Anatafutwa- Edmund Alisoma Tampere Finland 1990-1994

DALA

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,251
4,638
Salama wakuu!!

Poleni na majukumu. Kuna ujumbe unasambazwa kwenye magroup ya WhatsApp kuhusu mtajwa hapo juu (Edmund) kwa bahati mbaya wanaomtafuta hawajui jina lake la ubini ila wanadai kwamba huyu jamaa (Edmund) alisoma Tampere Finland kati ya mwaka 1990-1994 ambapo alikutana na dada mmoja Mzungu (Mfini) wakavunja amri ya sita na kwa bahati nzuri/mbaya jamaa walimtunga mimba huyo binti wote hawakuwa na taarifa na kwa kuwa ilikuwa tukio la siku moja, kila mmoja alichukua hamsini zake na kuendelea na maisha yake bila ya kuchukua mawasiliano yoyote.

Dada alitunza na kulea mimbaambapo baadae alijifungua mtoto wa kiume ambaye kwa madai yao ni mtu mzima sasa ila hamjui baba yake na angependa angalau kumfahamu.

Kwa yeyote mwenye kumjua Edmund au familia yake tuwasiliane ili niwaunganishe na anayehusika (Ni Mtanzania aliyekutana na huyo mtoto anaishi Finland)
 
Duuuh isije ikawa ni mimi maana na mimi niliwahi kuonja Madada wa huko nilipokuwa nasoma huko
 
Ivi hii c kazi ya kufanya balozi ama,au mabalozi wetu ni wavivu katika inshu kama izi
 
Wakina kaka mnapoteza DNA zenu sana tu, afadhali sisi wadada tukienda nje labda tuolewe kwa kutafuta makaratasi, lakini tunarudi numbani salama hatuachi reference kirahisi.
 
Wakina kaka mnapoteza DNA zenu sana tu, afadhali sisi wadada tukienda nje labda tuolewe kwa kutafuta makaratasi, lakini tunarudi numbani salama hatuachi reference kirahisi.

Inategemea ati
 
Aende chuoni atalipata jina kwa ukamilifu kisha aende ubalozi wa Tz atapata Maelezo yake. Chuoni pia atapata kujuzwa Advance au 1st Degree alisoma wapi

Ni changamoto
 
Back
Top Bottom