Ananiambia nijipange kwao Mahari huwa ni kubwa. Nimempa assignment

Hebu tupia hata kapicha kake mkuu wengine tuna mawe si kitoto hadi tunatamani kujiteka tunaweza kutoa hata mahali ya mil10 kama analipa
 
Mambo ya mahari yanazungumzika.
Nenda wewe na mshenga wako akazungumze na wakwe zako.
Halafu mahari hailipwi yote mtakapokubaliana.
Halafu hiyo 6M sio pesa ya kutisha kijana,kaza mattyakko duniani hakuna kitu cha bure au rahisi kikawa na ubora.

Otherwise jiunge na CHAPUTA kule hakuna mahari ni sabuni/lotion yako tu mambo Murua.
 
usivute tena Bangi ukiwa unataka kuongea na demu wako...
 
Kubali kataa mkuu vipo vitu kwenye jamii hatuwezi kuviondoa kwa Sasa labda uishi miaka 100,000.

Usipolipa mahari ujue huyo sio mkeo na hao sio watoto wako.
Heshima kama Mwanaume,Mume kwenye hiyo jamii ya mkeo utakuwa huna.

Watoto ni kwako, serikari na Mungu ukisema si wa yeyote kwanini wewe unajitambulisha kama mtu wa Same?

Lipeni mahari hacheni hizi ngokowa,
nani aliyekwambia Wazungu hawalipi mahari?
 
Oa familia ambayo mnalingana vipato
 
Mhh mbona kama una chuki nae
 
Achana nao hao mkuu, njoo nikupe dada yangu bure kabisa hata zawadi hatutaki maana anakunywa gongo, anakula ugoro, kuberi, anavuta bange, shisha na tumbaku ambayo haija chakatwa na anawatoto wanne mkuu tunakupatia wote bureee....😊
 
Ofcourse suala la mahari lina thamani sana kwa binti aliejutunza la sivyo hapaswi kupewa heshima ya kutolewa mahari.

Ubarikiwe upate mabinti na wewe...
 
Mahari anataja baba kwani anaolewa yeye? Mfyuuuuu,

Naenda kugalagazwa mie halafu mahari wale wengine,
Mahari Inategemea sana na tamaduni/uelewa wa baba upande wa binti, kwa mfano kuna jamii moja ya kanda ya kati hapa Tz kuku kadhaa tu ni mahari tosha unaoa! then kuna ukanda mwingine ni ng'ombe kadhaa nakama bint mweupe mahari inapanda maradufu, yet kuna jamii nyingine mahari anataja bint, nakubuka kuna mkubwa mmoja wa jeshi la polisi mahari alisema bint na alisema anataka msahafu wa dini yao tu hana jengine. Na kwa mfano baadhi ya jamii ya kikomoro aisee wana mahari kubwa na wao wako happy kuzitoa.

Kwa ufupi mara nyingi mahari hutemea upande wa muolewa wanasemaje (mara nyingi baba) na anayeoa aseme anataka mahari iwe kama anavyotaka yeye. Ingawa hizi pande mbili zinaweza kukaa zikanegotiate
 

Jamii Gani?
Jamii isiyo na Mila na desturi haina kitu kinaitwa Mahari.
Mila na desturi zipo kikabila Huko.
Ikiwa zingine mliziita Mila potofu hata zilizopo baadhi zinaweza kuitwa Mila potofu ikiwemo Hiyo ya kutoa Mahari.

Alafu kwenye jamii isiyo na mila na desturi heshima msingi wake hautokani na Maoni ya Watu wengine Bali inatokana na mtazamo WA MTU mwenyewe. Huko ndio tulikofikia.
Labda Huko vijijini.
Lakini mijini sehemu yenye mchanganyiko mkubwa wa Watu Watu wengi wameoa na kuolewa pasipo hayo makitu ya Mahari sijui vitu gani vya kimila na desturi.

Hayo mambo ya kimila yapo Huko vijijini. Mjini na sehemu yenye mchanganyiko wa Watu Watu wanaangalia Maisha Yao. Huo muda wa kujua Fulani alitoa Mahari au hakutoa Watu Hawana.
 
Kaa na binti wa watu, nyumbani kwao hawakutambui / hawakujui halafu bahati mbaya paaa kafa magetoni kwako hapo hapo uone namna tumbo la kuhara linavyoweza kukubana.

Kuvimbiana ova kifutu hakukusaidii sana. Nenda ukweni kiungwana watakalokwambia una nafasi ya kujielezea kama mume mtarajiwa, mkishimdwana sio kesi kwamba unaenda kufungwa mahakamani.

Halafu hawa watoto wa kike ukiwa unamvimbia sana kila wakati ni sawa na kumuonea tu. Lazima ujue kuishi naye kwa akili vinginevyo unaachana nae mapema ili ajue anashika njia gani
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…