Anatafutwa: Joaquim Lewanga

Anatafutwa: Joaquim Lewanga

Offline User

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
3,828
Reaction score
2,395
Wanajamii,
Mtajwa hapo juu ni rafiki yangu tulopotezana tangu mwaka 2008. Alimaliza Sheria UDSM mwaka 2006. Mara ya mwisho alikuwa ni Solicitor Mtwara. Mwenye kujua 'whereabouts' zake anifahamishe tafadhali au kama mwenyewe yupo hapa jukwaani ajitokeze!! - natanguliza shukrani za dhati.
 
Kuna familia fulani naifahamu mdada alipata tatizo kama la huyu ndoa ilifungwa, mdada akamwomba mumewe aoe mdogo wake mwanamke ili amzalie watoto. Na mpaka sasa wanaishi vizuri tu.

Lewanga alishafariki kwa ajali huko mtwara. RIP
 
Kuna mdau kani-PM kuhusu hiyo habari. Imenisikitisha sana! Alikua rafiki wa karibu sana! Mkuu una clues ilikuaje hyo ajali? Mwezi gani na alizikwa wapi? RIP Ras Joa
 
Tongs nafikiri ni kwenye mwezi february kwenye tarehe za 26 angalia mtandao wa malafyaleleoblogspot.com
 
Last edited by a moderator:
Kuna familia fulani naifahamu mdada alipata tatizo kama la huyu ndoa ilifungwa, mdada akamwomba mumewe aoe mdogo wake mwanamke ili amzalie watoto. Na mpaka sasa wanaishi vizuri tu.

Lewanga alishafariki kwa ajali huko mtwara. RIP
Kabendesa najua Tongs anaweza akawa amekuelewa ila mi naona umenichanganya sana humo nilimo bold, underline and italicise. Please nifahamishe vema nikuelewe mkuu. Samahani lakini
 
Last edited by a moderator:
Kabendesa najua Tongs anaweza akawa amekuelewa ila mi naona umenichanganya sana humo nilimo bold, underline and italicise. Please nifahamishe vema nikuelewe mkuu. Samahani lakini

Mi nimemuelewa mkuu! Hayo ulobold hayanihusu kwa kweli! Naamini kakosea tu si unajua!
 
Last edited by a moderator:
Wanajamii,
Mtajwa hapo juu ni rafiki yangu tulopotezana tangu mwaka 2008. Alimaliza Sheria UDSM mwaka 2006. Mara ya mwisho alikuwa ni Solicitor Mtwara. Mwenye kujua 'whereabouts' zake anifahamishe tafadhali au kama mwenyewe yupo hapa jukwaani ajitokeze!! - natanguliza shukrani za dhati.

Alilifariki mwezi wa pili kwa ajari ya gari. Alizikwa Kwao Moshi kama siku tatu au nne baadae. Mzazi mwenzie na mwanae bado wapo Mtwara. Pole sana kwa kufiwa na rafiki. Mimi alikuwa ni mme mtarajiwa wa classmate wangu UDSM
 
...........Je ni huyu...........
Ajali mbaya imetokea jana jioni mtwara maeneo ya msijute ikiwaua Mwanasheria wa Manispaa-Bw Joachim Lewanga Shayo aliyekuwa akielekea Masasi na Dereva bajaji wake na kumvunja viungo mwanamke mmoja baada ya kugongana uso kwa uso na gari la pili la tanesco makao makuu likija mtwara. Ajali imetokea maeneo ya Hiyari/Msijute wakati Marehemu alipokuwa akitaka kulipita gari lingine ndipo wakakutana uso kwa uso. Taratibu za msiba zinaendelea nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mangowela-Mtwara. Kwa walio Mtwara na kwingineko tafadhali mjulishe ndugu jamaa na marafiki na wenye kuitakia mema familia ya Marehemu Shayo.
BWANA ALITOA BWANA AMETWA JINA LA BWANA LIBALIKIWE

...........very sorry but.......

kutoka kwa
malafyaleleo.blogspots.com Tuesday, February 26, 2013
 
Back
Top Bottom