Anatuma watu kunichunguza kama nina mchumba

Anatuma watu kunichunguza kama nina mchumba

Punguza povu binti.
Hapa naona huu ugomvi wa familia yako unazidi kutamalaki, sababu tayari umewahisisha baba, mama, wajomba, waleta maneno, mahari, mafanikio, umasikini, chuki, visasi and ect:
Bila ubishi hata umefikia hatua ya kulileta hili hapa, maana yake limekua Kero kwako na hili jambo linakukosesha amani. Narudi kusema tafuta wasaha na ukahitimishe wewe na baba yako kwa mazungumzo, tena mkiwa wawili tu, na hapo utapata muafaka wa hili na kuamua wewe mwenyewe nini au lipi ufuate.
Baada ya hapo utaishi kwa amani, sababu hapa maandishi yako yanaonyesha rangi ya kukosa na kutoweka kwa amani moyoni mwako.
mkuu hakuna povu linalo nitoka ila kinacho niumiza ni kwann anifanyie uchunguzi kwenye jambo hili na asifanye uchunguzi kipindi nikiwa ninasoma kama nilikosa ada au la anahisi nn ???ni kwann asikae kimya akasubiri mpaka jambo hilo litokee au kupewa taarifa
 
Hivi unafikiri ni wewe mwenyewe uliyetelekezwa na baba yako?

Je waliosuswa na wazazi wote wawili lakini bado wakifanikiwa wanawafuata wazazi wao wasemeje?

Usimwite baba yako baba jina, huyo ni baba mbegu kwani mbegu yake imehusika kukutengeneza wewe.

Kwani akila hiyo mahari ndio utafilisika mazima?
hahaha! Eti Baba mbegu
 
asante mkuu yote ninayoongea yana ukweli ndani yake
Naisitoshe mkuu hilo linawezeka na wapo baadhi ya binadamu wasio na aibu wanaoweza kufanya hilo unalolizungumzia nandilo analolifanya sasa mzee huyu bila hata haya
Ni udhaifu gani huo mkuu unaona ninaweza kuwa nao?
...Ulishawahi hata kukaa naye na kuanza kumuuliza kipi kilimpelekea yeye kutokuwa sehemu ya maisha yako kwa kipindi chote hicho??..alikujibu nini?...
 
ninaapa mkuu mama hahusiki katika hili hajawahi kunieleza ubaya wowote wa huyu mzee ila nimeshuhudia mwenyewe nilikuwa nikijikomba sana kwa huyu baba bila mafanikio yoyote wala kuonyesha hali ya kutaka kunipasapoti katika malazi yangu
sahau yaliyopita upate heri, mzazi hakosei..
 
sijaambiwa mkuu wala kusikia kwa mtu hili nimeweza kuligundua mwenyewe kupitia kwa huyo mtu aliyetumwa
Kama umegundua kwa huyo alietumwa basi yeye ndio kakuambia jee ajaongeza maneno yake? Pia kwa ufahamu wangu mahari huwa ya mke mtarajiwa sasa sijui huyo alietumwa kajuaje kama baba anaitaka hio hela?

Sent from my SAMSUNG-SM-G900A using JamiiForums mobile app
 
Baba in zaidi ya kutungisha mimba. Lakini hakika baba ana baraka zake. Hebu tafakari,alimtelekeza mama yako kipindi umezaliwa ama sababu haswa ya kutojihusisha katika matunzo yako ni yepi?

Sijajua Una umri gani lakini kama upo 20+ sidhani kama kuna mantiki yoyote ya mzazi wako huyo kuwatuma watu wakuchunguze.
Mzee kashaona umri wako ni wa kuolewa, naye anataka chake!
 
Aisee ndugu yangu pole Hawa baba jina Hawa...kusamehe mtu aliekupotezea Ni hekima kutoka kwa Mungu mtu asiliongelee hivi hivi Kila mtu anajua shida aliyopitia. Muombe Mungu akujalie msamaha kama bado mtu asikulaumi kwa lolote ukifika wakati utasamehe na kuachilia. Mm muhanga wa Hilo swala and nakumbuka baba alikana mimba and wao walikuwa wanamaisha ya juu ikaonekana mama anasema ili apate urahisi wa maisha na kilichotokea akakana na mama alifariki nikiwa nazaliwa nimekua kwa shida na bibi angu eti niko chuo nashangaa nakuja kuombwa msamaha nilisema asionekane machoni pangu huyo anaejiita baba Ni baba jina. Hadi siku Mungu atanisaidia kusamehe vinginevo asithubutu ntammaliza Aisee, Hawa mababa jina wanaotafuta watoto wamekuwa wajinga sana. And alikana na anaoa hajapata mtoto tena anaona ninathaman sasa hivi asithubutu. Ka skumuona mama angu nisimuone na yeye aiseee. Sio Kila mwanaume Ni baba na Sio Kila mwanamke Ni mama. Huyu baba asiejua majukumu yake aende huyo..Aiseee ukiona hujampenda mchukie kabisaaa aende zake.. Nisimskie uwiiii
 
sahau yaliyopita upate heri, mzazi hakosei..
Ndgu Nani kasema mzazi akosei, hiyo haipo mzazi Ni binadam anakosea tena sana ndo maana Kuna wanaotupa watoto wao na wanaochinja. Baba asiejifikiria kuhusu mwanae akiwa na uhitaji wake anamtafuta mwanae wa nn. Aendeleee kuyomuhitaji. Unless huyu dada amuombe Mungu ampe rehema ya kusamehe makosa ya baba. Ila si kweli kwamba mzazi hakosei
 
tunaishi tukiquote misemo, na itabaki kuwa msemo...ila baba atabaki kuwa baba tuu.....hata umkane vipi,,,ni baba.
 
