Kwa hiyo akitangulia mtoto then ndoa ndio itadumu milele?
Heshima kwenu wanajamvi.
Umri wangu unakaribia 30. Nina mpenzi ambae tulipanga tufunge ndoa siku za karibuni. Ajabu ni kwamba sasa hivi anataka nimzalie mtoto ndoa 'itakuja tu'! Napata wasiwasi. Nimeshamkatalia ila naona hanielewi. Sasa hivi hataki kuongelea ndoa tena! Anachotaka ni mtoto TU.!!!!! Na ukianzisha habari ya ndoa anabadilika mpaka sura!!!Nahisi anatafuta sababu tuachane. Nimemwambia nipo tayari kusubiri, kama anayo nia tufunge ndoa ndio tuwe na mtoto. Natamani sana kwenda altareni na shela jamani! Ndio sala yangu kila siku. Hata kama hakutakuwa na sherehe kubwa nachotaka tu ni ndoa! Jamani mlio oa au kuolewa mlipitia haya? Naona nimechoka.
Suala siyo kutangulia mtoto, jamaa anaonekana hajajipanganga kwa hizo sherehe zenu za mashela. Wakae chini wakubaliane, wakatambulishane kwa wazazi, mahali itolewe waendelee na maisha. Hayo mengine watajipanga baadaye. Ndoa ni makubaliano ya watu wawili wakipewa na baraka za wazazi! Kuna ndoa ya kidini, kiserikali na kimila. Kidini ni ile inayohusisha wachungaji,mashehe na mapadri, ya kimila mnamaliza kila kitu nyumbani na ya kiserikali mnaenda kwa mtu wa viapo bomani. Mara nyingi ya kidini huwa inaunganishwa na ya kiserikali ndo maana vinatolewa vyeti vitatu. Sasa kama jamaa hiyo sherehe ya mashela haiwezi na we una hamu ya mume, chagua kitu ambacho ni simple. Ndio maana kukawa na kubariki ndoa na siku hizi wamerahisisha kuna ndoa za jumuia aafu zinagharamiwa na kanisa. Tatizo lenu mnataka sherehe na sio ndoa.
Kama kweli tatizo ni kujipanga kwa sherehe,hapaswi kuwa mkali na ku demand mtoto badala yake aongee na mwenzi wake watakubaliana. Katika aina zote za ndoa ulizotaja hakuna hata moja ambayo jamaa ame opt,yeye kaja na yake mapyaa ya kutaka mtoto kwanza ndoa itakuja tu!
Aseme kama tatizo ukata ataeleweka watafunga wanayo afford.
Ukweli unaufahamu, wadada wa siku hizi wanatafuta sherehe ya harusi kuliko ndoa. Yawezekana jamaa amekerwa na kila siku kuôngelewa mambo ya mashela!! Seriously, hata mimi nikiona maongezi yako yametawaliwa na sherehe za harusi kuliko maendeleo nasepa. Mara sijui x alipendeza hivi, y sherehe yake siku fulani! Yananihusu? Na wengine wanatuomba na hela kabisa wakachangie harusi! Nikutoe out, hela ya kusuka, pads, nguo, viatu mpaka mchango wa harusi!!
inaelkea mbahili ukute hutoi ht hio hela mmmnh:shocked::shocked::shocked:
kimbiaaaaaaaaa
hili ndio tatizo kubwa la watoto wa kike,akisikia ndoa hata na kichaa ataolewa ilimladi avae shela.....
labda nikuulize, mmekuwa kwenye uhusiano kwa miaka mingapi? Ameshatoa mahali au kujitambulisha kwenu? Huu ndo ujinga wanaofikiria wadada wa siku hizi. Wanachowaza wao ni kuvaa mashela tu huku hata kupika hawawezi. Na siku hizi tumewastukia. Mambo ya kusupp ndoa hatuyataki tena. Tunaoana kimya kimya, kama hufai tunaachana kimya kimya. Na ukichelewa hapo visichana vidogo vinakupora huyo mwanaume. Bora mi nimeshaanza kugandwa ili nimpe mimba..