Anasema hanitaki lakini haishi kunitumia text

Anasema hanitaki lakini haishi kunitumia text

gambakhuffu

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2010
Posts
509
Reaction score
547
Habari zenu wana bodi,
Kuna binti nilikuwa na date naye lakini hapa katikati ikatokea kutoelewana na isitoshe tupo ofisi moja, yote ni kwa sababu ya maneno yaliyoibuka ndipo akasema kuwa hataki mahusiàno na Mimi, lakini cha kushangaza haishi kunitumia jumbe mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii hata kwenye simu. Na text zake zote zinafanana kama ilivyokuwa awali wkt bado uhusiano upo on peak.
Hapo mwanzo nimejaribu kumbembeleza arudishe roho nyuma ili tuendelee lakini amebaki kuwa na msimamo uleule na cha kushangaza text anazotuma ni hadi usiku wa manane.

Nashindwa kuelewa msimamo wa huyu binti na mara zote hapo nyuma alikuwa analazimisha nimvishe pete lakini sikuwa nimejipanga na amekuwa mdadisi kwa watu kwa kila hatua ninayopiga mbaya zaidi nikimchomekea turudiane anakuwa mbogo na ameanza hata kuniamkia kitu ambacho hakikuwa kawaida hapo kabla.

Hii hali imeniumiza sana kwani binti amebaki kuwa na msimamo tata na ukweli ni kwamba tulishibana sana hadi coworkers wakawa wanaona wivu na kwa hivi sasa imekuwa kama vile wanashangilia kuona love birds tumetengana.

Naomba ushauri wenu wana jamvi nifanye nini kuepukana na hii hali na labda nimweleze nini ili tuendelee kama zamani.

Nawasilisha!!
 
Tangaza ofisini kwenu umepata mchumba upo kwenye process za kuoa
Kweli kabisa..
Hiyo inaitwa sitaki nataka. Anataka akuumize tu halafu baadae akurudie. Tangaza una mchumba basi,tafuta hata picha ya demu mmoja mkali weka peofile picha whatsapp andika usingizi wangu iache siku mbili utaona madongo atakayokupa,utasikia mara ooh mzuri mara ooh kumbe ndio wifi hamna lolote roho itakuwa inamuuma na atalia na moyo wake mchana na usiku.

Ila we naee kuwa mwanaume,kaza roho hiyo kwani huyo ndio demu wako wa kwanza,kwani kakukuta bikra???mbona unadharirisha wanaume wenzio we nawe!!!!? Ghkaaa!!!
Hebu jichetue kidogo na yeye aumie then kama unampenda mvalishe hiyo pete hata ukioa 2030 ilimradi pete anayoitaka umempa.
 
Mwanaume ni machine + misimamo sasa wewe kimoja hapo huna yaani hujatimia
Katika mashine najiamini cz sina historia ya kuwaacha juujuu, ikifika asubuhi alikuwa anachechemea kwa shughuli ya jana yake
 
Mwambie unataka kuoa asikutumie tena text only if u can
Kama bado hujielew MPE mshahara wako wote atakuelewa
 
Kweli kabisa..
Hiyo inaitwa sitaki nataka. Anataka akuumize tu halafu baadae akurudie. Tangaza una mchumba basi,tafuta hata picha ya demu mmoja mkali weka peofile picha whatsapp andika usingizi wangu iache siku mbili utaona madongo atakayokupa,utasikia mara ooh mzuriara ooh kumbe ndio wifi hamna lolote roho itakuwa inamuuma na atalia na moyo wake mchana na usiku.

Ila we naee kuwa mwanaume,kaza roho hiyo kwani huyo ndio demu wakk wa kwanza kakukuta bikra???mbona unahdaririsha wanaume wenzio we nawe!!!!? Ghkaaa!!!
Hebu jichetue kidogo na yeye aumie then kama unampenda mvalishe hiyo pete hata ukioa 2030 ilimradi pete anayoitaka umempa.
Maserati you're talking real, nimeipenda ushauri wako kwani kwa uchizi tu nimo ila karibuni nimejifanya mlokole flani. Iyo plan lazima nitaibuka nayo, hahaha!!
 
Inakuaje una kuwa na demu ofisi moja mkuu?
Mkuu imetokea tu, hata mi mwanzo sikuafiki lakini mtoto akawa amekolea bila kujali macho ya watu, lakini nikampa masharti mapenzi yetu yawe nje ya ofisi na hata tukiwa ofisini no body should notice, lakini bahati mbaya mambo yakaanza kuvuja kutokana na ukaribu uliokuwepo ukilinganisha na wafanyakazi wengine, hapo ndo yakaanza maneno!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom