Anayechafua Serikali ya Magufuli ni nani ?

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,293
Hili suali linanijia kila wakati na kuwaza sana.

Mienendo ya viongozi wetu na mwelekeo wao huathiri mwenendo wa nchi.

Natafakari wakati ule Rais Magufuli alivyoiningia katika uongozi namna alivyowatia watu wengi tamaa na imani kuwa sasa nchi inakwenda tunakotaka. Lakini ghafla tumeshuhudia mambo ambayo si ya kawaida hapa Tanzania.Ni wazi sasa upepo umegeuka na Tanzania ina taswira mbaya hapa NDANI NA NJE.

Kwanza kuanzia pale neno uzalendo lilipotafsiriwa kuwa ni kuunga mkono kila lifanywalo na watawala hata kama wanakosea na kuwadharau na kuwashughulikia wapingaji kuwa sio wazalendo hili lilikuwa pigo la kwanza. Kuanzia hapo nchi ikawa na visasi na migawanyiko.

Walau leo nataka tumjuwe anayechafuwa serikali ya Rais Magufuli kwani tatizo ni nini ?

Je, wanaochafuwa ni wale wanaoibua hoja na wakosoaji wakubwa wa Rais Magufuli kwenye awamu hii?

Au je ni wale wasiotaka watu kuhoji na kukosoa hata pale taratibu zinapovunjwa ? au ni nani?

Nilikuwa najiuliza kwa haya mambo yaliyopelekea kutokea matatizo kwenye nchi yetu hasa kwenye maeneo haya.

(a) Kuzuiwa maandamano na haki za kidemokrasia
(b) Bunge kukosa meno ya kuisimamia serikali
(c) Utekaji na mauaji
(d) Viongozi wa upinzani kusumbuliwa bila sababu
(e) Vyombo vya habari kuminywa kufanya kazi zao
(f) Viongozi wa serikali kuingilia mambo nyaliyo nje ya uwezo wao kisheria.
(g) Lugha za utata kutoka kwa viongozi n.k

Kupitia maeneo haya na mengine, nchi yetu imejikuta ikiwa na taswira mbaya leo. Sasa nani kayaleta haya wakati hayakuwepo kwa KIASI HIKI KABLA YA UTAWALA RAIS MAGUFULI?

Natarajia majibu yenye ufafanuzi mzuri .

Kishada
 
Hii mada ni mtambuka kama yalivyo malaria. Kwa mfano JPM alizuia Maandamano na mikutano eti hataki siasa, lakini Pole Pole kutwa anapokea wapinzani na kutuhabarisha mambo ya siasa. Halafu kuna chaguzi kila siku za kujaza nafasi za wagombea walioamuwa kujitoa kwenye vyama vyao na kumuuunga mkono JPM kwa nini asitoe agizo kuwa watu wamuunge mkono huko huko na wasitoke kwenye vyama vyao ili hio siasa aliyosema haitaki isifanyike ? Tunachezeana akili.
 
Yule DAUD Albert sijui Makonda vile kosa alilolifanya kule Clouds na akaachwa na yule pacha wake kule na HAYA YA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI yanavyochafua eti atakuja mtu halafu akwambie kuna watu hatari wanatumiwa na FBI .
 
Zamani Kikwete alipokuwa Rais akikosea kuna watu walikuwa wanasema ".....Kikwete ni mzuri ila wasaidizi wake ndio wanaomwangusha........". Swali langu kwa watetezi lilikuwa, je hao wasaidizi wa JK ni nani aliyewachagua/wateua? Hawakuwa na majibu kwa swali hilo.

Leo hii Magufuli naye ni Rais, anakosea mwenyewe kwa wazi bila kificho (rejea hotuba zake na matendo yake toka awe Rais) halafu eti mtu anatafuta mwenye tatizo! Tatizo ni yeye mwenyewe, wala msitafute maana hamtapata wa kumsingizia na hapa pia.

Kila mtu abebe mzigo wake, kama ni matendo mema apewe sifa au heshima yake; lakini kama ni maovu kadhalika abebe mzigo wa lawama na uwajibikaji. PERIOD.
 
Hata yale yaliyofanywa na msajili na bwana yule dhidi ya CUF eti nayo hayaonekani. Watu wanavamia ofisi za watu na kupiga waandishi wa habari na kujeruhi, anayehoji haya kwa nini hawa hawakamatwi kama zilivyo taratibu basi unaitwa mchochezi na kugeuziwa kibao. Ni nani huyu anaiharibu nchi hii ?
 
Joni ndiye anayechafua serikali ya Magufuli
 
Rafiki na mpokea ushauri kutoka kwa Mr. Slim. a.k.a Ngongoti Kagame ndiye anayeichafua serikali.

R.I.P Binti yetu Akwilina A. B
Ndoto zako zote zimezimwa kama vile mshumaa uzimwavyo.
 
Matamko na vitendo vyake mwenyewe ndivyo vimesababisha watu tumdharau
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Hili suali linanijia kila wakati na kuwaza sana.

Mienendo ya viongozi wetu na mwelekeo wao huathiri mwenendo wa nchi.

Natafakari wakati ule Rais JPM alivyoiningia katika uongozi namna alivyowatia watu wengi tamaa na imani kuwa sasa nchi inakwenda tunakotaka. Lakini ghafla tumeshuhudia mambo ambayo si ya kawaida hapa Tanzania.

Ni wazi sasa upepo umegeuka na Tanzania ina taswira mbaya hapa NDANI NA NJE.

Kwanza kuanzia pale neno uzalendo lilipotafsiriwa kuwa ni kuunga mkono kila lifanywalo na watawala hata kama wanakosea na kuwadharau na kuwashughulikia wapingaji kuwa sio wazalendo hili lilikuwa pigo la kwanza. Kuanzia hapo nchi ikawa na visasi na migawanyiko.

Walau leo nataka tumjuwe anayechafuwa serikali ya Magufuli kwani tatizo ni nini ?

Jee wanaochafuwa ni wale wanaoibua hoja na wakosoaji wakubwa wa JPM kwenye awamu hii ?

Au je ni wale wasiotaka watu kuhoji na kukosoa hata pale taratibu zinapovunjwa ? au ni nani ?

Nilikuwa najiuliza kwa haya mambo yaliyopelekea kutokea matatizo kwenye nchi yetu hasa kwenye maeneo haya.

(a) kuzuiwa maandamano na haki za kidemokrasia
(b) Bunge kukosa meno ya kuisimamia serikali
(c) Utekaji na mauaji
(d) Viongozi wa upinzani kusumbuliwa bila sababu
(e)Vyombo vya habari kuminywa kufanya kazi zao
(f) Viongozi wa serikali kuingilia mambo nyaliyo nje ya uwezo wao kisheria.
(g) Lugha za utata kutoka kwa viongozi n.k

Kupitia maeneo haya na mengine, nchi yetu imejikuta ikiwa na taswira mbaya leo. Sasa nani kayaleta haya wakati hayakuwepo kwa KIASI HIKI KABLA YA UTAWALA JPM?

Natarajia majibu yenye ufafanuzi mzuri .

Kishada

Ni dereva wa lori. Hana uwezo kuliendesha hilo gari.
 
Mkuu umeuliza swali ambalo tayari umeshalitolea majibu, sasa sijui tukujibu nini? yaani swali umelitolea multiple choice answers kabisa mtu usihangaike kutafuta majibu ya nje ulichokiongea. But ninachoweza kusema kwa maoni yangu, Demokrasia Afrika imewahishwa sana na pengine isingekuwepo kabisa kwasababu ndiyo kitu kinachochelewasha maendeleo yetu pia. Hatuna ajenda ya kitaifa ambayo watu wetu wanaweza kuisimamia kwa pamoja. Kila mtu ana haki ya kupinga chochote kile hata kama kina manufaa kwa taifa kwa mgongo wa Demokrasia na uhuru wa mawazo.

Wenzetu ambao kwasasa wanaaply Advance Democracy wanaweza kupingana kwa mambo yote lakini huwezi kuwasikia hata siku moja wakipingana kuhusu Their National Interest. Demokrasia ililetwa na wazungu Afrika ili watu wagombane na washindwe kufocus kwenye mambo muhimu ya kuwaletea maendeleo ili wao waendelee kututawala kiuchumi na kila kitu. Demokrasia tuliyofundishwa waafrika ni kwamba kila mtu ana haki ya kutawala, So waafrika na akili zetu zilivyo kweli muda wote tunaangalia ni jinsi gani kila mtu anaweza kutawala. kwahiyo kila mtu anatumia mbinu yoyote ile itakayomwezesha kutawala.Wenzetu wanaandamana kupinga bei za sukari, huduma za kijamii n.k. Lakini sisi tunaandamana kutaka madaraka ya kisiasa (Watu wanaandamana kwasababu wameporwa haki yao ya kutawala).Matokeo yake tunajeruhiana na mpaka kupoteza roho za wasio na hatia.

Nasema Demokarasia imewahishwa Afrika au pengine isingekuepo kutokana na msingi kuwa, mfumo huu hauendani na mila, desturi na tamaduni zetu kama waafrika nikimaanisha namna tulivyokua tukijitawala na kuendesha mambo yetu kabla ya kuja kwa wazungu (wakoloni). kwasababu maamuzi ya kila kitu yalifanywa na mtu mmoja (chifu au mfalme) aliyeshauriwa na watu wachache aliyewaamini kufanya maamuzi. Mtu huyu hakua na tamaa ya rasilimali za eneo lake kusema labda atajinufaisha na yeye na familia yake, kwasababu alijua atatawala mpaka mwisho wa maisha yake na hivyo eneo alilolitawala pamoja na watu wake aliwaona ndiyo kama nyumba na familia yake. kwahiyo kila kitu kilifanywa kwa manufaa ya jamii yote na hapakua na matabaka ya waliyonacho na wasiyo nacho. Mfumo huu ungeachwa afrika ina maana sasa hivi ungekua umedevelop na umeakisi maisha tuliyonayo sasa. Kwahiyo tungekua tuna practise mfumo wa utawala ambao unaroot na mila, desturi na tamaduni zetu. Kwahivyo tusingekua na matatizo tuliyonayo sasa kwasababu ungekua umeshaji adjust kutokana na changamoto ya mazingira tuliyonayo sasa. China wameliweza hili na ndiyo maana wamepiga hatua kimaendeleo, hawana mfumo huu wa Demokrasia. Mfumo wao wa kujitawala na kujiamulia mambo yao ni wa enzi na enzi toka kwa mababu zao ambao sasa hivi tunauita Socialism.

Wenzetu waarabu waliukataa pia huu mfumo kwasababu wanajua madhara yake, ndiyo maana nchi nyingi za kiarabu zimeendelea sana japo zina rasilimali chache Mfn UAE, Qatar, Saudi Arabia n.k. Nchi zote za kiarabu ambazo wazungu walilazimisha Demokrasia hazijawahi kuwa salama mpaka sasa na mifumo yake yote ya kiuchumi imeharibika mfn. Libya, Iraq, Syria n.k muda wote watu wanapigania madaraka na sababu kubwa ni kwamba kila mtu anaona ana haki ya kutawala na kupinga chochote kupitia mgongo wa Demokrasia. TUTAFAKARI TUNAPOELEKEA NA HIKI KITU KINAITWA DEMOKRASIA.
 
1.Rais ni mwongo maana aliongea tarehe 14/10/2017 kuwa kuna Watumishi wa Umma 59,000+ watapandishwa madaraja mwezi Novemba lakini hadi sasa hajapanda hata mmoja.

2.Rais alisema baada ya uhakiki kumalizika kutakuwa na maslahi bora kwa Watumishi wa Umma lakini hadi sasa wamepewa za uso.

Waandishi wa habari hizi hazifai kupamba kwenye front page maana sijawahi kuziona.

Kutoka hifadhi ya misitu ya Madihani
Mwanachama wa CCM.
 
