Anaweza kuzaa na mwanamume mmoja tu hapa duniani!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anaweza kuzaa na mwanamume mmoja tu hapa duniani!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbunge wa CCM, Dec 13, 2009.

 1. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya wapendwa nawaletea kisa kingine.

  Kuna mwanamke mmoja mtu mzima, alinifuata nimsaidie kumshauri mpenzi wake aliyenaye angalau akubali kuzaa nae hasa baada ya kukataa kumwoa! Alisema kwa uchungu huku machozi yakimtoka.

  Katika mazungumzo yetu, ilibainika kuwa yule mwanamke anawachukia wanaume wote hapa duniani isipokuwa huyo mmoja tu! Na hadi anakutana nae huyo pekee anayempenda alikuwa alikuwa kishakaa karibu muongo mzima bila mwanume na alishaamini kuwa hatahitaji mwanaume hadi mwiso wa maisha yake.

  Kuhusu alivyotokea kupendana na huyu mwanaaume, alisema alimsikia siku moja akiongelea vizuri masuala ya malezi ya watoto, akampenda hadi leo! Hana sababu nyingine.

  Alimshauri amuoe akakataa, alimshauri wazae mtoto, akakataa. Akaona kila dalili za kurudia maisha yale ya upweke ziko wazi, akajaribu kuzizuia zisifike,

  alikuja kwangu nimsaidie, nashukuru, sasa ana ujauzito wa huyo bwana na ana furaha sana, na mpenzi wake ana furaha na amani.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kwa digestion yangu aijakaa katika mmazingira ya Kibantu/Kiafrika zaidi!

  But all in all wapo watu wenye hali za hivi..Mwanamke anakuwa mkali tuu, hataki kabisa mambo ya wanaume, sister si sister(mtawa)..ili mradi tu haeleweki!

  Sijui ni masuala ya hormones!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mapepo tu hayo.
   
 4. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2009
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  nadhani anahitaji msaada wa kiroho zaidi.
   
 5. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2009
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Anahitaji sala zaidi
   
 6. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2009
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mgombea Ubunge je huyo mwanaume ni Single?
   
 7. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndiyo. ni single,

  wamekuwa wapenzi kwa zaidi ya miaka mitano ndipo mwanume alipotaka kuangalia mambo mengine ya maisha, akiwa na maana alitaka kuanza kujiandaa kuoa. mwanume alisema kuwa hakutaka kumuoa wala kuzaa nae kwa sababu hakumwona kama wanaendana nae na maishani mwake hakuwwahi kupanga kuoa mwanamke wa aina yake.
   
 8. m

  madule Senior Member

  #8
  Dec 13, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna cha mapepo wala nini, ni kwamba mwanamke huyo ni mkweli zaidi na inaonyesha ni namna gani ana upendo wa kweli maana anayempenda ni mmoja tuu!!! na huo ndio upendo wa kweli, wanaodhani aombewe sijui kwanini wanafikiri hivo. Tatizo tuliowengi hatuna upendo wa kweli hasa TZ ndio maana unaona hata wana ndoa sio rahisi kuongozana au hata kubusiana mbele ya watu. siku ambayo wataongozana na kushikana mikono ni ile tuuu siku ya harusi yao ambapo nadhani huenda ndio wanahitimisha upendo wao na kuanza maisha mengine!!! That woman is very strong!!! other ladies in here should learn something from her. wanaotaka aombewe wafikiri kwa mara ya pili na huenda wao ndio waombewe.:D
   
 9. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nikuhakikishie mzee PJ wote ni waafrika. wanishi dar mmoja kinondoni na mwingine kijitonyama

  katika mazungumzo yetu na wote wawili niligundua mengi sana katika maisha yao wote wawili yaliyoathiri saikolojia zao. huko kuwachukia wanaume kulitokana na sababu nyingine nje ya mapepo kama walivyochangia wengine hapa jamvini. moja ya sbabu ilitokana na kuwa alianza mapenzi katika umri mdogo sana, misukosuko aliyoipata ndani na nje ya familia yake ilipelekea kuamua "kustaafu" masuala ya mapenzi alipofikisha umri wa miaka 23 tu!

  hadi anakutana na huyo mpenzi wake alikuwa na umri wa miaka 32 (mpenzi wake akiwa na miaka 33) yaani takribani miaka 9 ma maisha ya ustaafu, tena bila penseni!
   
