Anataka nimuoe na mtoto wake

Anataka nimuoe na mtoto wake

Let me give time think on yr advice...! You the only bad thing is that after all that kindhearted to her mom what if she doesn't care all goods i have done to her! Wanawake nyie always ni opportunists possible badae asione wema wangu nadhani nitaumia sana....! Sasa hivi anashida analia na kujigalagaza chini but kusahau ni siku chache zijazo.

I agree with you .because we are humans and humans have nature inside.. hii si kwa wanawake tuu hata kwa wanaume pia. Kuna watu nawafahamu wamesomesha wapenzi wao , Lea watoto si wao kwa nia njema tuu na kuwapa vibali vya kuishi nnchi za nnje but still pamoja na kufanyiwa yote waliwaacha na kuwa na vimada wengine .. or kuwa na wanaume wengine. ..( hii imewakuta wadada wengi kuliko wakaka) . Hivi tukifikiria mangapi mazuri tuliyowatendea watu wengine halafu ni mangapi mazuri waliyoturudishia? Hatutaweza Kuwahudumia wengine ....So try to do things from your heart in Godly way without expect something back ..but to Hope for the reward from God.. Thanks..
 
Jamani naomba ushauri wa kujenga tu!

STORI NI NDEFU KIDOGO TAFADHALI SOMA UPATE KUNISHAURI;
Kuna mdada mmoja alitokea kunipenda mpaka akanitamkia na kwa vile mimi sikuwa ktk mahusiano wakati huo nilimkubalia ila baada ya muda akaniambia kuwa ana mtoto wa kike ambaye alimzaa baada ya jamaa mmoja kumpa mimba kisha akaitaa nilimhoji sana mazingira ya mimba kukataliwa akasisitiza kuwa aliyempa mimba alimkataa yeye na mimba yake akasema nilikuwa muungwana sikuta kutoa mimba nikaamua kuzaa na kulea mtoto.

Sasa muda ulivyozidi kwenda huku mahaba yakikokelea kama treni la makaa ya mawe tulijikuta kwenye mahaba mazito sana. Ila mimi sikutaka kuwa mvivu wa kufikiri nikazidi fuatilia juu ya mtu aliyezaa naye baada ya muda nikaja kujua kuwa yule mzazi mwenzake alikuwa mchumba wake ambaye alifikia hatua ya kutoa mahari na kabla ya ndoa ndipo akawa amezaa naye mtoto huyo.

Safari ya mahaba haikusimama kwangu njiani humo humo nikaambiwa aliwahi kuishi na huyo jamaa na baada ya muda jamaa alibadirisha mwelekeo akaamua kuoa mtu mwingine. Nili hoji kama hadi ulilipiwa mahari wewe si mke wa mtu akakataa katakata kuwa yeye walikubaliana kuachana yule bwana akaja nyumbani kwao akutaka urudishiwe mahari yake alimua kusamehe akaandika barua kuvunja uchumba.

Kesi ya mtoto, jamaa anaonekana akumkataa mtoto ila walishindwa kuelewana jinsi ya kumtunza mtoto baba mtu anataka mtoto amchukue na mama mtu kakataa kwa madai mwanae atateswa kwa madai yule mke aliyeolewa alisha sema hamtaki huyo mtoto pale. Baba mtu akasema hatatoa ata senti kumtunza mtoto akiwa na mama yake alitia madai kuwa sasa hivi mtoto ana miaka mi 4 akasome boarding awe analipa huko mama hataki.

Sasa picha yangu na huyu mdada ikaanza hivi nikamwambia mbona uko kinyume na maelezo yako ya mwanzo kumbe mtoto baba yake anamtaka wewe tu ndiyo hutaki! Akaanza kulia na kunimbia kuwa yeye ni yatima hana baba wala mama amekuzwa na mjomba wake baada ya wazazi wake wote wawili kufariki.

Anadai eti yeye amekuwa kwa shida sana na hivyo akimwachia mtoto wake atateseka tena kama yeye. Anachodai kwenye mahusiano yetu nimuoe yeye na mtoto wake yaani hataki mtoto wake aende kwa baba yake nikimuuliza vipi mtoto atahudumiwa maana baba yake kagoma hawezi kumhudumia anasema huyu naye tutamhudumia kama wanetu wengine tutakaojaliwa na mola.

Mimi nikiangalia kuhudumia mtoto ambaye ana baba yake tena anakazi nzuri kiukweli napata ukakasi mara ya mwisho wamepelekana Ustawi wa jamii jamaa kakomalia msimo wake.

Naombeni ushauri wenu, stori ni ndefu, ila mwenzenu ndiyo tayari niko kwenye mahaba mazito sijielewi tena.

MAHABA NISHIKE NIFINYANGE NIPIGE GWALA NINYONGE MPAKA NIKUFE KABISA...!

Neva sii b4 mwanaume wa sample yako! Nikueleze kitu kiukweli hujampenda huyo dada ungempenda mtoto wala si tatizo! Au utakua una wivu una akili ile mtalaka hatongozwi.
Lakini ujue katika hii dunia hakuna mwanamke anayeweza kutunza mtoto wa mwenzake acha mwenzio alee mtoto wake.
Mwisho ukipenda jipu upende na usaha wake. ........... Wewe vipi bwana, kulea mtoto mmoja tu una mawazo ukiwa na wako 4?
 
Mkuu nimekosea nini kuhoji uhalali wa kulea mtoto mwenye baba yake?
 
Ninachokushauri ndg yangu,husipende kuingilia na kufuatilia sana,mambo ya mwanamke wako na mzazi mwenzake ww hayo hayakuhusu nakushangaa unapata tabu ya nini?,wewe hoa huyo mwanamke wako hata kama huyo mtoto atakuwa pamoja na mama yake,kiubinadamu unawajibika kulea pia huyo mtoto kwasababu huko na mama yake,malumbano ya mwanamke wako na mzazi mwenzake kuhusu huyo mtoto ww hayakuhusu,waache wenyewe wapambane kama wataenda ustawi wa jamii au mahakamani ww hayakuhusu,na kama huyo mwanamke wako anataka aishi na mwanae hapo kwako mpokee na lea huyo mtoto tatizo nini kaka?na mama yake unae na unampenda?,

mambo ya kusema baba yake huyo mtt ana uwezo ww hayakuhusu kabisa,waache wenyewe wapambane mpaka hapo taratibu na sheria zitakapoamua kama mtoto anabaki kwa mama au aende kwa baba yake,kwahiyo nakushauri malumbano yao achana nayo,na story za mwanamke wako kusema huyu mtt yatima pia ww hayakuhusu, kwanini unaumiza kichwa?,kama baba yake yuko anafuatilia mwanae mwache afuatilie husiingilie na wala story za huyo mwanamke wako kusema mtoto ni yatima husisikilize,

kikubwa kwasasa kama huyo mwanamke wako atakuja kuishi na mwanae kwako naomba wapokee na watunze kama mzazi! huyo mtoto hana makosa yoyote,mpaka siku watakapokubaliana na mzazi mwenzake mtoto aende wapi,kwaiyo ww hoa huyo na mwanamke hata kama mwanae atakua nae,siku baba yake atakapomchukua sawa tu,ww utaendelea na maisha na mkeo lkn mambo yao husiyaingilie vyombo vya sheria vipo vitaamua na huyo mtoto husimnyanyapae mtunze hata kama baba yake ana uwezo kwakuwa kuna mgogoro

Kiswahili chako ni kigumu sana hasa kwenye matumizi ya VOWELS .. Unaweka H pasipohusika.. Mfano Hoa badala ya Oa, huko na mama yake badala ya Uko na mama yake... Unabadilisha maana ya maneno unayolenga..
 
Kwanza nikuombe samahani kwa ushauri wangu. Pili nikushauri kuogopa akinamama ambao wana watoto maana huwezi kuoa mtu na mtoto. Tatu mtoto kama ni wa kiume akikua takuchapa tu na ndiye atakuwa chanzo cha kuachana na mkeo. Nne mtoto na mzazi wake ni kidole na pete unaweza kuivua ila huwezi kuiacha aslani, nina maana wewe tunza lakini mwisho wa yote atarudi kwa baba yake tu

Mkuu umemaliza kila kitu kwenye red.

Note.
Zamani niliusiwa nisijaribu kuoa mke mwenye mtoto,labda awe baba wa mtoto amefariki.

Nasikia huwa wakionana hata kama mwanamke atakuwa amevaa nguo,basi yeye anamuona hadi maumbile yote ya ndani.

Akili kichwani mwako,ukimuoa tu,nakuahidi utarudi tena Jf kuomba msaada wa mawazo,kuna thread nyingi sana humu ndani,zababa mwenye mtoto nahisi anamla mke wangu.
 
Dear sio wanaume or wanawake wote wako hivyo mnavyohisi nyie . Jamani I have so many different friends wa kike/ kiume wameolewa na kuoa wakiwa na watoto si mtoto Bali watoto from their previous relationships. Na hao wanaume hawana watoto kabisa wameoa hawo wadada na wako happy raising those kids together ... na baba Wa watoto wako hai .. ( waume zao waliwapata through Fast and Prayers. They did that na kumake ahadi kwa Mungu ya sadaka. Na nilishuhudia kwa macho yangu . Siku walipooandika kwa karatasi what they wanted from God.. Na Mungu aliwajibu .. wanaishi maisha Furaha na Amani . Na tena kuna mmoja Mumewe kamuambia hana haraka ya kuwa na more kids since wanao 3 tayari (na hawa sio his biological kids) but its up to her to decide and he will follow it ) , jamani situngi hii ni kweli kabisa..

Jamani mwanamke kurudiana na Baby daddy wake huku akiwa ameshaaolewa na MTU mwingine kwangu Mimi naona ni tabia yake chafu tangu zamani hana msimamo , kutojiheshimu, kutojipenda, kutojithamini, ulimbukeni na kukosa maarifa. Kama haiku work before na baby daddy what makes her think ita work out now.? Ni upumbavu na amebomoa ndoa yake ya sasa mwenyewe kwa kukosa maarifa ( hapa ni kwa wale baadhi wenye tabia hizo chafu). Marafiki zangu hawajawahi kufanya hivi na wako happy na ndoa zao tena na kujuta kwa Ku waste their time with their ex aka baby daddy zao .. So sio wote wenye hiyo tabia mnayoiongelea. Thanks.
 
Twende PM baby...
 
Kiongozi, kwa upandewangu mimi I can understand and agree with your woman..ana point katika maelezo na msimamo wake

Kwanza ni asiimia kubwa ya wanawake wenye tabia za kuwatesa watoto wasio wa kuzaa wao

Pili the kid is still young...watu tunapenda sana kujifanya tumeendelea lakini kiuhalisia mtoto inabidi akae na wazazi au mzazi at least mpaka at the age of 12..sasa habari ya kumpeleka mtoto wa miaka 4 boarding sio nzuri

Tatu huyo baba mtoto angekuwa genuine asingeweka masharti kama hayo ya kutomhudumia mtoto mpaka asikilizwe yeye..na najiuliza hiyo ustawi gani wameenda ambako wameridhia baba asitoe matunzo kwa vigezo vyake baba

ninavyojua at that age mama ndo ana turufu ya kukaa na mtoto isipokuwa pale ushahidi ukitolewa kuwa mama haqualify kulea

Nakushauri usiachane na mpenzi wako, msaidie kulea mtoto wake bila kutegemea anything in return...namaanisha siku waki-renconcile na mzazi mwenzake wakaamua baba amchukue mtoto wewe uwe ready kufuata maazimio yao

Kila la kheri

To me this is the BEST comment!

Hta km ni kweli baba wa mtoto ni mzima, ana kazi nzuri nk kwa sababu kakataa kumlea mtoto akiwa kwa mama yake basi jitahidi umtunze tu huyo mtoto. Mtoto wa miaka minne (4) bado ni mdogo sana hivyo bado anahitaji malezi kamili ya mama yake mzazi.

Sikatai ni kweli anaweza akapelekwa shule ya boarding na huyo baba yake lakini fahamu wazi kuwa malezi ya watoto wadogo kwa 90% ni ya upande wa mama. Hivyo basi ni dhahiri bas huyo mama yake wa kambo itamlazim ajitwike hayo majukumu. Swali, Je atamlea kwa malezi STAHIKI?

Kubali tu kumlea mtoto, kumbuka mtoto hana hatia.
 
Dear sio wanaume or wanawake wote wako hivyo mnavyohisi nyie . Jamani I have so many different friends wa kike/ kiume wameolewa na kuoa wakiwa na watoto si mtoto Bali watoto from their previous relationships. Na hao wanaume hawana watoto kabisa wameoa hawo wadada na wako happy raising those kids together ... na baba Wa watoto wako hai .. ( waume zao waliwapata through Fast and Prayers. They did that na kumake ahadi kwa Mungu ya sadaka. Na nilishuhudia kwa macho yangu . Siku walipooandika kwa karatasi what they wanted from God.. Na Mungu aliwajibu .. wanaishi maisha Furaha na Amani . Na tena kuna mmoja Mumewe kamuambia hana haraka ya kuwa na more kids since wanao 3 tayari (na hawa sio his biological kids) but its up to her to decide and he will follow it ) , jamani situngi hii ni kweli kabisa..

Jamani mwanamke kurudiana na Baby daddy wake huku akiwa ameshaaolewa na MTU mwingine kwangu Mimi naona ni tabia yake chafu tangu zamani hana msimamo , kutojiheshimu, kutojipenda, kutojithamini, ulimbukeni na kukosa maarifa. Kama haiku work before na baby daddy what makes her think ita work out now.? Ni upumbavu na amebomoa ndoa yake ya sasa mwenyewe kwa kukosa maarifa ( hapa ni kwa wale baadhi wenye tabia hizo chafu). Marafiki zangu hawajawahi kufanya hivi na wako happy na ndoa zao tena na kujuta kwa Ku waste their time with their ex aka baby daddy zao .. So sio wote wenye hiyo tabia mnayoiongelea. Thanks.
Subiri kama ni boys wafike umri wa kujitegemea uone kazi. Sie tuna mifano mingi hai ambapo watoto wa kiume wanasuggest kwa mama zao waachane na mibaba ya kambo baada ya kutunza na the so called mibaba ya kambo. Akinamama at that point lazima waegemee upande wa watoto wao.
 
Kiswahili chako ni kigumu sana hasa kwenye matumizi ya VOWELS .. Unaweka H pasipohusika.. Mfano Hoa badala ya Oa, huko na mama yake badala ya Uko na mama yake... Unabadilisha maana ya maneno unayolenga..

Huwa ninapata ukakasi sana pindi nisomapo habari isiyozingatiwa matumizi sahihi ya alama za uandishi na mpangilio wa herufi.Mfano panapostahili R panawekwa L au badala hutaki mtu anaandika utaki​.
 
Wewe Kama mama mtoto wampenda mkubal na mtoto - Kwanza mdada huyo kesha kwambia ni yatima - Kuwa sehem ya mabadiliko ila kama vile ako na fix nyingi so bora awe open
 
Subiri kama ni boys wafike umri wa kujitegemea uone kazi. Sie tuna mifano mingi hai ambapo watoto wa kiume wanasuggest kwa mama zao waachane na mibaba ya kambo baada ya kutunza na the so called mibaba ya kambo. Akinamama at that point lazima waegemee upande wa watoto wao.

Dear sikatai yes kuna wengine it will happen that way. Yes Nina rafiki kama Dada to me anae son na amelelewa na step father since he was 2 years old . For now hivyo son Yuko college (sophomore this year ) na anampenda step father more than anything .. so as I said it depends . . Binafsi nninaamini mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Na samaki mkunje angali mmbichi akishakauka ni basi tena . Misemo yote niliaambiwagwa nikiwa nakuwa. Thanks.
 
mh! sasa kama wameenda hadi ustawi wa jamii na kisheria mtoto under 7 years anatakiwa kukaa kwa mama yake na baba ana wajibu wa kumuhudumia akiwa huko kwa mama yake....kama jamaa still kagoma, huyo mdada si angelipeleka hilo cortn! Maana sheria iko upande wake, unless jamaa awe na sababu za msingi zenye kuonyesha kasoro za huyo dada zitakazoathiri malezi ya mtoto.
 
Jaama atakuwa anatumika hapa mtu aokoe jahazi la usingle maza!! Hakuna kitu hapo.
Ila kama mmependana basi mwoane bila masharti.
Ni wazi kuna jambo linakusuta au your senses are telling you otherwise. Tunaweza kuandika mengi na ushauri lukuki lakni wewe you know you can trust your guts.
 
Mkuu nimekosea nini kuhoji uhalali wa kulea mtoto mwenye baba yake?

We jamaa ni mbinafsi Sana, hako katoto kamoja unakafikiria kwelikweli, hujampenda huyo Dada inaelekea. Ukitaka mtoto arudi kwa baba yake huko nako kuna mama mwengine, nae atahoji uhalali wa kumlea mtoto mwenye mama yake.

We funga macho tu, acha ubinafsi. Kubali tu kumlea huyo mtoto ambae hana makosa
 
mh! sasa kama wameenda hadi ustawi wa jamii na kisheria mtoto under 7 years anatakiwa kukaa kwa mama yake na baba ana wajibu wa kumuhudumia akiwa huko kwa mama yake....kama jamaa still kagoma, huyo mdada si angelipeleka hilo cortn! Maana sheria iko upande wake, unless jamaa awe na sababu za msingi zenye kuonyesha kasoro za huyo dada zitakazoathiri malezi ya mtoto.

Hamnq sababu zozote jamaa anajifanya kiburi tuu.
 
Back
Top Bottom