Trapped to a married man

Maya Angelou

JF-Expert Member
Oct 19, 2019
1,081
2,487
Naomba tu niseme kuna wakati kwenye maisha huwa hatutegemei baadhi ya mambo yatutokee ila inabidi tukubaliane na hali halisi.

Najua humu kuna watu tunajuana nao personally kiundani sana and am sorry if my confession will dissapoint you in anyway.

Back to my story 2015 nilikutana na huyu kaka tukawa marafiki na baadae tukawa wapenzi lakini aliniambia ameoa,
kipindi hicho I was so young and naive nilikuwa chuo kwakweli nakubali nilikuwa sijielewi, mahusiano yetu tuliendelea kwa miaka miwili mpaka baadae tulipoachana kwa sababu fulani.

Kipindi tulipo achana hakuacha kunitafuta meseji za hapa na pale hapo hatukuwa tukionana.Kwakweli sijawahi kutoka na mume wa mtu zaidi ya huyu na nilijisemea sitorudia tena kwaio nilisimama kwenye huo msimamo.

Fast foward this year tulionana alikuja kikazi mji niliopo tukaanza kuwa karibu tena na kwa sasa niseme ni wapenzi tena.

Kitu kinachofanya nije hapa kuomba ushauri ni kwamba huyu bwana anataka kunioa,we have this connection ni ngumu sana kuelezea jamani hiki kitu kimeniacha njia panda,anataka tuoane na nimzalie mtoto,anataka kuja nyumbani kujitambulisha afate process zote. Plan yake tufunge ndoa kisiri mimi yeye na watu wa karibu kama familia.

The future is promising amejicomit kuhusu mambo mengi na hili linazidi kuniogopesha.

Kitu cha ajabu nimeanza kulifikiria hili jambo in a serious way maana sikuwa na mpango nae lakini huku tunapoelekea mambo yanazidi kuwa magumu. Tumepanga apartment huku tukianza ujenzi wa nyumba na ana plan kuhamia mji niliopo na kuiacha familia yake mji mwingine.

Meanwhile upande wa pili kuna kaka ambae hajaoa anataka kuja kutoa mahali, well paying job we have a connection lakini hajafika level za yule mume wa mtu.

To be honest wote wawili nawapenda,nimeshindwa kujigawa au kufanya maamuzi.

Najiuliza hivi mume wa mtu anaweza kupenda tena nje kama hivi? Wanaume mliooa natamani nipate comment zenu pia kwa experience ya haya mambo.

Am still young in my late 20’s ambitious and the future is still so promising
Ukipata nafasi ya kunishauri ungenishauri nini?
Unaweza kuniita majina yote lakini ni maoni yako nitayapokea

PS: Huyu mume wa mtu sijatumia nguvu yoyote juu yake ni maamuzi yake ya hiari na akili zake timamu
Update
Japo nashambuliwa lakini nawashukuru mnaniongezea nguvu ya kufanya maamuzi although yanauma.Nyie nipeni ukweli tu ukweli ni dawa itakayo niponya
So far naona kuna dalili ya kumtumia huyu mume wa mtu since anataka mwenyewe why not,hii sio final ila kutokana na ushauri ninaona nipite namna hio
 
Pole kwa kujikuta njiapanda. Mwanangu nakushauri uolewe na huyo asiye na mke.

Kama wasemaji wasemavyo mke wa mtu sumu, hata mume wa mtu sumu pia. Kuna wanawake wamepata vilema kichaa na hata kufa kwa sababu ya waume za watu. Achane naye hata kama anakupenda vipi.

Usiipe nafsi yako kila inachokihitaji, itauponza mwili wako. iambie nafsi yako kuwa isukume damu na si vingine.

Samahani kama nitakuwa nimekukwaza.
 
Mimi mwenyewe nina mke ila kuna mdada natoka naye nampenda kinyama. Nina mpango wa kumuoa na yeye kakubali. So haya mambo yanatokea na huwezi kuyazuia kwa akili yako labda Mungu tu ndio azuie.

It feels better kujua kuna mtu ana pitia ninacho kipitia
Naomba nikuulize inamaana mkeo humpendi au ni nini kinatokea?
Utamuoaje bila wife kujua?
 
Pole kwa kujikuta njiapanda. Mwanangu nakushauri uolewe na huyo asiye na mke.

Kama wasemaji wasemavyo mke wa mtu sumu, hata mume wa mtu sumu pia. Kuna wanawake wamepata vilema kichaa na hata kufa kwa sababu ya waume za watu. Achane naye hata kama anakupenda vipi.

Usiipe nafsi yako kila inachokihitaji, itauponza mwili wako. iambie nafsi yako kuwa isukume damu na si vingine.

Samahani kama nitakuwa nimekukwaza.

Asante sana nimeupokea ushauri
 
Kwanini iwe ndoa ya siri? Kama anakupenda na anataka kukuwowa amjuze bi.mkubwa ili ajiandae kisaikolojia kuletewa bi.mdogo.

Yanini kubanana kwa mwanaume mmoja ilhali kuna kaka hapo yupo huru kabisa na nia kashatangaza?
 
"Meanwhile upande wa pili kuna kaka ambae hajaoa anataka kuja kutoa mahali,well paying job we have a connection lakini hajafika level za yule mume wa mtu"

Hapo naona umeamua kuangalia criteria ya POCHI,pochi ndio linakufanya umng'ang'anie huyo mume wa mtu.

Moyoni mwako hapo kuna kasauti kama nakasikia "mume wa mtu anajua kulea......".

Namuona single mother mtarajiwa akisha kuzalisha anarudi kwa mkewe,mnaanza kugombana kuhusu hela ya malezi ya mtoto.
 
It feels better kujua kuna mtu ana pitia ninacho kipitia
Naomba nikuulize inamaana mkeo humpendi au ni nini kinatokea?
Utamuoaje bila wife kujua?
Mke wangu nampenda mno na sipo tayari kumpoteza ila nimeshaamua liwalo na liwe. Yule mdada siwezi kumuacha aliwe na wahuni wengine maana jinsi ninavyomfeel siwezi hata kuelezea. Tukiwa chumbani huwa napata raha isiyokifani hivyo nimeshaamua bora nimuoe tu kuliko kumwacha akaolewa na mwanaume mwingine nikaishi a miserable life for the rest of life. Wife will have to just understand. I love her (my wife) but I'm also deeply in love with another woman.
 
Raha ya haya mambo ni kuwa ukikubali uoelewe kisirisiri na mume wa mtu na akamuacha mkewe bila taarifa, kuna siku atampenda mdada mwingine na ataanza kuishi nae na kumuoa kisirisiri na wewe akakuacha mkoa uliopo and the series will continue. Najua kuna imani zinaruhusu wake hadi wanne, ila hiyo ya kisirisiri ni issue kubwa hata kama imani yenu inaruhusu mitala

Kama huyo mume wa mtu ndie aliefungua mlango mara nyingine inakuwaga sio rahisi kumkatalia bila msaada wa Mungu, hivyo unahitaji kumuomba Mungu akuepushe na kikombe hicho.
 
Mke wangu nampenda mno na sipo tayari kumpoteza ila nimeshaamua liwalo na liwe. Yule mdada siwezi kumuacha aliwe na wahuni wengine maana jinsi ninavyomfeel siwezi hata kuelezea. Tukiwa chumbani huwa napata raha isiyokifani hivyo nimeshaamua bora nimuoe tu kuliko kumwacha akaolewa na mwanaume mwingine nikaishi a miserable life for the rest of life. Wife will have to just understand. I love her (my wife) but I'm also deeply in love with another woman.

Aisee unacho jibu hapa ni kama huyu jamaa,a very confusing situation to us christians nimeanza kuwaelewa waislam kwa hili
 
Nimeishia kusoma kwenye 'kufunga ndoa kisiri'...

Niseme tu wewe roho chafu ya kishetani inakutumia utenganishe ndoa ya watu... kaa mbali na huyo jamaa utampata wako

Mi nimeshamaliza labda Elitwege na Magonjwa Mtambuka waje kumalizia Bia yetu
Huyu Bia yetu mtoe hapo yeye anajua kulamba miguu ya Mzee Magufuli kumuita hapa kuja kutoa ushauri ni kama vile unamuonea.

Tukirudi kwenye mada huyo hana nia njema na wewe muepuke na fanya kila mbinu umukwepe wanaume sisi tunajitambua ni ngumu kwa mwanamme mwenye familia tena yenye watoto akimbie familia yake aje kwako wewe mwanamke ambaye bado unahangaika na maisha.

Ukilazimisha kujisogeza sana kwake ataishia kukutumia kama chombo cha starehe kutimiza haja zake akiwa anakuja huko ulipo, na nimeona hapo una mpenzi tayari kwanini usi focus kwake na nyie mkaja kufunga ndoa mkawa na maisha yenu mazuri kama familia.
 
Kama mume wa mtu dini yake inaruhusu kuongeza mke basi olewa nae maana inaonesha anakupenda bt kama dini yake hairuhusu acha na uolewe na huyo mwingine.
 
"Meanwhile upande wa pili kuna kaka ambae hajaoa anataka kuja kutoa mahali,well paying job we have a connection lakini hajafika level za yule mume wa mtu"

Hapo naona umeamua kuangalia criteria ya POCHI,pochi ndio linakufanya umng'ang'anie huyo mume wa mtu.

Inawezekana ndio au hapana nimeshindwa kuifafanua situation hii vizuri
Lakini naomba tu nikwambie nipo wakati mgumu
Umeshawahi kupenda watu wawili kwa wakati mmoja?
 
Aisee unacho jibu hapa ni kama huyu jamaa,a very confusing situation to us christians nimeanza kuwaelewa waislam kwa hili
Mimi mwenyewe mkiristo ila ndio hivyo nafsi yangu ndio imefikia maamuzi ya kuoa mke wa pili. Nimemwambia tutafunga ndoa hata kwa kujificha, kama ndoa haitawezekana basi tuishi bila ndoa. Cheti cha ndoa ni makaratasi tu wala hayachangii chochote kwenye kupendana.
 
Back
Top Bottom