Anayedaiwa msimamizi wa mali za mke wa Balali ashtakiwa kwa utakatishaji fedha

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
6,307
Points
2,000

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
6,307 2,000
Dar es Salaam. Elizabeth Balali (54), mfanyabiashara mkazi wa Boko Magengeni amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya kujipatia Sh25 milioni kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha.

Mshtakiwa huyo anayedaiwa kuwa msimamizi wa mali za mke wa gavana wa zamani wa Benki Kuu Tanzania (BoT), marehemu Daudi Balali, amesomewa mashtaka hayo leo Alhamisi Oktoba 10, 2019 na wakili Wankyo Simon mbele ya hakimu mfawidhi, Kelvin Mhina.

Wankyo amedai kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alijipatia Sh25 milioni kwa ulaghai kutoka kwa Dk Roderick Kisenge.

Anadaiwa kumuuzia eneo la mita 900 ambalo halijapimwa lililopo Boko Dovya wilayani Kinondoni wakati akijua si lake.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, Wankyo amedai katika kipindi hicho mshtakiwa alipokea Sh25 milioni kutoka kwa Dk Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Elizabeth hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza makosa ya uhujumu uchumi.

Hakimu Mhina katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 109/2019 alimueleza mshtakiwa huyo kuwa licha ya mahakama kutokuwa na uwezo wa kuisikiliza, pia shtaka la utakatishaji wa fedha halina dhamana.

Naye Wankyo alieleza kuwa upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo kuahirishwa hadi Oktoba 24, 2019 itakapotajwa tena, mshtakiwa kupelekwa rumande.

-Mwananchi-
 
davisoni

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2014
Messages
380
Points
500

davisoni

JF-Expert Member
Joined May 3, 2014
380 500
Utapeli ni utakatishaji wa fedha Money laundry
unapewa pesa upeleke FAT kwa ajili ya michezo unazichepusha na kuzalisha faida hapo ni UTAKATISHAJI (uhujumu)
unadai unaweza kufua umeme kwa mitambo yako kumbe unazima mingine ili wewe ulipwe zaidi kilichozidi ni kutuhujum
Nimekuelewa ,lakini swala hili la kuuza kiwanja linaletaje uhujumu uchumi?Kama ni hivyo basi mitaani wengi ni wauhjumu uchumi
 
Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2016
Messages
4,604
Points
2,000

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2016
4,604 2,000
Naomba kuelimishwa kidogooo,hivi mtu akimuuzia mwenzie kiwanja ambacho sio chake,hii inaingiaje kwenye uhujumu uchumi?hiyo di utapeli?
Wajuvi was sheria mnisaidie,Maana MTAANI haya mambo yapo Sana.
Kesi hapo ni utakatishaji pesa. Yaani fedha zipatikanazo kwa utapeli zinaitwa pesa haramu (chafu).
Kitendo cha kuzitapeli na kujimilikisha inaitwa kutakatisha.
 
Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Messages
10,328
Points
2,000

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2012
10,328 2,000
Naomba kuelimishwa kidogooo,hivi mtu akimuuzia mwenzie kiwanja ambacho sio chake,hii inaingiaje kwenye uhujumu uchumi?hiyo di utapeli?
Wajuvi was sheria mnisaidie,Maana MTAANI haya mambo yapo Sana.
Nadhani kipo cha mno zaidi ya hilo,,,
maana hapa ni utapeli wa kuuza kitu ambacho si chake atiiii...!
 
Jeff Mangi

Member
Joined
Sep 23, 2019
Messages
44
Points
125

Jeff Mangi

Member
Joined Sep 23, 2019
44 125
Hapana soma hyo sheria vzr
Kutakatisha. Kufanya kitu kuwa kisafi

Unapata fedha kwa njia isiyo halali. Wizi,utapeli,kukwepa kodi,kudhulumu,kuuza madawa ya kulevya.

Fedha uliyoipata unaenda kuitumia kununua vitu halali. Mpaka hapo unanunua Mali halali kwa kutumia fedha zisizo halali. Kwa kiingereza inaitwa money loundering. Laundry ni sehemu wanapofulia nguo
 
Ngisibara

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2009
Messages
2,600
Points
2,000

Ngisibara

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2009
2,600 2,000
Hii sheria jamani... Baada ya miaka 3-4 bwana mkubwa akimwonea huruma baada ya kukonda, atamwomba akiri kosa, kuomba msamaha na kurejesha pesa huku upelelezi ukiwa bado haujakamilika!
Hi sheria inashtaki mpaka kibaka au ni uamuzi wa wakili kuamua huyu ashtakiwe kwa kosa hili na yule aende mahakamani kwa shtaka la uhujumu uchumi kwani sasa inatuchanganya kuelewa ninini hasa maana ya "kufisadi"
 
Ntolonyonyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
2,032
Points
2,000

Ntolonyonyo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
2,032 2,000
Mh....kuna ukakasi hapa...basi kesi zote zinazohusiana na kuibiana pesa ni kutakatisha pesa na uhujumu uchumi,wezi wanaotuibia pesa mitaani ni wahujumu uchumi na utajatishaji pesa et??

Kutakatisha pesa ni kuingiza pesa haramu ambayo kiuhalisia haiwezi kuingia kwenye mzunguko na kupitia wewe inaingia....pesa chafu....mtu kauza madawa ya kulevya anaweka kwenye akaunti yako...tayari hapo pesa inaingia kwenye mzunguko...etc
Kutakatisha. Kufanya kitu kuwa kisafi

Unapata fedha kwa njia isiyo halali. Wizi,utapeli,kukwepa kodi,kudhulumu,kuuza madawa ya kulevya.

Fedha uliyoipata unaenda kuitumia kununua vitu halali. Mpaka hapo unanunua Mali halali kwa kutumia fedha zisizo halali. Kwa kiingereza inaitwa money loundering. Laundry ni sehemu wanapofulia nguo
 
kabombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Messages
21,849
Points
2,000

kabombe

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2011
21,849 2,000
Ndugu zangu hili swala la uhujumu uchumi nadhani sasa ni kwa ajili ya kukomoa watu tu basi. angalia kesi kama hii yaani mtu unakosaje dhamana wakati swala ni hilo dogo tu halafu thamani ya fedha ni 25 mn tu.
Soma vizuri,shitaka ni utakatishaji
Kupokea pesa ya zao la wizi maana yake ni utakatishaji
Huyo mama amepokea pesa huku akijua kwamba ameuza kiwanja ambacho si chake,kisha akaingiza hiyo pesa kwenye mfumo halali kama kunywea bia,kununua gari huko ni kutakatisha
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2017
Messages
1,946
Points
2,000

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2017
1,946 2,000
Inafanana na sheria za kikoloni - kuzuia watu kupata uhuru na kuwanyanyasa kisaikolojia. Yaani mtu akikukamata na gunia la korosho akasema umehujumu uchumi, unakwenda mahabusu bila dhamana na upelelezi unachukuwa miaka na miaka... bila kukamilika. Yaani ni sawa na kufungwa kabla ya hukumu. Naamini kuna siku huu msumeno utawakata walioipitisha pia. Tumekuwa wakoloni weusi.
Hi sheria inashtaki mpaka kibaka au ni uamuzi wa wakili kuamua huyu ashtakiwe kwa kosa hili na yule aende mahakamani kwa shtaka la uhujumu uchumi kwani sasa inatuchanganya kuelewa ninini hasa maana ya "kufisadi"
 
Mshumaa wa Mbao

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Messages
340
Points
250

Mshumaa wa Mbao

JF-Expert Member
Joined Aug 5, 2019
340 250
Naomba kuelimishwa kidogooo,hivi mtu akimuuzia mwenzie kiwanja ambacho sio chake,hii inaingiaje kwenye uhujumu uchumi?hiyo di utapeli?
Wajuvi was sheria mnisaidie,Maana MTAANI haya mambo yapo Sana.
hiyo fedha ya udanganyifu baada ya kuipata akiweka katika mzunguko halali wa hela ilhali kapata isivyo kihalali..hii ni sawa kwa watu wa madawa ambao hupata mifedha mingi na huzuga kwa kuchukua kiasi fulan cha hizo hela na kuanzisha shughuli fulani ya kibiashara inayoficha biashara haramu(madawa)

hiyo biashara inayoonekana ndio huifanya kana kwamba kujisafisha mbele ya macho ya watu

kuna movie fulani inaonyesha wakuda wa madawa ambao wana kiwanda cha madawa .mbele ya hicho kiwanda wamekificha na supermarket. na kwenye hiyo supermarket wana kila kitu na wanahudumia tu huku shughuli za chini ya carpet zinaendelea
 
Ngisibara

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2009
Messages
2,600
Points
2,000

Ngisibara

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2009
2,600 2,000
Inafanana na sheria za kikoloni - kuzuia watu kupata uhuru na kuwanyanyasa kisaikolojia. Yaani mtu akikukamata na gunia la korosho akasema umehujumu uchumi, unakwenda mahabusu bila dhamana na upelelezi unachukuwa miaka na miaka... bila kukamilika. Yaani ni sawa na kufungwa kabla ya hukumu. Naamini kuna siku huu msumeno utawakata walioipitisha pia. Tumekuwa wakoloni weusi.
Kwa namna nyingine tuseme ni kizuizini ya kimtindo fulani hivi?
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
17,072
Points
2,000

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
17,072 2,000
Utapeli ni utakatishaji wa fedha Money laundry
unapewa pesa upeleke FAT kwa ajili ya michezo unazichepusha na kuzalisha faida hapo ni UTAKATISHAJI (uhujumu)
unadai unaweza kufua umeme kwa mitambo yako kumbe unazima mingine ili wewe ulipwe zaidi kilichozidi ni kutuhujum
Nadhani umeshindwa kuelewa dhima ya neno kutakatisha pesa.
 
Forum statistics

Threads 1,343,413
Members 515,033
Posts 32,783,909
Top