platozoom
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 9,548
- 11,517
Ni jioni ya leo nimekaa kwenye kibaraza na Laptop yangu. Mara anatokea mtoto wa kike umri miaka kama
nane hivi mtoto wa jirani yangu, anasoma darasa la tatu.
Akaniita "Uncle plato shikamoo, naomba laptop niangalie akaunti yangu ya facebook"! Kwanza sikuwa nafahamu kama ana facebook account lakini pia Sikuwa na kazi yeyote zaidi ya kuperuzi e-mail za kale....Nikamruhusu (kwa udadisi).
Akachakua na kufungua. Halafu baada ya kitambo nikamuuliza ana marafiki wangapi, akajibu 30! Halafu akaniambia unaona hili jina (kwenye akaunti yake), ni m-boy rafiki yangu. Huwa ananisumbua na last week nimemdanganya nimesafiri na baba kwenda Nairobi but he is so sturbon!. Nikamuuliza anakusumbua kivipi? akasema "nothing than charting"!
Sasa sijui kwa sababu ya utoto akanionyesha inbox yake:
Boy: Mambo
Mtoto: Shwari
Boy: Mbona umeadimika sana
Mtoto: Am around niko na dady tunaenda Coco beach
Boy: Umerudi lini kutoka nair
Mtoto: Wikend, badae nitakutafuta tuchati..bye mwaa
Boy: Poa, keep in touch!
Mtoto hakuwahi kufika Nairobi wala muda huo anasema alikuwa home ila anamdanganya tu. Inavyoonekana jamaa ana
umri mkubwa pengine wa Sekondari na naamini hawakuwahi kuonana. Nimepigwa na butwaa sikuwa na ushauri wa haraka.
Haya wananchi kizazi cha Mummy Daddy hicho!