Anayedaiwa msimamizi wa mali za mke wa Balali ashtakiwa kwa utakatishaji fedha

hebu tupe jibu basi maana wewe unakosoa tu
Mahakama yenyewe inashindwa kuwahukumu watuhumiwa wa kesi za namna hii (utakatishaji, Uhujumu, wizi wa kitapeli)
tupe somo Mkuu
Ni hivi, lets say nimepora benki milioni 100, sasa nikitaka kuzitumia hizii lets say kununua nyumba inaweza kuja kuleta maswali kwamba hizi pesa nyingi za ghafla nimezitoa wapi? Sasa ili kuzihalalisha (kuzitakatisha) naweza nikatumia mbinu tofauti tofauti. Mfano naweza kununua shamba kubwa porini huko hata kwa milioni 2 tu, halafu baada ya mwaka naliuza kwa milioni 90 kwa mteja hewa, yaani zile pesa nilizoiba ndio zinanunua shamba langu kwa kumtumia mshirika wangu katika utakatishaji, hiyo pesa inaingizwa kwenye akaunti yangu kama pesa safi kabisa ya mauzo ya shamba langu, na hiyo pesa hata nikijengea nyumba huwezi niuliza nimetoa wapi, si nimeuza shamba langu halali? Na hapo ndio pesa inakuwa imetakatishwa. Na hakuna mwenye haki ya kuniuliza kwanini umeuza shamba bei kubwa, si langu?
 
sasa nimekuelewa
lkn 100m utakaa nazo wapi mpaka mwaka upite
kwa sasa nasikia hizi Benki kuna kitengo maalm cha kucheck hela za ghafla zinatoka wapi hasa kuanzia zaidi ya 10m umezipata wapi na vyanzo vyako ndio nikasema wakisadiki ndipo wanakata kodi yao
 
Kutakatisha. Kufanya kitu kuwa kisafi

Unapata fedha kwa njia isiyo halali. Wizi,utapeli,kukwepa kodi,kudhulumu,kuuza madawa ya kulevya.

Fedha uliyoipata unaenda kuitumia kununua vitu halali. Mpaka hapo unanunua Mali halali kwa kutumia fedha zisizo halali. Kwa kiingereza inaitwa money loundering. Laundry ni sehemu wanapofulia nguo

Mkuu unadhani basi hawa watu hawaelewi, wanaelewa sana. Tatizo wanataka kujustify theories zao kuhusu utakatishaji. Lakini tafsi rahisi ndo hiyo: kufanya fedha uliyoipata kwa njia isiyo halali kuwa halali
 
Siku hizi hilo neno linatumika vyovyote ili mradi tu mlengwa awekwe kolokoloni. Chochote utakachofanya, mwendesha mashitaka akisema ulitakatisha fedha na kuhujumu uchumi basi unawekwa chemba kwa miaka kadhaa... Mahakamani unaletwa tu kupigwa picha na waandishi wa habari huku "upelelezi" ukiendelea. Kwa hiyo ndivyo ilivyo...
Nadhani umeshindwa kuelewa dhima ya neno kutakatisha pesa.
 
Siku hizi hilo neno linatumika vyovyote ili mradi tu mlengwa awekwe kolokoloni. Chochote utakachofanya, mwendesha mashitaka akisema ulitakatisha fedha na kuhujumu uchumi basi unawekwa chemba kwa miaka kadhaa... Mahakani unaletwa tu kupigwa picha na waandishi wa habari huku "upelelezi" ukiendelea. Kwa hiyo ndivyo ilivyo...
Hii ndio Lugha PANA kwa sasa kwa Mwendesha Mashtaka, ndio maana kina Kitilya walitakatisha hela ingawa ilisharudishwa au haikutolewa kabisa
Maimu vitambulisho vya NIDA aliviwekea Insurance wakati waliomuuzia mitambo na material walishaweka katika mauzo yao kwa hiyo chha juu kikarudishwa, sasa kusudio alilolitaka ni utakatishaji
 
tapeli anataka fedha zako lakini hana mpango wa kukuua, jambazi anataka fedha zako na uhai wako ikibidi.
Miaka ya nyuma kwenye gazeti la Sunday News kulikuwa na kona ya katuni inaitwa Bogi Benda inachekesha sana. Basi siku moja jambazi akamyooshea Bogi Benda bastola na kumwamrisha ''give me your money or i will blow out your brain'' Bogi akamjibu ''Just blow out my brain, nowdays you can live without brain but not money''. Tapeli akikomba ka-akiba kako unaweza kufa kwa mengi japo hajakupiga risasi.
 
kesi za utapeli kwasasa zinaitwa 'kutakatisha fedha' na 'uhujumu uchumi', history will judge JPM harshly
Umeona kuna kosa la uhujumu uchumi hapo braza?