Tayari umejenga chuki kubwa kwa baba yako, na hiyo imetokana na ulio yasikia toka kwa mama yako.
Umekua na mawazo negative na baba tayari, hiyo tu inatosha kusema kwamba una chuki kuu juu yake.
Anyway......
Kwetu sisi wakristo tunasema hata kama alikutenda na hakukujali, samehe saba mara sabini, pia mpende Audi yako, alafu muheahimu baba na mama ili upate miaka mingi na heri duniani.
Ushauri.....
Jaribu kuondoa mawazo yako sasa kuhusu mabaya ya baba yako. Pia epuka kusikiliza maneno ya watu wa pembeni kwakua yawezekana wakawa kichocheo cha chuki katiyenu kwakua yawezekana wanaijua historia yenu.
Anza kuishi maisha yako kwakua tayari wewe ni mtu mzima, na usitake kujua baba na mama wana tifauti gani ambayo ilipelekea uambiwe mzee haku kuhudumia.
Jitahidi kua karibu na wazazi wote wawili na kila mmoja mpe nafasi yake na msikikize kwa wakati wake.
Kama hajaelewa Busara hii.. Ndo
Basi tena
 
Ni baba mzazi ambaye hakujihusisha kabisa na matunzo ya aina yoyote toka kukua kwangu mpaka nilipofikia sasa, hivi karibuni amekuwa akiwatuma watu wanichunguze kama nina mchumba na ukizingatia siku za nyuma amekuwa akimwaga lawama kwa mama kwamba amepokea mahari mwenyewe na amemnyima wakati ni kitu ambacho hakijawahi tokea kwakweli nashindwa kuelewa lengo hasa la huyu mzee ni nini?

Kwanini atume watu kunichunguza kama nina mchumba anataka nini?

Na ikitokea siku mahari imeletwa nyumbani asiposhirikishwa wala kupewa kutakuwa na ubaya wowote?

Hivi nikimwita baba jina nitakuwa nakosea?

Nikwanini anaanza kunifuatilia kipindi hiki ambacho tayari ninajitegemea mwenyewe huko nyuma alikuwa anafanya nini?

Wandugu naombeni mawazo yenu maana simwelewi huyu mzee
Pole mrembo,ila sisemi kama rahisi au niseme kila mja na moyo wake na maamuzi yake,kumbuka Baba daima atababikia kua Baba,awe amekimbia majukumu yake awe ameyakubali,ukiwa kama mtoto wacha aseme anavyojisikia ukweli unaujua wewe ndani ya nafsi yako na Mwenyezi mungu,mpe heshima yake kama Baba mueleze linalo mukhusu kuelezwa kama Baba
mengine muachie Mungu,timiza majukumu yako kama mtoto huenda huo ndio mtihani wako kwa mwenyezi mungu,
jaribu sana kumsamehe mapungufu yake na mwenyezi mungu ataku daraja kubwa na maisha mazuri..
 
Ni baba mzazi ambaye hakujihusisha kabisa na matunzo ya aina yoyote toka kukua kwangu mpaka nilipofikia sasa, hivi karibuni amekuwa akiwatuma watu wanichunguze kama nina mchumba na ukizingatia siku za nyuma amekuwa akimwaga lawama kwa mama kwamba amepokea mahari mwenyewe na amemnyima wakati ni kitu ambacho hakijawahi tokea kwakweli nashindwa kuelewa lengo hasa la huyu mzee ni nini?

Kwanini atume watu kunichunguza kama nina mchumba anataka nini?

Na ikitokea siku mahari imeletwa nyumbani asiposhirikishwa wala kupewa kutakuwa na ubaya wowote?

Hivi nikimwita baba jina nitakuwa nakosea?

Nikwanini anaanza kunifuatilia kipindi hiki ambacho tayari ninajitegemea mwenyewe huko nyuma alikuwa anafanya nini?

Wandugu naombeni mawazo yenu maana simwelewi huyu mzee
Hunkuelewi kivipi?huyo ni baba yako na wewe ni mtoto wake,usijidanganye eti sasa unajitegemea sijui kujitekenya au kutekenywa,yeye ndio alikukojoa wewe na wewe hata ufanye nini huna jeuri juu ya baba yako,zaidi ukileta ujuaji na kumtukana ujue laana itakutafuna tu,sasa hivi umeshajua mambo ya mautamu na kujiona umekuwa hiyo iatkutafuna tu,muheshimu baba yako.
 
sijaambiwa mkuu wala kusikia kwa mtu hili nimeweza kuligundua mwenyewe kupitia kwa huyo mtu aliyetumwa
Wewe acha ushamba,muheshimu baba yako,eti ooooh najitegemea,una kitu gani cha kujiona eti wewe unajitegemea?
 
