Wana ccm wote wapenda chama wanafurahia yanayoendelea dodoma.
Sidhani kama kuna mtu ambaye mkewe au mumewe akimsaliti atafurahia usaliti wake, ni lazima atachukua hatua.
Wanaofukuzwa wote ni vibaraka wa aliyekuwa mwanachama wa ccm, mamvi, na wanaendelea kuwa waaminifu kwake. Kuendelea kuwaacha ndani ya ccm ni kukiuza chama.
Ila habari ya wanaofukuzwa sio njema kabisa kwa chadema maana sasa hawana namna ya kuendelea kupitisha mambo yao na kuharibu ccm, au kupata info za ndani, maana watu wao hawapo, na hili ni funzo, wewe kama ni mwana ccm kuwa muaminifu kwa chama, katiba inakutaka hivyo, ukiona chama hakikufai kwa kutofanya unavyoona wewe inafaa, toka nenda kwingine, usipotoka na tukikujua tutakufukuza.
(Ndio maana chadema mlimfukuza Zitto Kabwe toka chadema kwa kigezo kuwa ni 'msaliti', so usaliti ni kosa la kufukuzwa chama, period
Muda wa kuchekeana umekwisha. Hatutaki wana ccm mchana wakati usiku ni wana chadema.
Poleni chadema, mjipange. Hongera CCM kwa kukipanga chama na kutuhudumia wananchi