"Utakatishaji fedha" na "kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu" ni makosa tofauti kabisa na uhujumu uchumi.
 
Dar es Salaam. Elizabeth Balali (54), mfanyabiashara mkazi wa Boko Magengeni amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya kujipatia Sh25 milioni kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha.

Mshtakiwa huyo anayedaiwa kuwa msimamizi wa mali za mke wa gavana wa zamani wa Benki Kuu Tanzania (BoT), marehemu Daudi Balali, amesomewa mashtaka hayo leo Alhamisi Oktoba 10, 2019 na wakili Wankyo Simon mbele ya hakimu mfawidhi, Kelvin Mhina.

Wankyo amedai kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alijipatia Sh25 milioni kwa ulaghai kutoka kwa Dk Roderick Kisenge.

Anadaiwa kumuuzia eneo la mita 900 ambalo halijapimwa lililopo Boko Dovya wilayani Kinondoni wakati akijua si lake.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, Wankyo amedai katika kipindi hicho mshtakiwa alipokea Sh25 milioni kutoka kwa Dk Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Elizabeth hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza makosa ya uhujumu uchumi.

Hakimu Mhina katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 109/2019 alimueleza mshtakiwa huyo kuwa licha ya mahakama kutokuwa na uwezo wa kuisikiliza, pia shtaka la utakatishaji wa fedha halina dhamana.

Naye Wankyo alieleza kuwa upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo kuahirishwa hadi Oktoba 24, 2019 itakapotajwa tena, mshtakiwa kupelekwa rumande.

-Mwananchi-
Sheria zetu zina ukakasi.

Hapo kosa dhahiri lahuyo mama ni wizi kwa mtindo wa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.

Sasa hapo mshtakiwa kahujumu vipi uchumi?
Na katakatishaje fedha?

Utakatishaji ni pale mtu anapata kipato kisicho halali kama biashara ya madawa wa kulevya.
Anapoziingiza fedha benki anaziingiza kwenye circulation, hapo anatakatisha fedha.

Matumizi ya maneno ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha vinatumika visivyo.
 
Naomba kuelimishwa kidogooo,hivi mtu akimuuzia mwenzie kiwanja ambacho sio chake,hii inaingiaje kwenye uhujumu uchumi?hiyo di utapeli?
Wajuvi was sheria mnisaidie,Maana MTAANI haya mambo yapo Sana.
Braza hakuna kosa la uhujumu uchumi hapo. Soma tena taarifa hiyo.
 
Utapeli ni utakatishaji wa fedha Money laundry
unapewa pesa upeleke FAT kwa ajili ya michezo unazichepusha na kuzalisha faida hapo ni UTAKATISHAJI (uhujumu)
unadai unaweza kufua umeme kwa mitambo yako kumbe unazima mingine ili wewe ulipwe zaidi kilichozidi ni kutuhujum
Actually you are absolutely wrong.
 
Kutakatisha. Kufanya kitu kuwa kisafi

Unapata fedha kwa njia isiyo halali. Wizi,utapeli,kukwepa kodi,kudhulumu,kuuza madawa ya kulevya.

Fedha uliyoipata unaenda kuitumia kununua vitu halali. Mpaka hapo unanunua Mali halali kwa kutumia fedha zisizo halali. Kwa kiingereza inaitwa money loundering. Laundry ni sehemu wanapofulia nguo
Ha haaa
 
Issue Sio Jpm issue ni Hao watu Wa DPP ambao hawako smart... Kujipatia pesa kwa Njia ya udanganyifu inakuwaje ni money laundering?
Yaani kama haujui money lounderng ni kitu gani na "kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu' ni kitu gani si uulize au usome sheria zake kwanza. Tatizo wabongo wote ni wanasheria, wote ni wahandisi, wote ni madaktari etc.
 
sasa nimekuelewa
lkn 100m utakaa nazo wapi mpaka mwaka upite
kwa sasa nasikia hizi Benki kuna kitengo maalm cha kucheck hela za ghafla zinatoka wapi hasa kuanzia zaidi ya 10m umezipata wapi na vyanzo vyako ndio nikasema wakisadiki ndipo wanakata kodi yao
We jamaa jiongeze, hujawahi kusikia mtu kakamatea na bilioni 6 ziko kwenye ndoo sealed kabisa chini ya uvungu wakitanda? Hizo ni 'nguo chafu' zinasubiri kufuliwa, hazipelekwi benki hadi zifuliwe (zitakatishwe).
 
Yaani kama haujui money lounderng ni kitu gani na "kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu' ni kitu gani si uulize au usome sheria zake kwanza. Tatizo wabongo wote ni wanasheria, wote ni wahandisi, wote ni madaktari etc.
sasa mnakuja na kusahihisha wenzenu wakati majibu hamuweki
Huyo Mwanasheria Mkuu ni mara ngapi anapishana na Mawakili
Mwaga hizo sheria zako za utakatishaji na sisi tuzichambue
juzi tu kuna Wachina wamehukumiwa utakatishaji na wala sio pesa walizokamatwa nazo na tena huko zenj
It is true that in May the Ministry of Finance and Planning published the Anti-Money Laundering (Electronic Funds Transfer and Cash Transactions Reporting) Regulations, 2019 (Regulations) vide GN No 420.
The Regulations are made under section 29 of the Anti-Money Laundering Act. Under regulation 4, every electronic fund transfer must be accompanied with information required in the Second Schedule and every currency transaction shall contain information required in the First Schedule.
Hii issue ni ya pesa tu, sasa huyu Mama ni kiwanja kwa pesa na hakuziweka Bank
sheria inasemaje hapo? maana sasa mtakamata hata wenye mashamba au kuwa na wake wengi ili tu mnataka kujiMWAMBAFY

Legal Update – 30 May 2019

Anti-Money Laundering Funds Transfer Regulations Issued
  • Mandatory report formats introduced with more details of remitter and receiver of funds
  • Strict reporting guidelines for lawyers and accountants
  • Reporting Person must now report to the FIU all transactions over USD 10,000 for currency transactions and USD 1000 (for electronic transfers)
  • Gaming activity operators to report cash transactions, payments on bets
 
Hata mimi nilidhani ni kosa la utapeli,hebu tujulisheni kosa la uhujumu uchumi linawezekana pale raia anapomkosea raia mwenzie?
Naomba kuelimishwa kidogooo,hivi mtu akimuuzia mwenzie kiwanja ambacho sio chake,hii inaingiaje kwenye uhujumu uchumi?hiyo di utapeli?
Wajuvi was sheria mnisaidie,Maana MTAANI haya mambo yapo Sana.
 
Naomba kuelimishwa kidogooo,hivi mtu akimuuzia mwenzie kiwanja ambacho sio chake,hii inaingiaje kwenye uhujumu uchumi?hiyo di utapeli?
Wajuvi was sheria mnisaidie,Maana MTAANI haya mambo yapo Sana.
Sasa hizi sheria ni kukomoana!! Yaani hata kosa hilo nalo siku hizi ni uhujumu uchumi?!!! Daaaa tumekwishaaaa
 
Kutakatisha. Kufanya kitu kuwa kisafi

Unapata fedha kwa njia isiyo halali. Wizi,utapeli,kukwepa kodi,kudhulumu,kuuza madawa ya kulevya.

Fedha uliyoipata unaenda kuitumia kununua vitu halali. Mpaka hapo unanunua Mali halali kwa kutumia fedha zisizo halali. Kwa kiingereza inaitwa money loundering. Laundry ni sehemu wanapofulia nguo
Acha kupotosha watu bwana, sio kila wizi ni money laundry, dhuruma, utapeli, sema kwa sasa wanakomoa tu watu, hujasikia mmoja eti alikuwa anawadanganya wanawake na kufanya nao mapenzi naye wamempa kesi ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi? Juzi buguruni mtu amepewa kesi ya uhujumu uchumi kwa sh. 250,000
 
Back
Top Bottom