Hivi ungeandika kwa kiswahili rahisi cha kawaida, ungepungukiwa na nini? Siingilii uhuru wako wa kuchagua lugha ya kujieleza ila kama nia yako ilikuwa kupata msaada, ungeongea kawaida. Hata hivyo wengine tumekuelewa na nitakujibu kama ifuatavyo.
Kwa kutumia aina ya lugha yako ni kwamba, unatakiwa kuacha undezi/ undorobo aka ubwege.
Huyo ni mtu kamili, mwenye hisia zake na akili timamu, aliposema kuwa hamuendani, hakusema kwa bahati mbaya kwani amefanya hivyo baada ya kukuchambua na kuona kuwa hukidhi viwango anavyovitaka yeye, huwezi kubadili hilo na pia halikufanyi wewe kuwa mjusi au nzi kwani unabaki kuwa mtu tu.
Hizo kelele za kuwa unampenda bado, ni sahihi kwa sababu ulimpenda sana na ulijipa confidence kuwa yeye ndio kila kitu kwako ila tatizo linakuja pale unapong'ang'ania kuwa unamhitaji bado wakati mpaka picha umetumiwa na si kwa kuwa alikosea, huko ni kuwa -----.
Yeye si Pumzi ya uhai kwamba utakufa ukimkosa, au kwamba ulimzaa wewe kuwa huwezi kutenganishwa nae.
Endelea na maisha yako/kazi/masomo ukiwa na mtazamo wa kuyaboresha maisha yako. Futa namba yake na acha kumsumbua kabisa. Tafuta mtu atakaekuthamini na kukupenda kwa jinsi ulivyo na ufurahie maisha yako badala ya kukaa unaota kupendwa na mtu asiekuhitaji.
Wanawake wanapenda attention na kuliliwa ila ikizidi wanatafsiri kuwa ni udhaifu wa aina fulani hata kama wanaliliwa na mtu wanaempenda sana na wanakuwa bored. Kwa hiyo usitegemee kilio chako kitamfanya akuone wa maana au kukurudia kwa sababu tayari amesema hamuendani na amekwishakuonyesha anaempenda.
So please, kick rocks and take a walk! I mean very far away! From her!