Anavyofanya huyu Mchungaji ndivyo Mwenyezi Mungu na Yesu Kristo wanavyotaka au walivyoagiza?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Ukiingia tu Kanisani Kwake utakuta kuna Viti vimeshapangwa kabisa ambapo......
  • Vya mbele kabisa hukaa VIP wa Kikristo
  • Vya katikatika kabisa hukaa wanaojitahidi kuufukuzia u VIP wa Kikristo
  • Vya nyuma kabisa hukaa sisi Mangumbaru / Masikini wa Kikristo ( tunaouota u VIP wa Kikristo )
Na hata katika utoaji wa Sadaka vile Vikapu huwa vinatiririshwa na kuserereshwa Kwanza katika viti vya mbele na vya kati na wakishajiridhisha na Kipato walichokikusudia sasa ndipo hutukumbuka akina Mangumbaru / Masikini siye huku viti vya nyuma ambao pia huwa tumebanana utafikiri Ndizi za Bukoba.

Naomba kuuliza Waumini wenzangu wa Kikristo je haya anayoyafanya huyu Mchungaji ndivyo hata maagizo ya Mwenyezi Mungu au Yesu Kristo wa Nazareth yalivyosema? Kumbe hata Mbinguni si ajabu na kwenyewe tukapangwa hivi?

Karibuni katika utiririkaji na usererekaji juu ya hili kwani binafsi nimechoka sasa na huu Ubaguzi wa wazi wazi wa Kiroho na huyu Mchungaji kama asipobadilika anaweza kunifanya ama niachane tu na Ukristo niwe Mpagani au nihamie tu kwa Ndugu zetu ambao Mwenyezi Mungu / Allah akipenda basi kati ya Ijumaa au Jumamosi ijayo wataanza kutusababisha tuwe katika likizo ndefu kidogo ya kutokwenda Guest / Lodge, kunywa Bia, Kutongoza, Kutukana na Kudanganya.

Jumapili njema.
 
mama kashakula bingo ya ubunge sasa anasubiria uwaziri huku akipiga jaramba urais 2025
 
manabiii wa uongo walishasemwa watakuja, viashiria hvyo ni moja kati ya wale manabii wa uongo.

hauwezi kuweka matabaka kanisani.
 
Duh unaroho ngumu kutengwa kote huko wewe bado unakwenda tu kwani mm naamini Yesu aliwafwata masikini
 
heri masikini wa roho (wa kikristo) maana thawabu yenu ipo mbinguni

hao VIP na SUB-VIP ni sawa na wale mafalisayo na waandishi ambao hupenda kukaa mbele ya masinagogi wakiabudu kwa kujipiga vifua na kutoa sadaka kubwa kwa sifa

kwa mujibu wa maandiko...ni vigumu kwa wao kuingia peponi kuliko ngamia kupenya tundu la sindano
 
Mathayo 25:11,"Na manabii wengi wa uongo watatokea na kudanganya wengi" . Yalishatabitiwa na Mkuu Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita.
 
ukienda kanisani nenda kamuabudu mungu wako usiende kutafta umbea na majungu kukagua watu wamevaa nn wame toa sh ngap, wamefanya nn. huu ushauri wangu tu
 
Back
Top Bottom