HERI Ya sikukuu kwenu wote ni matumaini yangu kwamba wote kwa wingi wenu mmesherehekea na mnaendelea kusheherekea sikukuu kwa Furaha na amani tele, bila kupoteza muda ni vyema nikaweka mada iliyopo mezani.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26 ninaishi katika jiji la Arusha nikiwa sio tu mkazi bali hata mzaliwa wa jiji hili linalosifika haswa kwa utalii likiwa linesheheni vivutio mbalimbali.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na binti mmoja kutoka kwenye familia ambayo hela kwao sio kitu cha kujiuliza mara mbilimbili nikimaanisha kwamba zimefurika, binti huyo ametokea kunipenda hadi aibu, Amekua akituma marafiki zake waniletee mazawadi kedekede, na hata amefanya uchunguzi kubaini marafiki zangu ambao nao wamekua wakifaidika kutoka kwa binti huyo kisa mimi, kwani kwa zaidi ya miaka miwili sasa amekua akinitaka kama mchumba wake na zaidi kama mume wake wa baadae.
Tumekua tukiwasiliana kwa kipindi cha karibu miezi 3 na ameonesha nia ya kunipenda kwa dhati lakini mimi wala nimejitahidi lakini hazipandi asa ndugu zanguni mnanishauri nimpotezee au nimgande kwenu wakubwa.