 10. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimekupata mkuu,

  nimekubali maoni yako,

  kwa kifupi, pamoja na mambo mengine nilimshauri yule bwana asihangaike kutafuta mchumba mwingine! sikuona sababu kwa nini asimuoe. sababu alizotoa zilikuwa ndogondogo tu. hadi leo tunaendelea na ushauri nasaha na anaelekea kukubali kumuoa, naamini atakubali tu.

  kweli wengi wetu hatujajua maana ya ndoa na mahusiano. watu wengi tu hapa wanadhani huyu dada ana mapungufu, lakini naamini ni mtu muhimu sana hasa katika kipindi hiki cha hatari ya ukimwi na naamini ana uwezo mkubwa sana kuihifadhi ndoa yake kama hatimaye itafungwa
   
 11. m

  madule Senior Member

  #11
  Dec 13, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good! mweleweshe huyo jamaa yako anabahati sana amepata mke makini na asijefanya kosa kumwacha, ataruka mkojo na kukanyaga .......!
   
 12. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kwenye thread kama umeisoma vizuri, ni mama mtu mzima, ina maana age kidogo imeenda na wanawake wana limit kwa muda wa uzazi, so anaweza kufanya lolote ili apate mtoto, by the way kuna watu ambao wako hivyo, hawapendi tu kuolewa ila wanatafuta mtoto tu na wanaendelea na maisha yao kama kawaida

  wakati mgombea ubunge anamshauri alibaini kuwa keshakaa karibu muongo mmoja (10 yrs) bila kuwa na mahusiano na mwanaume. its means kabla ya huo muongo mmoja alikuwa na wanaume wengine ambao ndio chanzo cha yeye kutowapenda wanaume.

  ukiniambia hapo ni upendo wa kweli my dia, napata shida kidogo kuutafsiri huu, hivi itakuingia akilini mpenzi wako akuambie "i hate all mens/womens in the world except u!!!"
   
 13. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hebu soma mchango wangu hapa chini, nilimjibu mchangiaji mmoja jana nafikiri kuna baadhi ya majibu.

  nikuhakikishie mzee PJ wote ni waafrika. wanishi dar mmoja kinondoni na mwingine kijitonyama

  katika mazungumzo yetu na wote wawili niligundua mengi sana katika maisha yao wote wawili yaliyoathiri saikolojia zao. huko kuwachukia wanaume kulitokana na sababu nyingine nje ya mapepo kama walivyochangia wengine hapa jamvini. moja ya sbabu ilitokana na kuwa alianza mapenzi katika umri mdogo sana, misukosuko aliyoipata ndani na nje ya familia yake ilipelekea kuamua "kustaafu" masuala ya mapenzi alipofikisha umri wa miaka 23 tu!

  hadi anakutana na huyo mpenzi wake alikuwa na umri wa miaka 32 (mpenzi wake akiwa na miaka 33) yaani takribani miaka 9 ma maisha ya ustaafu, tena bila penseni
   
 14. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kwa kupenda mwenyewe au alibakwa?
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,014
  Likes Received: 23,934
  Trophy Points: 280
  Huyu bwana inabidi awe makini sana! Siku akiacha kuzungumzia masuala ya malezi ya watoto, atachukiwa kuliko wanaume wote duniani!
   
 16. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  uko sawa kabisa.
   
 17. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  duniani kuna mambo
   
 18. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  alipenda mwenyewe, shida ila wenzie walikuwa wamemzidi umri na wazoefu zaidi
   
 19. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahahahaaaaaaaa

  nimefurahi sana kwa mcango huu.

  ni moja ya kanuni muhimu sana, palilia sifa zako hadi mwisho.

  kuna watu wanabadilika mfano baada ya kuolewa au kuoa wanaonyesha tabia nyingine kwa wenzi wao na hawaonyeshi kunyenyekea tena kama mwanzo. matokeo yake ndoa zinaanza kuchacha, muhimu sana tusikunjue makucha baada ya mambo kutuendea vizuri.

  unawza kurejea kisa cha nani wa kwanza kujulishwa mtoto anapozaliwa uona mojawapo ya matokeo ya kurefusha makucha ndani ya ndoa
   
 20. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tena sana mzee, hasa ndani ya ndoa, usipime!!!!!!!!!
   
Loading...