Anaomba msaada ili aweze kumaliza form four mwaka 2014.

Secret Star

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,567
2,000
Kijana Shadrack kifaru ana shida kubwa kwa sasa wazazi aliokuwa akiwategemea kwa ajili ya kumsomesha wapo hoi kwa maradhi wote kwa pamoja mama yake mpaka sasa amelazwa muhimbili mwezi wa tatu akisumbuliwa na Kansa ya Ngozi, Pia baba yake ni Kilema na hajiwezi kwa lolote yupo Huko Songea. Kijana Shadrack kwa sasa yupo Kidato cha TATU huku akiwa ni miongoni mwa wanafunzi watatu Bora katika Darasa.. Ndoto zake zimeanza kufifia baada ya mama yake aliyekuwa akimsaidia kwa hali na mali kuugua gonjwa hili hatari na kwa sasa hajiwezi Tena... Shadrack anaomba msaada kwa yeyote mwenye uwezo aweze kumsaidia, aweze kumaliza Kidato cha Nne salama kwani anaamini bila kusoma Maisha yake yeye na familia yake kwa ujumla yatakuja yawe magumu zaidi mbeleni... Kwa yeyote aliyevutwa na hili anaweza kuwasiliana nami kwa Simu no 0764435828 ambapo nitamuunganisha moja kwa moja na kijana huyo anayehangaika huku na huko akitafuta msaada wa kusomeshwa.. (kwa sasa yupo mbagala)

UWEKEZAJI BORA NI ELIMU
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom