Anaishi na mume mwizi, akidhani anafanya kazi bandarini

Mjini pakiwashinda si mrudi vijijini mnang'ang'ania darisalade na mishe hazisomeki
 
Habari za humu wakuu,

Nmejiunga JF nina muda kidogo ila ni mpenzi msomaji tu sijawahi kutoa uzi leo nmeguswa niseme hili.

Bado kuna wanawake wanaolewa na mume ambaye hajui chanzo cha uchumi wake au hana uhakika na kazi aliyotajiwa.

Mimi nmeshuhudia hili, kuna sehemu nimepanga hapa Dar, Tupo wapangaji watatu na kila mmoja mlango wake hivyo sio rahisi sana kukutana mara kwa mara. Kila mmoja anatoka asubuhi na kurudi jioni katika mishe zake.

Japo aliyenifanya nitoe uzi yeye ni mke wa mwizi, yeye huwa yupo nyumbani mara nyingi na anajua mme wake anafanya kazi bandarini(Kwa mdomo wake akitamka).

Zimepita wiki kama mbili hivi, mume wake alikuja maeneo ya kariakoo. Mimi Siku hiyo nilikuwa nina mteja anataka nimuelekeze fundi mzuri wa simu, nikampeleka kwa ninaowajua.

Nilipofika nikamkuta jirani yangu hapo kwa fundi pia, hakunisalimia vizuri japo mimi nikajichekesha kuwaambia mafundi kama kuwa tunaishi wote home. Ghafla akaondoka(nikajua labda kavurugwa simu imeroga) basi ikaishia hapo.

Siku zikaenda, mmoja wa wale mafundi akapita dukani. Katika story akasema jirani yako alikuja kakuulizia. Nikapatwa kiu ya kuuliza anakujaga kufanya nini(maana mimi nlikuwa nmemuona tena mara mbili)nikazugwa ila nikaambiwa ni mwendo kasi(wezi wa simu huko katika daladala, anaingia vyuoni, na anakuja kuuza kariakoo, karibu kila baada ya siku 3 analeta simu.)

Nikauliza nasikia anafanya kazi bandarini, nikaambiwa anadanganya hivyo. Aisee nliishiwa nguvu, jamaa bitozi mnoo, smart, anavaa vitu vya thamani na bei mbaya kumbe kibaka.

Wanandoa ya msikitini na Mke akijua mumewe yupo bandarini (ni asilimia 99% mke hajui jamaa kibaka). Namuonea huruma maana siku ataitwa kuja kuchukua maiti (wamempiga kafumwa) au atamkuta polisi. Ila Mungu ipo siku ataweka hadharani ili yule mtoto na Mjane wasije achwa mazingira ya ajabu.

NB: Wakaka smart ndio wengi huleta simu kuuza za kuiba dada zangu. Wananukia hao na raba zao kama Baba Tiffa. Chunguzeni msiingie tu kisa wanapesa za harakaharaka. Na huwa ndio wala bata sana maana hazina jasho na wanajua kesho zipo.

Komaeni na hao hao mnaojua wanaishu gani japo pesa za kuunga unga.
Kama kila siku anaacha hela ya kubadilisha mboga sio mbaya.
 
acha tu kuwe na changamoto, hii ni dunia lazima kuwe na mchannyiko wa utafutaji siku akikamatwa ndio imetimia hiyo"Maisha yana madhara mkuu
 
Mkaushie kama wewe hajakudhuru mwache na mishe zake na wewe kimpango wako,haya mambo ya kuchunguzana ndiyo mwanzo wa uchawi.
 
Aisee hii post imenikumbusha kisa kimoja cha mwaka 2008 hivi kwenye zile kesi za EPA. Kuna dada mmoja very innocent alikutana na jamaa kwenye haya makanisa ya walokole. Yule jamaa alimpenda dada huyo na kumwambia kuwa ameokoka miaka mingi na ni mfanyabiashara ya madini. Na akampeleka ofisi moja ya mhindi akamwambia ndiyo boss wake. Akaweka wazi kuwa anataka amuoe huyo dada. Wakaoana 2005. Cha kushangaza dada akawa wanaona simu za mumewe haziwekwi chini na alikuwa nazo nyingi na line za simu nyingi. Yaani simu anaingia nazo bafuni kuoga anaweka kwenye bukta. Pia wakawa anaona anauza vitu used kama simu, saa, laptop n.k. Yule dada akawa anajiuliza maswali bila majibu. Hapo tayari ana mtoto mmoja. Kwa kuwa dada ni mtu wa kusali sana basi inaelekea alishirikisha na wachungaji. Basi ikaja kugundulikakuwa mume ni:
1. Mnunuzi wa bidhaa za wizi na kuziuza
2. Ni mzinzi I aliyekubuhu - alithibitisha wanawake zaidi ya 10 kama side chicks.
3. Alikuwa ni mastermind wa draft la wizi wa zile pesa za EPA ambapo hata yule aliyemtambulisha kuwa ni boss mahindi naye alikuwa mwizi wa EPA na alikuwa na kesi pia.
4. Na mengine mengi tu ikiwemo kumuibia vitu vya thamani kama dhahabu, vito n.k

Jamaa alikamatwa kwa kesi ya EPA na akakaa mahabusu muda mrefu mpaka yule dada alivyofanikisha kumtoa na alitumia pesa nyingi sana mpaka mkopo ili mume atoke.

Alipotoka mianya ya misheni town ikawa haipo. Pesa ikamwishia na hatima ya akamgeukia mke ndiyo akamuibia vitu nilivyotaja. Hivyo mwizi haachi asili anaweza hata kujiibia mfukoni.

Yule dada alipata stress kubwa mno ila Ushauri hasa ya na maombi ndiyo vilimsaidia. Yaani Karibu angekuwa chizi.

Kwa sasa dada huyo anaendelea vizuri kama single mother akipata bado Ushauri nasaha ili aweze kusahau pia kupona maana alipata health issues zitokanazo na stress ila anazidi kuimarika siku hadi siku. Dada ni mpambanaji mzuri mno na kwa sasa yuko mbali sana kimaendeleo baada ya kuachana na mwizi.

Kifupi mwizi ni mtu anayerudisha mtu nyuma mno kimaendeleo.
Ila wanaume wanajua kulostisha wanawake in the name of love

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Ulaghai unafanywa katika mazingira kama mazingaombwe, unakuja stuka asubuhi
 
Na kweli mkuu sinaga habari ya kufatilia maisha ya mtu, kila mtu atavuna alichopanda.

Mtoto wa dingi angu mdogo alikuwa mdokozi,ni dogo kwangu tukiwa kwa bibi kule Tukuyu kikiibwa kitu alikuwa anakana katakata, hivyo tabia ya wizi akaizoea, sasa tumekuwa watu wazima mwaka jana kama mwezi wa tatu kaiba ng'ombe wa watu kapigwa miaka kumi jela. Dingi akasema sijui mdogo wako huku sijui kafanyaje tumsaidie nikaziba masikio,Sitaki hata kujua habari zake...he is now serving ten years in jail
Sifa mojawapo ya mtu mwizi ni uwezo mkubwa wa kukataa Tena kwa viapo
 
Tatizo mnapenda sana hela,sasa ndio unakutana na mtu anakupenda alafu hana hela lazima afake akupate tu.
 
Ulaghai unafanywa katika mazingira kama mazingaombwe, unakuja stuka asubuhi
Kabisa mkuu. Kuna watu wako smart sana katika kuficha maovu yao. Halafu crew ya wezi wa EPA wengi au kama wote walikuwa wanajifanya walokole na wazee wa kanisa. Aibu tupu
 
Back
Top Bottom