Anatuma watu kunichunguza kama nina mchumba

La gioconda

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2015
Posts
679
Reaction score
1,286
Ni baba mzazi ambaye hakujihusisha kabisa na matunzo ya aina yoyote toka kukua kwangu mpaka nilipofikia sasa, hivi karibuni amekuwa akiwatuma watu wanichunguze kama nina mchumba na ukizingatia siku za nyuma amekuwa akimwaga lawama kwa mama kwamba amepokea mahari mwenyewe na amemnyima wakati ni kitu ambacho hakijawahi tokea kwakweli nashindwa kuelewa lengo hasa la huyu mzee ni nini?

Kwanini atume watu kunichunguza kama nina mchumba anataka nini?

Na ikitokea siku mahari imeletwa nyumbani asiposhirikishwa wala kupewa kutakuwa na ubaya wowote?

Hivi nikimwita baba jina nitakuwa nakosea?

Nikwanini anaanza kunifuatilia kipindi hiki ambacho tayari ninajitegemea mwenyewe huko nyuma alikuwa anafanya nini?

Wandugu naombeni mawazo yenu maana simwelewi huyu mzee
 
Baba in zaidi ya kutungisha mimba. Lakini hakika baba ana baraka zake. Hebu tafakari,alimtelekeza mama yako kipindi umezaliwa ama sababu haswa ya kutojihusisha katika matunzo yako ni yepi?

Sijajua Una umri gani lakini kama upo 20+ sidhani kama kuna mantiki yoyote ya mzazi wako huyo kuwatuma watu wakuchunguze.
 
Hivi unafikiri ni wewe mwenyewe uliyetelekezwa na baba yako?

Je waliosuswa na wazazi wote wawili lakini bado wakifanikiwa wanawafuata wazazi wao wasemeje?

Usimwite baba yako baba jina, huyo ni baba mbegu kwani mbegu yake imehusika kukutengeneza wewe.

Kwani akila hiyo mahari ndio utafilisika mazima?
 
Tayari umejenga chuki kubwa kwa baba yako, na hiyo imetokana na ulio yasikia toka kwa mama yako.
Umekua na mawazo negative na baba tayari, hiyo tu inatosha kusema kwamba una chuki kuu juu yake.
Anyway......
Kwetu sisi wakristo tunasema hata kama alikutenda na hakukujali, samehe saba mara sabini, pia mpende Audi yako, alafu muheahimu baba na mama ili upate miaka mingi na heri duniani.
Ushauri.....
Jaribu kuondoa mawazo yako sasa kuhusu mabaya ya baba yako. Pia epuka kusikiliza maneno ya watu wa pembeni kwakua yawezekana wakawa kichocheo cha chuki katiyenu kwakua yawezekana wanaijua historia yenu.
Anza kuishi maisha yako kwakua tayari wewe ni mtu mzima, na usitake kujua baba na mama wana tifauti gani ambayo ilipelekea uambiwe mzee haku kuhudumia.
Jitahidi kua karibu na wazazi wote wawili na kila mmoja mpe nafasi yake na msikikize kwa wakati wake.
 
La gioconda
Hayo maneno umesikia akisema baba yako kuwa uchunguzwe kuwa una mchumba au kuna mtu ndio kakuambia? Manake kuna watu wanapenda kuwalisha watu maneno (wanafik) kwenye dunia hii nimesoma baba na mama ndio marafiki wa kweli waliobakia tunajuana tu. Usimsuse baba kwa unayoyasikia kaa nae akupe story ya upande wake ukajua kwanini alikuwa hayupo kwenye maisha yako.
 
Huyo hastahili kuitwa baba bali ni sperm donor. Hakuwepo kwenye shida na raha zako wakati unakuwa sasa kama una mchumba au la inamhusu nini!? Kwa maoni hastahili kupata hata senti moja ya mahari, lakini hayo ni maamuzi yako kama apate au la.

Hao ndiyo wale hukimbia majukumu yao kama wazazi Baba/Mama kisha hutaka kunufaika pale wanaposikia mtoto waliyemtelekeza anafanya vizuri kimaisha, mfano halisi ni Baba Diamond ambaye aliingia mitini kwa miaka mingi huku hajui wala hajali wanae wamelala wapi wamekula nini, lakini sasa anataka kunufaika na kwenda hata kwenye vyombo vya habari ili kumshinikiza DP amsaidie.

Ni baba mzazi ambaye hakuji husisha kabisa na matunzo ya aina yoyote toka kukua kwangu mpaka nilipofikia sasa
Hivi karibuni amekuwa akiwatuma watu wanichunguze kama nina mchumba na ukizingatia siku za nyuma amekuwa akimwaga lawama kwa mamy kwamba amepokea mahari mwenyewe na amemnyima wakati nikitu ambacho hakijawahi tokea kwakweli nashindwa kuelewa lengo hasa la huyu mzee ni nn???

kwanin atume watu kunichunguza kama nina mchumba anataka nn???

Na ikitokea siku mahar imeletwa home asiposhirikishwa wala kupewa kutakuwa na ubaya wowote???

Hivi nikimwita baba jina nitakuwa nakosea???

Nikwann anaanza kunifuatilia kipindi hiki ambacho tayari ninajitegemea mwenyewe huko nyuma alikuwa anafanya nin???
wandugu naombeni mawazo yenu maana simwelewi huyu mzee
 
Mchumba mie nimeshapatikana. Lete no ya Mpesa/Tigopesa ya mama yako nidumbukize humo mahari kimya kimya bila ya baba jina kujua.
 
Huyo hastahili kuitwa baba bali ni sperm donor. Hakuwepo kwenye shida na raha zako wakati unakuwa sasa kama una mchumba au la inamhusu nini!? Kwa maoni hastahili kupata hata senti moja ya mahari, lakini hayo ni maamuzi yako kama apate au la.

Hao ndiyo wale hukimbia majukumu yao kama wazazi Baba/Mama kisha hutaka kunufaika pale wanaposikia mtoto waliyemtelekeza anafanya vizuri kimaisha, mfano halisi ni Baba Diamond ambaye aliingia mitini kwa miaka mingi huku hajui wala hajali wanae wamelala wapi wamekula nini, lakini sasa anataka kunufaika na kwenda hata kwenye vyombo vya habari ili kumshinikiza DP amsaidie.
Halafu bila haya anatuma watu?
Kudhihiridha jinsi gani ni mchumia tumbo.... na ukosefu wa nidhamu....
Angetaka kujua kwa nia njema si angeuliza straight kistaarabu tu? Hata kama alitelekeza angepewa tu heshima yake na kujibiwa

Nikirudi kwa Binti; uliyeokota nae kuni ndie wa kuota nae moto....kula tu na mama yako mahari
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi unafikiri ni wewe mwenyewe uliyetelekezwa na baba yako?

Je waliosuswa na wazazi wote wawili lakini bado wakifanikiwa wanawafuata wazazi wao wasemeje?

Usimwite baba yako baba jina, huyo ni baba mbegu kwani mbegu yake imehusika kukutengeneza wewe.

Kwani akila hiyo mahari ndio utafilisika mazima?
sawa mkuu ale mahari kwa jasho lipi alilolitoa kwa ajili yangu??? kwa malez na malaz gan aliyonipa ?????
 
Baba in zaidi ya kutungisha mimba. Lakini hakika baba ana baraka zake. Hebu tafakari,alimtelekeza mama yako kipindi umezaliwa ama sababu haswa ya kutojihusisha katika matunzo yako ni yepi?

Sijajua Una umri gani lakini kama upo 20+ sidhani kama kuna mantiki yoyote ya mzazi wako huyo kuwatuma watu wakuchunguze.
alimtelekeza kipindi nimezaliwa na sababu hasa hakuna pesa ndizo zilizomchanganya na kwenda kutanua na wanawake wengine huku akimuacha mamy akihangaika nami leo pesa zimeisha na ameona tayari nina mafanikio yangu ndio anaanza kuleta pua yake na kuanza kuwatuma watu wanichunguze kama ninachumba kuhusu miaka nina 24
 
Ni baba mzazi ambaye hakuji husisha kabisa na matunzo ya aina yoyote toka kukua kwangu mpaka nilipofikia sasa
Hivi karibuni amekuwa akiwatuma watu wanichunguze kama nina mchumba na ukizingatia siku za nyuma amekuwa akimwaga lawama kwa mamy kwamba amepokea mahari mwenyewe na amemnyima wakati nikitu ambacho hakijawahi tokea kwakweli nashindwa kuelewa lengo hasa la huyu mzee ni nn???

kwanin atume watu kunichunguza kama nina mchumba anataka nn???

Na ikitokea siku mahar imeletwa home asiposhirikishwa wala kupewa kutakuwa na ubaya wowote???

Hivi nikimwita baba jina nitakuwa nakosea???

Nikwann anaanza kunifuatilia kipindi hiki ambacho tayari ninajitegemea mwenyewe huko nyuma alikuwa anafanya nin???
wandugu naombeni mawazo yenu maana simwelewi huyu mzee

Baba ni baba tu, hata kama anavuta shisha, kama alilala na Mama yako ukapatikana jua kwamba Mama yako alirizia na alimkubali, usithubutu kujiingiza kwenye ugomvi wao ukakosa baraka ya ndoa yako! Mama yako asikuingize kwenye chuki ambayo haitakusaidia. Mshirikishe Baba yako kwenye kila Kitu akubariki.
 
Huyo hastahili kuitwa baba bali ni sperm donor. Hakuwepo kwenye shida na raha zako wakati unakuwa sasa kama una mchumba au la inamhusu nini!? Kwa maoni hastahili kupata hata senti moja ya mahari, lakini hayo ni maamuzi yako kama apate au la.

Hao ndiyo wale hukimbia majukumu yao kama wazazi Baba/Mama kisha hutaka kunufaika pale wanaposikia mtoto waliyemtelekeza anafanya vizuri kimaisha, mfano halisi ni Baba Diamond ambaye aliingia mitini kwa miaka mingi huku hajui wala hajali wanae wamelala wapi wamekula nini, lakini sasa anataka kunufaika na kwenda hata kwenye vyombo vya habari ili kumshinikiza DP amsaidie.
Ckuwai kufikiri kama ww unaweza ongea kitu kama hiki kumbe kuna baadhi ya nyanja we ni kilaza
 
La gioconda
Hayo maneno umesikia akisema baba yako kuwa uchunguzwe kuwa una mchumba au kuna mtu ndio kakuambia? Manake kuna watu wanapenda kuwalisha watu maneno (wanafik) kwenye dunia hii nimesoma baba na mama ndio marafiki wa kweli waliobakia tunajuana tu. Usimsuse baba kwa unayoyasikia kaa nae akupe story ya upande wake ukajua kwanini alikuwa hayupo kwenye maisha yako.
sijaambiwa mkuu wala kusikia kwa mtu hili nimeweza kuligundua mwenyewe kupitia kwa huyo mtu aliyetumwa
 
sawa mkuu ale mahari kwa jasho lipi alilolitoa kwa ajili yangu??? kwa malez na malaz gan aliyonipa ?????
Hiyo mahari atakula kwa miaka mingapi?

Na je niwewe ndiye utakayegharamia mahari?

Vitu vidogo sana hivyo.
 
Hivi wewe umemtenda Mungu mangapi amekusamehe sembuse wewe ushindwe kumsameha binadam mwenzako tena babayako wenzako wanatafuta hata baba wa kambo wanakosa wewe huyo wa kukuzaa unamkataa.Kwan nnani alikuambia katuma watu wakuchungeze, shida yenu wanawake mnapenda kuishi maisha ya tamthilia
 
Angalia moyo wako kama unaonaje! waache kusema mama amekudanganya kwani huyo baba alijishughulisha na wewe lakini bado mama hakuwa na shukrani? maana nashangaaga watu kusema ooohhh mama kakujaza maneno! kakujaza ama kakueleza ukweli! angejiahughulisha ungemuona tu! hiyo sio chuki ulojenga naturally mtu ambaye hajakulea huwezi kuwa na upendo naye from no where.

Ubaba wake unakuja tu kisa mahari kwa hiyo ukiolewa bure ama kwa mkopo ubaba nawewe hana? inshort ni mchunaji huyo
 
Ni baba mzazi ambaye hakuji husisha kabisa na matunzo ya aina yoyote toka kukua kwangu mpaka nilipofikia sasa
Hivi karibuni amekuwa akiwatuma watu wanichunguze kama nina mchumba na ukizingatia siku za nyuma amekuwa akimwaga lawama kwa mamy kwamba amepokea mahari mwenyewe na amemnyima wakati nikitu ambacho hakijawahi tokea kwakweli nashindwa kuelewa lengo hasa la huyu mzee ni nn???

kwanin atume watu kunichunguza kama nina mchumba anataka nn???

Na ikitokea siku mahar imeletwa home asiposhirikishwa wala kupewa kutakuwa na ubaya wowote???

Hivi nikimwita baba jina nitakuwa nakosea???

Nikwann anaanza kunifuatilia kipindi hiki ambacho tayari ninajitegemea mwenyewe huko nyuma alikuwa anafanya nin???
wandugu naombeni mawazo yenu maana simwelewi huyu mzee

MPIGIE SIMU MSHUA WAKO KISHA MUAMBIE UMEGUNDUA ANAKU-FBI ILA KWA KILE ANACHOTAKA KUJUA NI KUWA "WEWE NI MSAGAJI NA MUDA SI MREFU UNATAKA KUOA KWA HIYO AJIANDAE KUKULETEA MAHARI YA KWENDA KULIPA HUKO UKWENI UNAKOENDA KUOA"

HAPO LAZIMA AOMBE POOH NA ATULIE TULI KAMA MAJI MTUNGINI.....KILA LA HERI KATI YAKO NA MSHUA WAKO.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom