Analazimisha nimuoe wakati mimi sitaki

High Vampire

JF-Expert Member
Nov 17, 2012
2,546
1,453
jamani naombeni ushauri nina dada ambaye nilikuwa na uhusiano naye , mbaya zaidi ameanza kujitambulisha kwa wazazi wangu kuwa mimi nimeshamuoa na ananifuata hadi ofisini akisema amewambia wazazi wangu kuwa tunafunga harusi mwaka ujao na baba yake ni mganga wa kienyeji nifanyaje ili nisipatwe na hili tatizo kuoa bila malengo
 
Joyceline

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
1,010
147
Mweleze ukweli kwamba hutaki kumuoa , unasema mlikuwa na uhusiano that means mlishaachana sasa anataka nini tena, kuwa na msimamo wewe ni mwanaume
 
Mzalendo wa ukweli

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
559
148
jamani naombeni ushauri nina dada ambaye nilikuwa na uhusiano naye , mbaya zaidi ameanza kujitambulisha kwa wazazi wangu kuwa mimi nimeshamuoa na ananifuata hadi ofisini akisema amewambia wazazi wangu kuwa tunafunga harusi mwaka ujao na baba yake ni mganga wa kienyeji nifanyaje ili nisipatwe na hili tatizo kuoa bila malengoKama hutaki kumuoa unadhani sisi tutakushauri kitu gani wakati umeshaamua mwenyewe? Muoe basi
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,146
9,464
1. Yeye ndo kawaambia wazazi wako........
2. Yeye ndo anakuja ofisini kwako......
3. Baba yake ni mganga wa kienyeji......

Wewe ndo muoaji na hujapeleka hata posa unaweweseka nini sasa.......je kama ungekuwa unaolewa wewe si ungewehuka........!!!!!!!

Are you real serious...................???????????????????????
 
Papizo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
4,906
1,338
Mtoto wa kiume saa zingine inabidi uwe na uwamuzi mgumu,sasa hapo ukiwa na family si itakuendesha sana,ndio wasichana wa sasa hivi walivyo wanapenda sana kuolewa wakishaona mtaani mwenzao kaolewa...so kuwa na msimamo wewe mwanaume na kuwa straight kwamba huwezi kumuowa au muda wako bado

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,801
24,510
pole mwaya. na wewe kajitambulishe wa mganga wa kienyeji aka baba mkwe, na umuambie humuoi mwanae. uone kama hujageuzwa christmas turkey:madgrin:
 
Osaka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
1,762
550
jamani naombeni ushauri nina dada ambaye nilikuwa na uhusiano naye , mbaya zaidi ameanza kujitambulisha kwa wazazi wangu kuwa mimi nimeshamuoa na ananifuata hadi ofisini akisema amewambia wazazi wangu kuwa tunafunga harusi mwaka ujao na baba yake ni mganga wa kienyeji nifanyaje ili nisipatwe na hili tatizo kuoa bila malengo

Kwani kuna shida gani baba yake akiwa Mganga wa kienyeji? Chukua hatua dogo, huyo hakufai, piga chini.
 
mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
21,202
28,030
jamani naombeni ushauri nina dada ambaye nilikuwa na uhusiano naye , mbaya zaidi ameanza kujitambulisha kwa wazazi wangu kuwa mimi nimeshamuoa na ananifuata hadi ofisini akisema amewambia wazazi wangu kuwa tunafunga harusi mwaka ujao na baba yake ni mganga wa kienyeji nifanyaje ili nisipatwe na hili tatizo kuoa bila malengo

duh!!! kwanza umedumu nae muda gani?
 
fazaa

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,985
1,007
Sa unacho ogopa nini mwanaume unaogopa mwanamke si aibu.

Kama ulikuwa humtaki vipi ukawa na uhusiano naye.

I c kumbe baba yake mganga, sa ndo ulie tu...utajiukuta unaowa utake ustake, na ushike adabu ya kumwadanganya ma bint wa watu kama unawapenda wakati huwapendi.
 
High Vampire

JF-Expert Member
Nov 17, 2012
2,546
1,453
nmeshamwambia sana ila jana kanitumia sms inasema sunajua baba mganga na mimi nkamwambia lolote ufanye namwachia mungu hiyo sms ndio inanichanganya
 
mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
21,202
28,030

kha!!! imekula kwako hiyo mwana....sasa kweli kumuoa hawezi kukulazimisha ila cha moto utakipata. ata hakikisha kuwa life lako la mapenzi analivuruga vibaya na hivi baba mganga wakienyeji...unaweza shangaa ukienda kwa demu mwengine kitu hakidindi hahaha
 
Fixed Point

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
11,304
12,736
pole mwaya. na wewe kajitambulishe wa mganga wa kienyeji aka baba mkwe, na umuambie humuoi mwanae. uone kama hujageuzwa christmas turkey:madgrin:
shosti hapa umenifanya nionekane mwehu, lol!
Christmas turkey siyo?
 
lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,710
29,049
Dogo HAMA NCHI manake uchawi hauvuki bahari!!!!!!! Bila hivo utake usitake utamuoa! Either umuoe hivi kama binadamu au kama Msukule!

Mi kabla sijatoka na mtu namuuliza baba yako nani nchini humu? Watu wananiona fisadi! Haya sasa umemtukana mamba kabla hujavuka mto! KAJIUNGE NA UPADRI/UCHUNGAJI Baaaaaaaaaass!
 
Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,601
1,677
jamani naombeni ushauri nina dada ambaye nilikuwa na uhusiano naye , mbaya zaidi ameanza kujitambulisha kwa wazazi wangu kuwa mimi nimeshamuoa na ananifuata hadi ofisini akisema amewambia wazazi wangu kuwa tunafunga harusi mwaka ujao na baba yake ni mganga wa kienyeji nifanyaje ili nisipatwe na hili tatizo kuoa bila malengo
Kwa kuwa baba yake ni mganga wa kienyeji ndicho kinachokutisha..............................!
Unahofia kuondokewa na uume au nguvu za kiume........?
Kama ni hivyo limekuganda na ujue amejiandaa ndo maana yupo waruwaru kuitambulisha.......!:biggrin1::biggrin1:
 
prianka

JF-Expert Member
Aug 29, 2012
684
168
mwambie ukweli kama humtaki usikute hata dem mwenyewe hujamwambia kama hutaki kumuoa au ulimuhaidi tangia mwanzo ndo maana na yeye kafanya ivyo,na hilo litakua fundisho maana sasa mnataka kuonja 2 na kuangalia mkato wa chumba na madhari yake je kukavu au kuna unyevu unyevu alafu mnasepa kua makini na udanganyifu pengine kuchungu njombaaaaaaaaaaaaa
 
Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,941
5,541
kuwa mganga ndo unaogopa simama ktk imani utafanikiwa kama umeshaoa anatangaza ndoa atakuwa hana akili timamu mkataze kuingia ofisi kwako pia mwambie wife ukweli kabla hajagundua.
 
zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
250
jamani naombeni ushauri nina dada ambaye nilikuwa na uhusiano naye , mbaya zaidi ameanza kujitambulisha kwa wazazi wangu kuwa mimi nimeshamuoa na ananifuata hadi ofisini akisema amewambia wazazi wangu kuwa tunafunga harusi mwaka ujao na baba yake ni mganga wa kienyeji nifanyaje ili nisipatwe na hili tatizo kuoa bila malengo
vp unamwogopa kwa kuwa baba yake ni mganga wa kienyeji? vp huo uganga ameanza zamani toka ukiwa na uhusiano na mwanaye au ni siku za karibuni?
kama ni zamani ulikuwa unafahamu kabla hujamuaproach?
Mwombe Mungu atakusaidia hakuna analoshindwa Mungu atakutegulia kila mtego na huyo msichana ataondoka mwenyewe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom