Mkuu umeuliza swali ambalo tayari umeshalitolea majibu, sasa sijui tukujibu nini? yaani swali umelitolea multiple choice answers kabisa mtu usihangaike kutafuta majibu ya nje ulichokiongea. But ninachoweza kusema kwa maoni yangu, Demokrasia Afrika imewahishwa sana na pengine isingekuwepo kabisa kwasababu ndiyo kitu kinachochelewasha maendeleo yetu pia. Hatuna ajenda ya kitaifa ambayo watu wetu wanaweza kuisimamia kwa pamoja. Kila mtu ana haki ya kupinga chochote kile hata kama kina manufaa kwa taifa kwa mgongo wa Demokrasia na uhuru wa mawazo.
Wenzetu ambao kwasasa wanaaply Advance Democracy wanaweza kupingana kwa mambo yote lakini huwezi kuwasikia hata siku moja wakipingana kuhusu Their National Interest. Demokrasia ililetwa na wazungu Afrika ili watu wagombane na washindwe kufocus kwenye mambo muhimu ya kuwaletea maendeleo ili wao waendelee kututawala kiuchumi na kila kitu. Demokrasia tuliyofundishwa waafrika ni kwamba kila mtu ana haki ya kutawala, So waafrika na akili zetu zilivyo kweli muda wote tunaangalia ni jinsi gani kila mtu anaweza kutawala. kwahiyo kila mtu anatumia mbinu yoyote ile itakayomwezesha kutawala.Wenzetu wanaandamana kupinga bei za sukari, huduma za kijamii n.k. Lakini sisi tunaandamana kutaka madaraka ya kisiasa (Watu wanaandamana kwasababu wameporwa haki yao ya kutawala).Matokeo yake tunajeruhiana na mpaka kupoteza roho za wasio na hatia.
Nasema Demokarasia imewahishwa Afrika au pengine isingekuepo kutokana na msingi kuwa, mfumo huu hauendani na mila, desturi na tamaduni zetu kama waafrika nikimaanisha namna tulivyokua tukijitawala na kuendesha mambo yetu kabla ya kuja kwa wazungu (wakoloni). kwasababu maamuzi ya kila kitu yalifanywa na mtu mmoja (chifu au mfalme) aliyeshauriwa na watu wachache aliyewaamini kufanya maamuzi. Mtu huyu hakua na tamaa ya rasilimali za eneo lake kusema labda atajinufaisha na yeye na familia yake, kwasababu alijua atatawala mpaka mwisho wa maisha yake na hivyo eneo alilolitawala pamoja na watu wake aliwaona ndiyo kama nyumba na familia yake. kwahiyo kila kitu kilifanywa kwa manufaa ya jamii yote na hapakua na matabaka ya waliyonacho na wasiyo nacho. Mfumo huu ungeachwa afrika ina maana sasa hivi ungekua umedevelop na umeakisi maisha tuliyonayo sasa. Kwahiyo tungekua tuna practise mfumo wa utawala ambao unaroot na mila, desturi na tamaduni zetu. Kwahivyo tusingekua na matatizo tuliyonayo sasa kwasababu ungekua umeshaji adjust kutokana na changamoto ya mazingira tuliyonayo sasa. China wameliweza hili na ndiyo maana wamepiga hatua kimaendeleo, hawana mfumo huu wa Demokrasia. Mfumo wao wa kujitawala na kujiamulia mambo yao ni wa enzi na enzi toka kwa mababu zao ambao sasa hivi tunauita Socialism.
Wenzetu waarabu waliukataa pia huu mfumo kwasababu wanajua madhara yake, ndiyo maana nchi nyingi za kiarabu zimeendelea sana japo zina rasilimali chache Mfn UAE, Qatar, Saudi Arabia n.k. Nchi zote za kiarabu ambazo wazungu walilazimisha Demokrasia hazijawahi kuwa salama mpaka sasa na mifumo yake yote ya kiuchumi imeharibika mfn. Libya, Iraq, Syria n.k muda wote watu wanapigania madaraka na sababu kubwa ni kwamba kila mtu anaona ana haki ya kutawala na kupinga chochote kupitia mgongo wa Demokrasia. TUTAFAKARI TUNAPOELEKEA NA HIKI KITU KINAITWA DEMOKRASIA.