Anasa hizi kumpa hasira Mh Rais.Huponza na wasiohusika

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Tunapofanya matukio na kuweka mapicha hadharani, tujue kabisa yanamfikia Mh Rais na ni hasara,kibano kwetu sisi, hatumkomei yeye, tunajikomoa sisi.

Utakuta watu wawili wamekaa bar, wanachupa za bia 40 kwenye meza yao.Hii ina effects zake kwenye mambo ambayo Mh Rais anakuwa anaamini tuna pesa ya 'bata'.

Sherehe zinafanyika za kufuru, watu wanakula mvinyo mbaya kabisa.Pesa wanatoa wapi?

Utakuta mtu ana kadi za harusi 10, za send off 7, za kitchen party 3 na zote anachangia kuanzia elfu 50 mpk laki na nusu.

Mh Rais, endelea na "muziki mnene". Sisi n wagumu kuelewa.
IMG-20170108-WA0000.jpg
IMG-20170107-WA0177.jpg
 
Pointless.........
 
Mleta mada unaonekana kazini kwako unavaa viraka,ili tajiri yako asikuone kama una pesa.
Aliekwambia Rais ana shida na pesa yako nani?mtagombana na Magufuli kama umezipata pesa kwa wizi au hulipi kodi bas.
 
Ukishakuwa masikini kila MTU utamuombea awe masikini ndo maana uswahilini hakuna maendeleo, hata pabanwe vip hatuwezi fanana maisha sasa km MTU anavitega uchumi vyake vya halali kaamua kula bata maisha magumu kwetu lkn waliojipanga vizuri wanapeta tu.
 
Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake. Kuna watu wanafanyakaz kama punda, Wameajiriwa, wanabiashara, wanalima, wanahisa kwenye mabenk na makampun makubwa kwanin wasitumie? Mleta mada kuwa mpole Mkuu.
 
Sasa kama wanafanyakazo au biashara na kupata pesa zao, tabu ipo wapi wao kula maisha wanavyotaka?

Hata akiendelea kubana abane, wale wanaokula wasivyostahili ndio wanaohumiabna kulia lia. Na hapo waliozoea madili ya pesa za wananchi.

Kila mtu na maisha yake, acha watanue kama wanauwezo.
 
Hivi kwa akili zenu mnqdhani kuna mtu wa kipato cha juu aliyeyumba?? Ukisikia maumivu ujue walengwa ni wale wa kipato cha chini ambao mzee anawqita wanyonge,,hata akaze vipi ataua raia wake kama nyie,tena azidishe haswaaa,apambane na wanyonge wake waliomweka hapo
 
Back
Top Bottom