa Nyumbani kwake majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo. Baada ya kuanguka, Masanja alifariki muda mfupi baadae wakati akipelekwa Hospitali.
Yani nyumba yako mwenyewe ukaruke ukutaaaa?? 😃😃😃
 
Back
Top Bottom