Anatafuta nini kwenye simu yangu?



Kwa majibu yote hayo, nadhani akili itakukaa sawa Bujibuji.
 
Last edited by a moderator:
Hapa kuna nini msiri wangu mwaJ?
 
Last edited by a moderator:

Yaelekea ulishamweka kwenye mazingira ya wewe kutoaminika. Au yawezekana ana inferiority complex
 
We acha tu msiri wangu, hapa kuna matatizo makubwa. Bujibuji aliachwa kwenye mataa na Madame B sababu ya kuwa na domo zege akachanganyikiwa alipoibuka akadhani mie ni mkewe wakati hata kuoa alikuwa bado.
Mapacha tumewapata wapi?
Mbona ulikuwa ukinihubiria kuwa kina Zion Daughter ni wanangu wa mbegu na Mwita Maranya mtarimno mkubwa umelala doro?
 
Last edited by a moderator:
We acha tu msiri wangu, hapa kuna matatizo makubwa. Bujibuji aliachwa kwenye mataa na Madame B sababu ya kuwa na domo zege akachanganyikiwa alipoibuka akadhani mie ni mkewe wakati hata kuoa alikuwa bado.


Orait orait "Anyone who has never made a mistake has never tried anything new" -
Albert Einstein
 
Uwe unampa mapema apekue kabla hujalala mkuu so that ukillala asipekue
 
Mpe dose ya kutosha huo usingizi atakaopata hata cm hatakumbuka kugusa. Acha kuwa selfish ukimaliza tuu ww ushaanza kukoroma lazma atafute kinachokuchosha kupitia cm yako 😀
 
Bujibuji vipi bado haujapona? Moyo bado unadundia nyayoni?
mwaJ j hebu click hapa chini kwenye hii link
http://ia600209.us.archive.org/19/items/BusuPandeTatu/03BusuPandeTatu.wma

[BUSU PANDE TATU - BIMA]
(Bima Lee, mwaka 1989 kibao kilitungwa na Max Bushoke, kuimbwa
nae pamoja na Jerry Nashon, Athumani Momba, na Bwana Mugunda)

(Bushoke)
vipi penzi lajisuta lenyeweeeeeee

vipi sasa mbona lajisuta lenyewe
ulipokubali kunipenda ah ah
hukulazimishwaa
uliahidi kwa ahadi na viapo pia
uliahidi kwa ahadi na viapo pia
mwanzoni ilikuwa penzi motomoto
busu pande zote tatu za uso ohooooo

(wote)
ukweli nimeuona kwenye hili penzi letu
mwenye pendo la udanganyifu sasa ameonekana
kwenye mapenzi ya kweli
watu hushirikiana sheri
kwenye dhiki na faraja
kote hushirikiana
viko wapi sasa jamae
maneno ulionieleza
NAKUPENDA HAKUNA MWENGINE TENA
KUMBE YOTE NI UONGO

(Nashon)
uko wapi sasa moto wa mapenzi yetu mimi na wewe.. mimi nawe mamaa
uko wapi sasa moto wa mapenzi yetu mimi na wewe
mbona umezimika hata majivu hayaonekani
mamiii mamiiiii

(wote) Kibwagizo
ama ni kweli mapenzi hayana mdhamini
nimeamini
yaweza vunjika wakati wowote

(Nashon)
ama ni kweli mapenzi hayana mdhamini
duniani duniani siku hizi
I love you busu nyingi ........ uongo huo
mamii mamiii

(wote) kibwagizo

(Nashon)
uko wapi sasa moto wa mapenzi yetu mimi na wewe
mbona umezimika hata majivu hayaonekani
mamii mamii

(wote) kibwagizo
 
Last edited by a moderator:

Naona midundo ya moyo imegoma kutoka nyayoni. Itabidi tukuchangie ukatibiwe India.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…