N
Mkuu umeuliza swali ambalo tayari umeshalitolea majibu, sasa sijui tukujibu nini? yaani swali umelitolea multiple choice answers kabisa mtu usihangaike kutafuta majibu ya nje ulichokiongea. But ninachoweza kusema kwa maoni yangu, Demokrasia Afrika imewahishwa sana na pengine isingekuwepo kabisa kwasababu ndiyo kitu kinachochelewasha maendeleo yetu pia. Hatuna ajenda ya kitaifa ambayo watu wetu wanaweza kuisimamia kwa pamoja. Kila mtu ana haki ya kupinga chochote kile hata kama kina manufaa kwa taifa kwa mgongo wa Demokrasia na uhuru wa mawazo.

Wenzetu ambao kwasasa wanaaply Advance Democracy wanaweza kupingana kwa mambo yote lakini huwezi kuwasikia hata siku moja wakipingana kuhusu Their National Interest. Demokrasia ililetwa na wazungu Afrika ili watu wagombane na washindwe kufocus kwenye mambo muhimu ya kuwaletea maendeleo ili wao waendelee kututawala kiuchumi na kila kitu. Demokrasia tuliyofundishwa waafrika ni kwamba kila mtu ana haki ya kutawala, So waafrika na akili zetu zilivyo kweli muda wote tunaangalia ni jinsi gani kila mtu anaweza kutawala. kwahiyo kila mtu anatumia mbinu yoyote ile itakayomwezesha kutawala.Wenzetu wanaandamana kupinga bei za sukari, huduma za kijamii n.k. Lakini sisi tunaandamana kutaka madaraka ya kisiasa (Watu wanaandamana kwasababu wameporwa haki yao ya kutawala).Matokeo yake tunajeruhiana na mpaka kupoteza roho za wasio na hatia.

Nasema Demokarasia imewahishwa Afrika au pengine isingekuepo kutokana na msingi kuwa, mfumo huu hauendani na mila, desturi na tamaduni zetu kama waafrika nikimaanisha namna tulivyokua tukijitawala na kuendesha mambo yetu kabla ya kuja kwa wazungu (wakoloni). kwasababu maamuzi ya kila kitu yalifanywa na mtu mmoja (chifu au mfalme) aliyeshauriwa na watu wachache aliyewaamini kufanya maamuzi. Mtu huyu hakua na tamaa ya rasilimali za eneo lake kusema labda atajinufaisha na yeye na familia yake, kwasababu alijua atatawala mpaka mwisho wa maisha yake na hivyo eneo alilolitawala pamoja na watu wake aliwaona ndiyo kama nyumba na familia yake. kwahiyo kila kitu kilifanywa kwa manufaa ya jamii yote na hapakua na matabaka ya waliyonacho na wasiyo nacho. Mfumo huu ungeachwa afrika ina maana sasa hivi ungekua umedevelop na umeakisi maisha tuliyonayo sasa. Kwahiyo tungekua tuna practise mfumo wa utawala ambao unaroot na mila, desturi na tamaduni zetu. Kwahivyo tusingekua na matatizo tuliyonayo sasa kwasababu ungekua umeshaji adjust kutokana na changamoto ya mazingira tuliyonayo sasa. China wameliweza hili na ndiyo maana wamepiga hatua kimaendeleo, hawana mfumo huu wa Demokrasia. Mfumo wao wa kujitawala na kujiamulia mambo yao ni wa enzi na enzi toka kwa mababu zao ambao sasa hivi tunauita Socialism.

Wenzetu waarabu waliukataa pia huu mfumo kwasababu wanajua madhara yake, ndiyo maana nchi nyingi za kiarabu zimeendelea sana japo zina rasilimali chache Mfn UAE, Qatar, Saudi Arabia n.k. Nchi zote za kiarabu ambazo wazungu walilazimisha Demokrasia hazijawahi kuwa salama mpaka sasa na mifumo yake yote ya kiuchumi imeharibika mfn. Libya, Iraq, Syria n.k muda wote watu wanapigania madaraka na sababu kubwa ni kwamba kila mtu anaona ana haki ya kutawala na kupinga chochote kupitia mgongo wa Demokrasia. TUTAFAKARI TUNAPOELEKEA NA HIKI KITU KINAITWA DEMOKRASIA.
Anayechafua serikali ya Magufuli ni nani ?
 
Back
Top Bottom