Mimi ni mfanyakazi wa serikali kwa bahati mbaya nimejaaliwa huruma.
Nina watoto wanne kila mmoja na mama yake na kila mmoja ana historia yake ya kuachana nao.
Hivi majuzi kuna mchepuko umenitamkia wazi kuwa anataka mtoto,umri umeshamuenda sana.
Nimeingiwa na huruma sana na kwa vile yeye ni mwajiliwa serikalini akili imeniambia nizae nae tu atalelewa vyema na mama yake sababu imekuwa kawaida ya siku hizi kuwa na single mama.
yeye presha imemtawala kwani hivi karibuni aliambiwa ana uvimbe na ili usiwe kero azae mtoto.
Karibuni tena alinikutanisha na ndugu yake,baadae akanionesha sms ya ndugu ake alienioneshea akimwambia hata huyu ameshindwa kukupa ujauzito?.Siku nyengine ilibahatika kumuona baba yao,niliingiwa na huruma na kujiuliza mkwe hana hata mjukuu wa kumpigia kelele,huruma tu.
Jamani nimeingiwa na huruma na mke wangu alishanasa mawasiliano na ameanza kuufuatilia huu uhusiano wetu natamani nimwambie tu kuwa huyu nae ana taka mtoto tu.
Nisaidieni nitaeleweka nyumbani?huruma imenijaa na naona hakuna sababu ya yeye kuwa mnyonge kisa mtoto.