Anaishi na mume mwizi, akidhani anafanya kazi bandarini

kidawisee

Senior Member
Feb 27, 2020
143
212
Habari za humu wakuu,

Nmejiunga JF nina muda kidogo ila ni mpenzi msomaji tu sijawahi kutoa uzi leo nmeguswa niseme hili.

Bado kuna wanawake wanaolewa na mume ambaye hajui chanzo cha uchumi wake au hana uhakika na kazi aliyotajiwa.

Mimi nmeshuhudia hili, kuna sehemu nimepanga hapa Dar, Tupo wapangaji watatu na kila mmoja mlango wake hivyo sio rahisi sana kukutana mara kwa mara. Kila mmoja anatoka asubuhi na kurudi jioni katika mishe zake.

Japo aliyenifanya nitoe uzi yeye ni mke wa mwizi, yeye huwa yupo nyumbani mara nyingi na anajua mme wake anafanya kazi bandarini(Kwa mdomo wake akitamka).

Zimepita wiki kama mbili hivi, mume wake alikuja maeneo ya kariakoo. Mimi Siku hiyo nilikuwa nina mteja anataka nimuelekeze fundi mzuri wa simu, nikampeleka kwa ninaowajua.

Nilipofika nikamkuta jirani yangu hapo kwa fundi pia, hakunisalimia vizuri japo mimi nikajichekesha kuwaambia mafundi kama kuwa tunaishi wote home. Ghafla akaondoka(nikajua labda kavurugwa simu imeroga) basi ikaishia hapo.

Siku zikaenda, mmoja wa wale mafundi akapita dukani. Katika story akasema jirani yako alikuja kakuulizia. Nikapatwa kiu ya kuuliza anakujaga kufanya nini(maana mimi nlikuwa nmemuona tena mara mbili)nikazugwa ila nikaambiwa ni mwendo kasi(wezi wa simu huko katika daladala, anaingia vyuoni, na anakuja kuuza kariakoo, karibu kila baada ya siku 3 analeta simu.)

Nikauliza nasikia anafanya kazi bandarini, nikaambiwa anadanganya hivyo. Aisee nliishiwa nguvu, jamaa bitozi mnoo, smart, anavaa vitu vya thamani na bei mbaya kumbe kibaka.

Wanandoa ya msikitini na Mke akijua mumewe yupo bandarini (ni asilimia 99% mke hajui jamaa kibaka). Namuonea huruma maana siku ataitwa kuja kuchukua maiti (wamempiga kafumwa) au atamkuta polisi. Ila Mungu ipo siku ataweka hadharani ili yule mtoto na Mjane wasije achwa mazingira ya ajabu.

NB: Wakaka smart ndio wengi huleta simu kuuza za kuiba dada zangu. Wananukia hao na raba zao kama Baba Tiffa. Chunguzeni msiingie tu kisa wanapesa za harakaharaka. Na huwa ndio wala bata sana maana hazina jasho na wanajua kesho zipo.

Komaeni na hao hao mnaojua wanaishu gani japo pesa za kuunga unga.
 
Anamaanisha wamefunga ndoa msikitini maybe

QUOTE="establishment, post: 38057514, member: 297344"]
Umesema wana ndoa ya Msikitini?
[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom