Punguza povu binti.
Hapa naona huu ugomvi wa familia yako unazidi kutamalaki, sababu tayari umewahisisha baba, mama, wajomba, waleta maneno, mahari, mafanikio, umasikini, chuki, visasi and ect:
Bila ubishi hata umefikia hatua ya kulileta hili hapa, maana yake limekua Kero kwako na hili jambo linakukosesha amani. Narudi kusema tafuta wasaha na ukahitimishe wewe na baba yako kwa mazungumzo, tena mkiwa wawili tu, na hapo utapata muafaka wa hili na kuamua wewe mwenyewe nini au lipi ufuate.
Baada ya hapo utaishi kwa amani, sababu hapa maandishi yako yanaonyesha rangi ya kukosa na kutoweka kwa amani moyoni mwako.