Anataka kuzaa naye tu mtoto hatamuhusu baba.

Bonge la ofa!Ila embu tutafakari

Bonge la ofa!Mtoto wa kike mpaka kasema ujue kapenda kweli,akimtosa atakuwa hakumtendea haki!Kwa namna maelezo yalivyo jamaa hawezi kuwa na tatizo na mkewe maana mwanamke ni muelewa huyo!lakini ajitahidi kucheza chini ya kiwango asijemfanya amn'gang'anie bure!
 
mtotowamjini Unajua sitaki kuamini kama huyu demu hana watu wanaotaka kumuoa wengine hata hawajaoa ila mabinti wasasa hivi wako selective sana.

aisee sio mabinti pekee hata wanaume pia wako selective...sasa kumpata mtu ambae kweli unaona anafaa kua mwenzi wako wa maisha ni ngumu...dunia saivi imebadilika...uaminifu ni zero kwenye mahasuiano siku hizi
 
Well said na nitajaribu kupeleka na jina lako kama ataridhia kuwa na wwe nitakujulisha.

Hujanitendea haki mkuu,kuna kitufe cha like hapo kwenye PC yako au hujakiona?Kwa suala la kupeleka jina wala hakuna gogoro,mwambie tu kuwa kuna mtu huku anaitwa Mtakatifu Paka mweusi yuko singo na anakidhi vigezo,na kama nitakuwa sina baadhi ya vigezo mwambie nitakopa kwa mtani wangu Chimunguru ili aridhike na aache kutamani mume wa mwanamke mwenzie.......
 
Last edited by a moderator:
Gari , Nyumba na mafanikio aliyinayo ni yake......Usipoteze damu yako kwa mali zake.Wala usimsaliti mke wako kwa tamaa zake.
 
mwenzako akinyolewa tia maji. wadada mlioko humu mliolewa mjifunze kuwaombea waume zenu, wanajaribiwa sana na wadada,wake za watu, ili mradi kuhatarisha usalama wa ndoa.

kama hawawezi kujiombea wenyewe shauri yao. Si jukumu langu kulinda ndoa, bali ni jukumu letu sote.

Hivyo basi kila mmoja atimize wajibu wake wa kulinda ndoa, kinyake, bila kushurutishwa, kuombewa, kufuatiliwa wala kukumbushwa.
 
1}. Kwa heshima ya rafiki yake, kaka ya mwanamke asikubali kitendo hicho. Kumzalisha na kumuacha itachukuliwa na rafiki yake ni kitendo cha kuharibu maisha ya dadake ingawa atakuwa amefanya hivyo kwa ridhaa ya mwanamke lakini kaka hatafahamu hilo na kusababisha kuvunyika kwa mahusiano yao ya muda mrefu yaliyokuwa na heshima kwa familia zote na hata marafiki zake wengine wa karibu watamdharau na watamuogopa kwa hilo.

2). Haitawezekana kama mwanamke anavyodai kuwa akizaa asijali kuhusu mtoto. Kwanza jamaa nafsi itamsuta kwa kumtelekeza mtoto wake kwakuwa hiyo ni damu yake haina tofauti na ya mtoto wa ndoa. Pili, uzoeefu unaonesha kwamba mwanzoni mwa mapenzi mwanamke anakubaliana na hali zote kuwa hatakusumbua kwa mkeo, mchumba au hata rafiki yako uliyenayo kabla yake. Ukweli ni kwamba mnapoingia kwenye mahusiano na mapenzi yakashamili mwanamke anakuruka na anasahau yote mliokubalina na anajiona ana haki sawa kabisa na uliyenayo kabla yake hata kama ni mkeo, hivyo atamsumbua sana na ikiwezekana atafanya kila liwalo ili mke wa jamaa afahamu. We don't live in a theoretical world, We do live in a pragmatic world ambapo haya yote ninayokueleza yanatokea. Mambo haya hayana elimu kusema kuwa eti ni professor ataelewa, hakuna kitu, jamaa ataharibu mahusiano ya ndoa yake bure, asifanye hilo.

3). Mwanamke kama alikuwa anampenda angemweleza jamaa kabla ya kuoa, au angefanya juhudi za kumtafuta lakini inaonesha walikutana tena by chance. Jamaa ni mwanaume asidanganywe na elimu na vijimali vya mwanamke. Nawakumbusha wanaume wenzangu kuwa wanaume tunapaswa kuwajibika kwa wake zetu, tunapaswa kuwatunza wake zetu na watoto wetu kuanzia chakula, malazi, nguo, elimu, matibabu, starehe na mambo yote yanayohusu maisha ni jukumu letu sisi hata kama mwanamke anafanyakazi hiyo ni just an added advantage. Kwa hiyo jamaa asiwe na tamaa ya zawadi itakayoharibu maisha yake ya ndoa. We need to live with respect and dignity tusishawishike na vitu vidogo tukapoteza thamani yetu na utu wetu kwa jamii iliyotuzunguka.

