Ananipenda lakini simuhitaji

Ananipenda lakini simuhitaji

Kimatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2017
Posts
286
Reaction score
272
HERI Ya sikukuu kwenu wote ni matumaini yangu kwamba wote kwa wingi wenu mmesherehekea na mnaendelea kusheherekea sikukuu kwa Furaha na amani tele, bila kupoteza muda ni vyema nikaweka mada iliyopo mezani.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26 ninaishi katika jiji la Arusha nikiwa sio tu mkazi bali hata mzaliwa wa jiji hili linalosifika haswa kwa utalii likiwa linesheheni vivutio mbalimbali.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na binti mmoja kutoka kwenye familia ambayo hela kwao sio kitu cha kujiuliza mara mbilimbili nikimaanisha kwamba zimefurika, binti huyo ametokea kunipenda hadi aibu, Amekua akituma marafiki zake waniletee mazawadi kedekede, na hata amefanya uchunguzi kubaini marafiki zangu ambao nao wamekua wakifaidika kutoka kwa binti huyo kisa mimi, kwani kwa zaidi ya miaka miwili sasa amekua akinitaka kama mchumba wake na zaidi kama mume wake wa baadae.

Tumekua tukiwasiliana kwa kipindi cha karibu miezi 3 na ameonesha nia ya kunipenda kwa dhati lakini mimi wala nimejitahidi lakini hazipandi asa ndugu zanguni mnanishauri nimpotezee au nimgande kwenu wakubwa.
 
Usichezee bahati kama hizo mkuu. Mm nilipata kama.hiyo almanusura nioe kabisa. Wazaz wake wakaingilia kati na kukataa.. mambo yakaishia hapo
HERI Ya sikukuu kwenu wote ni matumaini yangu kwamba wote kwa wingi wenu mmesherehekea na mnaendelea kusheherekea sikukuu kwa Furaha na amani tele, bila kupoteza muda ni vyema nikaweka mada iliyopo mezani.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26 ninaishi katika jiji la Arusha nikiwa sio tu mkazi bali hata mzaliwa wa jiji hili linalosifika haswa kwa utalii likiwa linesheheni vivutio mbalimbali.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na binti mmoja kutoka kwenye familia ambayo hela kwao sio kitu cha kujiuliza mara mbilimbili nikimaanisha kwamba zimefurika, binti huyo ametokea kunipenda hadi aibu, Amekua akituma marafiki zake waniletee mazawadi kedekede, na hata amefanya uchunguzi kubaini marafiki zangu ambao nao wamekua wakifaidika kutoka kwa binti huyo kisa mimi, kwani kwa zaidi ya miaka miwili sasa amekua akinitaka kama mchumba wake na zaidi kama mume wake wa baadae.
Tumekua tukiwasiliana kwa kipindi cha karibu miezi 3 na ameonesha nia ya kunipenda kwa dhati lakini mimi wala nimejitahidi lakini hazipandi....... Asa ndugu zanguni mnanishauri nimpotezee au nimgande kwenu wakubwa.
 
endelea tu kuchezea fursa..

sometime kama una uhakika mtu akupenda we jitose mazima mengine yatajulikana mbele ya safari.
hasara roho tu moyo sio kesi
 
Wenye mapenzi ya dhati tutakwambia umweleze ukweli binti wa watu, na usimchezee.

Walio fursa-oriented (after money) watakushauri vingine. Anyway, Mungu amsaidie huyo binti wa watu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom