Anaweza kusoma Master's kwa GPA 3.1?

Akilitime

JF-Expert Member
Dec 27, 2017
581
757
Wasalaam wakuu.

Mdogo wangu ana GPA 3.1 ya chuo kikuu cha Dar es salaam.

Hivi hii G.P.A yake ndogo anaweza kupata nafasi ya kusoma Masters?

Karibu wataalamu wa masuala ya elimu.
 
Hapo Masters' anasoma bila wasiwasi mkuu, hata akitaka kuendelea hapo hapo UD. Kwa hiyo GPA hawezi tu kuja kufundisha chuo
 
Inawezekana kusoma masters ukiwa na lower second GPA bila wasiwasi, vyuo vingi tu na course nyingi tu.
 
Anasoma bila mashaka ila asiweke wazo la kuwa lecturer. GPA hiyo haitaruhusu, unless asome first degree nyingine na apate at least 3.5
 
Hapo Masters' anasoma bila wasiwasi mkuu, hata akitaka kuendelea hapo hapo UD. Kwa hiyo GPA hawezi tu kuja kufundisha chuo
Anasoma bila mashaka ila asiweke wazo la kuwa lecturer. GPA hiyo haitaruhusu, unless asome first degree nyingine na apate at least 3.5
Ohooo kwaiyo hata akipata PHD kufundisha chuo imeshampita pembeni mkuu
Kwa Tanzania ukikosa hiyo 3.5 au 3.8 kutegemea na chuo ndio basi tena hata kama utapata PhD huwi lecturer. Kule USA ukitusua ukapata PhD nzuri wewe unapita na kuwa Professor, juzi tu niliona video ya mdada wa Nigeria alipiga 2.6 lakini akapata chuo USA na sasa ni Professor kwenye chuo kikuu USA.
 
TCU Wanataka GPA ya 3.5 ila baadhi ya vyuo kupunguza ushindani wanaweka 3.8. Hao wote wa 3.8 kukiwa na uhitaji au kimaro wanachukua 3.5 bila shida. Less than 3.5 ndio shida
Uko sahihi kabisa. Ila kwa usawa huu kama mtu hana 3.8 ni bora afanye mambo mengine, ni ukweli ambao haumezeki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…