Anapodai macho yangu yanamtongoza...

Anapodai macho yangu yanamtongoza...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,504
Reaction score
911,249
Adai kweli sijamtamkia, lakini ajua ninamtaka!
Adai macho yangu yanamchokoza, siju kivipi!
Adai nayo yanambipu, lakini yeye bado ni nguli!
Akiri sijamkonyeza, lakini macho yambembeleza!
Rafikize kawatonya, mimi ninamchemkia yeye!

Sijui ninachemka vipi, kwani sijalonga mie!
Kama kaandikiwa, mie kwake sina ujanja!
Itabidi nijisalimishe, hivyo awe na subira!
Kigori hasikii bali naye kunizulia majambo!
Rafikize kawatonya, mimi ninamchemkia yeye!

Ni kweli mtoto wa watu kaumbika lakini, Mmh!
Aaache domo kaya, kwani ananiaibisha mie!
Jicho halina pazia na nionacho nilete raha!
Lakini jicho kusisim'ka haimaanishi ni moyo!
Rafikize kawatonya, mimi ninamchemkia yeye!


N.B........................yatosha kwa leo!
 
Rutashubanyuma siku nyingi sijakuona aise na ukiingia tuu waingia na kigongo
Hope uko salama
May be macho yako yamekaa kimtego aise
 
Last edited by a moderator:
Rutashubanyuma siku nyingi sijakuona aise na ukiingia tuu waingia na kigongo
Hope uko salama
May be macho yako yamekaa kimtego aise

Nipo! Anatakiwa kutofautisha kunivuta na siha yake murua na mimi kumkubali...............AISEEEEEEEEEE!
 
ndio maana yake, yaano moyo wako umefunuka kabisa mbele ya mrembo so hauna pa kujifichia labda uvae mawani ya mbao!

Atakiwe awe na subira kwani penzi ni kikohozi na haliwezi kufichika...........
 
Wengine hadi nikimkodolea mwanaume mwenzangu bado mnatuzaba vibao...

Labda humkodoloi ila watongozea kwa macho pia...........bila ya kujijua. Jichunguze kofi haliji vivi hivi.
 
Back
Top Bottom