Tajirimsomi
JF-Expert Member
- Jan 12, 2017
- 4,824
- 5,580
Habari za mida ndugu zangu wakubwa shikamooni. Kijana nakuja kwenu nahitaji msaada wenu wa kimawazo.
Kuna mama mmoja tumejuana kupitia mambo ya kanisa ambaye niliunganishwa naye kutoka kwa rafiki yangu baada ya yule mama computer yake kuwa na hitilafu akawa anahitaji mtaalamu baada ya kuhangaika nayo sana ndo akanipata mimi kupitia rafiki yangu Mungu alisaidia tatizo nikalitatua halikuwa kubwa sana sema mafundi wakishindwa kutambua tatizo ni nini.
Baada ya hapo mama akatokea kunizoea nami nikamzoea pia tukaishi kwa kuheshimiana kama mama na mwanae nashauri mambo mengi ya kiutaalamu pia ananishauri mambo mengi ya kimaisha nafurahia uhusiano wetu.
Uyo mama ana watoto wanne wa kiume mmoja na mabinti watatu. Kuna binti yake wa tatu kamaliza diploma mambo ya kilimo mlokole sana kwa kweli mzuri msitaarabu sana mama yake ananilazimisha nimtongoze awe mpenzi wangu anadai anatamani sana niwe mkwe wake na anadai binti yake ananifaa na kweli ananifaa yapata wiki ya tatu ananiambia ayo maneno nashindwa nifanyeje ntaanza vipi na nini kitakuwa hatima ya uhusiano wangu na uyo mama.
Naombeni ushauri wana JF sijui nifanye nini?