Wengi naona kama wanaotetea tabia za wa baba wa hivi ni wale hata wasiojali watoto wao au hawajawahi kuonja maumivu ya maisha ya kukimbiwa na baba na kujali wengine.

Tumuombee Mungu amuongoze katika maamuzi yoyote atakayofanya.

Hata biblia inasema mengi kwa mfano haya:-

1 Timothy 5:8

But if anyone does not provide for his relatives, and especially for members of his household, he has denied the faith and is worse than an unbeliever.

Ephesians 6:4

Fathers, do not provoke your children to anger, but bring them up in the discipline and instruction of the Lord.

Luke 17:3

"Be on your guard! If your brother sins, rebuke him; and if he repents, forgive him.

Deuteronomy 6:6-9

"These words, which I am commanding you today, shall be on your heart. "You shall teach them diligently to your sons and shall talk of them when you sit in your house and when you walk by the way and when you lie down and when you rise up. "You shall bind them as a sign on your hand and they shall be as frontals on your forehead.
"You shall write them on the doorposts of your house and on your gates.

Colossians 3:21

Fathers, do not exasperate your children, so that they will not lose heart.

Ezekiel 20:18

"I said to their children in the wilderness, 'Do not walk in the statutes of your fathers or keep their ordinances or defile yourselves with their idols.

Matthew 18:6

but whoever causes one of these little ones who believe in Me to stumble, it would be better for him to have a heavy millstone hung around his neck, and to be drowned in the depth of the sea.

Proverbs 11:21

Assuredly, the evil man will not go unpunished, But the descendants of the righteous will be delivered.

Ezekiel 18:20

The soul who sins shall die. The son shall not suffer for the iniquity of the father, nor the father suffer for the iniquity of the son. The righteousness of the righteous shall be upon himself, and the wickedness of the wicked shall be upon himself.
 
Hivi unafikiri ni wewe mwenyewe uliyetelekezwa na baba yako?

Je waliosuswa na wazazi wote wawili lakini bado wakifanikiwa wanawafuata wazazi wao wasemeje?

Usimwite baba yako baba jina, huyo ni baba mbegu kwani mbegu yake imehusika kukutengeneza wewe.

Kwani akila hiyo mahari ndio utafilisika mazima?
Mhh hapana,kama ungekuwa unajua ugumu wa kutelekezwa na mzazi wala usingejibu kirahisi hivi,nina mfano hai kidogo,nina mdogo wangu mtoto wa mama mdogo baba yake alimteleza tangu day one alivyopewa taarifa za kuzaliwa mtoto hakuwa kutoa hata sent tano kuhusu dogo,dogo kalelewa na uncle kuanzia hiyo day one mpa dogo anapata degree ya kwanza, na pia akaleta na kashfa juu,sasa dogo ni boss kampuni flani baba yake mzazi anamtaka na kujitamba kabisa yule ni mtoto wangu yule,mkosi ulivyo sasa hao wa kwake wa ndoa ni akuna hata mmoja mwenye mbele wala nyuma,je baba huyu naye aitweje???
 
Wa
Ni baba mzazi ambaye hakujihusisha kabisa na matunzo ya aina yoyote toka kukua kwangu mpaka nilipofikia sasa, hivi karibuni amekuwa akiwatuma watu wanichunguze kama nina mchumba na ukizingatia siku za nyuma amekuwa akimwaga lawama kwa mama kwamba amepokea mahari mwenyewe na amemnyima wakati ni kitu ambacho hakijawahi tokea kwakweli nashindwa kuelewa lengo hasa la huyu mzee ni nini?

Kwanini atume watu kunichunguza kama nina mchumba anataka nini?

Na ikitokea siku mahari imeletwa nyumbani asiposhirikishwa wala kupewa kutakuwa na ubaya wowote?

Hivi nikimwita baba jina nitakuwa nakosea?

Nikwanini anaanza kunifuatilia kipindi hiki ambacho tayari ninajitegemea mwenyewe huko nyuma alikuwa anafanya nini?

Wandugu naombeni mawazo yenu maana simwelewi huyu mzee

Wakiristu waliachiwa falsafa ya kumpenda adui.Ni vizuri ukaanza kuishi falsafa hiyo.Ninachokiona wewe umejazwa maneno na mama yako kwamba baba hakuwa na msaada wowote ule.Wewe ulikuwa mdogo je ulijuaje kama hakuwa akitimiza wajibu wake kwako?Je yeye mama aliweza kutoa kila ulichohitaji na kwa wakati?

Wewe uko katika wakati wa kuanza familia jifunze mambo mazuri ya kurithisha watoto wako.Hata wewe sio mwema.Je,Mungu ameacha kukutendea mema licha ya kwamba kuna wakati unamkosea?Tenda wema hukumu ni kazi ya Mungu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom