Anayedaiwa msimamizi wa mali za mke wa Balali ashtakiwa kwa utakatishaji fedha

Kesi hapo ni utakatishaji pesa. Yaani fedha zipatikanazo kwa utapeli zinaitwa pesa haramu (chafu).
Kitendo cha kuzitapeli na kujimilikisha inaitwa kutakatisha.
Hakuna kitu kama hicho hapo kuna inshu nyingine,kuna jamaa yangu ana kesi kama hiyo mtu alimuuzia kiwanja ambacho sio chake tena kwa milioni 50!! Mbona kesi iliyofunguliwa ni kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na hadi leo ipo mahakamani, na jamaa yuko nje kwa dhamana? Na kama ingewekwa humo mbona watu wengi mtaani wangekuwa magerezani? Haya kuna jamaa alikua anawadanganya kina dada anatembea nao, alipokamatwa amepewa kesi ya uhujumu uchumi hapo vinauhusianao gani?
 
Kesi hapo ni utakatishaji pesa. Yaani fedha zipatikanazo kwa utapeli zinaitwa pesa haramu (chafu).
Kitendo cha kuzitapeli na kujimilikisha inaitwa kutakatisha.
Swali ni moja. Inawezekanaje kwa Mwananchi kumfungulia Mwananchi Mwenzake kesi Ya Uhujumu Uchumi au Utakatishaji wa Fedha.
 
Huyu wakili WANKYO SIMONI mbona kila kesi ya uhujumu yupo yeye? Au ndio masta waku'NEGOTIATE?
 
Kutakatisha. Kufanya kitu kuwa kisafi

Unapata fedha kwa njia isiyo halali. Wizi,utapeli,kukwepa kodi,kudhulumu,kuuza madawa ya kulevya.

Fedha uliyoipata unaenda kuitumia kununua vitu halali. Mpaka hapo unanunua Mali halali kwa kutumia fedha zisizo halali. Kwa kiingereza inaitwa money loundering. Laundry ni sehemu wanapofulia nguo
Anipunguzie kama 200m nimsaidie kuziosha.
 
Ndugu zangu hili swala la uhujumu uchumi nadhani sasa ni kwa ajili ya kukomoa watu tu basi. angalia kesi kama hii yaani mtu unakosaje dhamana wakati swala ni hilo dogo tu halafu thamani ya fedha ni 25 mn tu.
Unaongea ivyo kwakuwa ujatapeliwa ela zako
 
Back
Top Bottom