Rafiki yangu mmoja jana tukiwa mahali alinipa kisa kinachohitaji mchango wa mawazo yako.
Kuna mrembo mmoja ambaye jamaa alijuana naye kupitia kaka yake(ie kaka wa huyu mrembo na huyu rafiki yangu walikuwa marafiki mpaka wakawa wanatembeleana nyumbani hapo ndo chanzo cha huyu mrembo kumjua huyu rafiki yangu.)Miaka kama 5 imepita bila yule jamaa kuonana na yule dada wa rafiki yake ambaye yeye alikuwa anamchukulia kama ni mdogo wake pia.
Juzi kati ghafla wakakutana Benk na yule mrembo wakaongea kidogo ikiwa ni pamoja na kubadilishana namba za simu.
Ikapita kama siku 4 mara simu ikaita kucheki ni yule mrembo wakaongea kikubwa yule mrembo akamuomba wakutane week end inayofuata.
Ikafika hiyo siku wakakutana wakaongea mengi sana na yule mrembo akatumia fursa hiyo kumweleza jamaa kwamba alikuwa hayupo nchini alienda Uingereza kuchukua Masters yake na ameshajenga nyumba yupo kwake ana gari 2.
Na ana pato zuri tu kwa mwezi.
Huyo Mrembo ndo ana miaka 29 sasa hivi.
Jamaa akafuraia mafanikio aliyofikia kwa kumpa hongera sana.
Yule binti akamwambia "Si nilichokuitia ila naomba usinifikirie vibaya kwani najua wewe ni rafiki mkubwa wa kaka yangu na ninajua una mke,Ninachoomba kwako ni nahitaji kuzaa na wewe kwani nimekuwa nikikupenda kwa mda mrefu sana ila niliogopa kukuambia mpaka ukaja kuoa ninachoomba kutoka kwako ni unipe mimba then mtoto atakaye zaliwa hasikuhusu kabisa kama una ogopa itakuletea shida kwa mkeo.
Na naomba sana usinifikirie vibaya kwani ni ukweli nakupenda sana na ukinikubalia nakuhaidi nitakupa zawadi nzuri sana"

Jamaa akamwambia nipe mda kidogo nifikirie then nitakupa jibu ndo jamaa kanitafuta jana kanipa kisa hiki.
Anaomba mchango wangu pamoja na wako juu ya hili.
 
1}. Kwa heshima ya rafiki yake, kaka ya mwanamke asikubali kitendo hicho. Kumzalisha na kumuacha itachukuliwa na rafiki yake ni kitendo cha kuharibu maisha ya dadake ingawa atakuwa amefanya hivyo kwa ridhaa ya mwanamke lakini kaka hatafahamu hilo na kusababisha kuvunyika kwa mahusiano yao ya muda mrefu yaliyokuwa na heshima kwa familia zote na hata marafiki zake wengine wa karibu watamdharau na watamuogopa kwa hilo.

2). Haitawezekana kama mwanamke anavyodai kuwa akizaa asijali kuhusu mtoto. Kwanza jamaa nafsi itamsuta kwa kumtelekeza mtoto wake kwakuwa hiyo ni damu yake haina tofauti na ya mtoto wa ndoa. Pili, uzoeefu unaonesha kwamba mwanzoni mwa mapenzi mwanamke anakubaliana na hali zote kuwa hatakusumbua kwa mkeo, mchumba au hata rafiki yako uliyenayo kabla yake. Ukweli ni kwamba mnapoingia kwenye mahusiano na mapenzi yakashamili mwanamke anakuruka na anasahau yote mliokubalina na anajiona ana haki sawa kabisa na uliyenayo kabla yake hata kama ni mkeo, hivyo atamsumbua sana na ikiwezekana atafanya kila liwalo ili mke wa jamaa afahamu. We don't live in a theoretical world, We do live in a pragmatic world ambapo haya yote ninayokueleza yanatokea. Mambo haya hayana elimu kusema kuwa eti ni professor ataelewa, hakuna kitu, jamaa ataharibu mahusiano ya ndoa yake bure, asifanye hilo.

3). Mwanamke kama alikuwa anampenda angemweleza jamaa kabla ya kuoa, au angefanya juhudi za kumtafuta lakini inaonesha walikutana tena by chance. Jamaa ni mwanaume asidanganywe na elimu na vijimali vya mwanamke. Nawakumbusha wanaume wenzangu kuwa wanaume tunapaswa kuwajibika kwa wake zetu, tunapaswa kuwatunza wake zetu na watoto wetu kuanzia chakula, malazi, nguo, elimu, matibabu, starehe na mambo yote yanayohusu maisha ni jukumu letu sisi hata kama mwanamke anafanyakazi hiyo ni just an added advantage. Kwa hiyo jamaa asiwe na tamaa ya zawadi itakayoharibu maisha yake ya ndoa. We need to live with respect and dignity tusishawishike na vitu vidogo tukapoteza thamani yetu na utu wetu kwa jamii iliyotuzunguka.

Umemaliza kila kitu mkuu na kama wewe si Teacher basi ni Mtumishi,hahahahhahhahahahah am kiding.
 
Back
Top Bottom