Hiyo biashara sista angu ameshaingia na ananishawishi kujiunga lkn mambo yangu wakati huu ni mabaya. Kifupi unahitaji capital ya kama 3m au zaidi kununua products zao zinaweza kuw saa au holiday package. Ukishanunua unakuwa member, sasa ili uweze kupata commission inakubidi na wewe ulete wenzako wawili. Sista ameniambia kuna watu wanapokea kamisheni kwa mwezi mpaka $3000 (dola elfu tatu), hata yeye amedai ameshaanza kupokea kamisheni yake. Yaani ukishajiunga, na ukafanikiwa kuinvite wenzako wawili au zaidi, kazi pekee kwako ni kuendesha semina kwa members wapya, yaani utapangiwa tarehe na venue kwa ajili ya kuwaelekeza. Ukiweza hivyo basi utajiri nje nje yaani mpunga utakuwa unaingia kila mwezi tu.
Note: Hayo niliyosema nimeelezewa na sista lkn bado sijaprove, kama kuna mtu ambaye tayari ni member aje atuthibitishie