Anayebadilisha ajira Halmashauri ni nani?

KPClassic

Senior Member
Aug 12, 2012
103
27
Jamani naomba kujua anebadilisha kazi kwa mwajiriwa wa halmashauri ni nani ?

Mfano mi nilikua mwalimu msingi, nikienda masomoni degree ya education management, nimerud but kazi ya kufundisha msingi nimechoka na sekondari sihitaji kwenda wala uratbu sitaki pia.

Nianzie wapi nataka kuwa mtumishi wa halmashauri.
 
Mkurugenzi wa halmashauri ndie bosi wa watumishi wote wa wilayani walio serikali kuu kama walimu na wengine.

Anaetakiwa kukubadilishia kazi ni mkurugenzi, andika baruaa kwenda kwa mkurugenzi ukiomba kubadilishiwa kitengo. Kama halmashauri haina urasimu na ukiritimba ni jambo la siku chache lakini navyojua halmashauri zetu inawezekana usikubaliwe au ukakubaliwa.

Jaribu mkuu.
 
Unafikri wewe tu ndo umesoma sasa kama kufundisha ulienda kusoma hiyo course ili iweje.
 
Jamani naomba kujua anebadilisha kazi kwa mwajiriwa wa halmashauri ni nani mfano mi nilikua mwalimu msingi, nikienda masomoni degree ya education management, nmerud but kaz ya kufundisha msingi nmechoka na sekondari sihitaji kwenda wala uratbu ctaki pia, nianzie wapi nataka kua mtumishi wa halmashauri.

Utasubiri sana, wako watu kibao wana Masters of Education Management and Planning lakini wanapiga chaki. Jaribu kuomba ualimu ukuu labda.
 
fuata ushauri huu wa lost id
Anaetakiwa kukubadilishia kazi ni mkurugenzi, andika barua kwenda kwa mkurugenzi ukiomba kubadilishiwa kitengo.full stop
 
Hongera sana kwa kurudi shule na kuongeza kisomo.....jaribu pia kumuona afisa utumishi wa halmashauri ulipo anaweza kukupa utaratibu wa jinsi ya kufuata....kila lakheri mkuu
 
Mkurugenzi wa halmashauri ndie bosi wa watumishi wote wa wilayani walio serikali kuu kama walimu na wengine.

Anaetakiwa kukubadilishia kazi ni lmkurugenzi, andika baruaa kwenda kwa mkurugenzi ukiomba kubadilishiwa kitengo. Kama halmashauri haina urasimu na ukiritimba ni jambo la siku chache lakini navyojua halmashauri zetu inawezekana usikubaliwe au ukakubaliwa.

Jaribu mkuu.

Shukran mkuu
 
Hongera sana kwa kurudi shule na kuongeza kisomo.....jaribu pia kumuona afisa utumishi wa halmashauri ulipo anaweza kukupa utaratibu wa jinsi ya kufuata....kila lakheri mkuu
Tenx ndugu mapovu
 
Utasubiri sana, wako watu kibao wana Masters of Education Management and Planning lakini wanapiga chaki. Jaribu kuomba ualimu ukuu labda.

Yeye anafikiri yeye tu ndo kasoma wakati kuna watu kibao wana masters wametulia wanafundisha.
 
Jamani naomba kujua anebadilisha kazi kwa mwajiriwa wa halmashauri ni nani ?

Mfano mi nilikua mwalimu msingi, nikienda masomoni degree ya education management, nimerud but kazi ya kufundisha msingi nimechoka na sekondari sihitaji kwenda wala uratbu sitaki pia.

Nianzie wapi nataka kuwa mtumishi wa halmashauri.

Fungua website ya TAMISEMI inamaelekezo yote, unaandika barua kwa katibu mkuu kupitia kwa mkurugenzi wako tamisemi ndo inakubadilisia ajira mfano toka elimu kwenda mipango,kilimo, au kada yoyote. ila kama ni kubadilisha cheo mfano mwalimu kwenda uratibu hutakiwi kuomba ila utendaji kazi wako ndo utakupandisha. lakini kwa suara lako unayo haki ya kuomba kubadilisha idara hii inaitwa kuboresha utendaji wa kazi kumbuka kama idara unayoomba imejaa mkurugenzi anaweza kataa ombi lako
 
Back
Top Bottom