Anahitajika Mwanafunzi anayesomea Agriculture General

Anahitajika Mwanafunzi anayesomea Agriculture General

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
6,658
Reaction score
3,665
Salaamu.

Nahitaji mwanafunzi wa mwaka wa pili SUA anayeingia mwaka wa tatu aliyesomea Agriculture General na anajua vizuri masuala ya kilimo cha kisasa.

Namhitaji kwa ajili ya ushauri kwenye mradi wangu wa kilimo. Nitamgharamia kusafiri kwenda Tabora kwenye huo mradi kwa ajili ya ushauri na tathmini kisha akimaliza atarudi kuendelea na masomo yake.

Kumbuka kutakuwa na interview ya kumpima kama atakidhi ujuzi ninaotaka awe nao. Walio tayari waje inbox na huku watapatiwa mawasiliano na namna ya kutekeleza hilo na interview.

Asanteni na karibuni.
 
Kwahy hawaitajiki??ila kama utaitaji wa waliomaliza wapo....ukimwambia ukweli atakuelewa tu
 
Kwahy hawaitajiki??ila kama utaitaji wa waliomaliza wapo....ukimwambia ukweli atakuelewa tu
Nahitaji mtu akanifanyie kazi isiyozidi mwezi mmoja. Namlipa. Nahitaji mwananfunzi maana nitamuhitaji tena akifunga chuo...
 
Sasa mkuu,sasa hivi Vyuo ndo vinaelekea kufunguliwa,bado wiki moja na kidogo tu,kwa hiyo kufanya hiyo kazi kwa mwezi mmoja itakuwa ngumu,Ushauri wangu mtafute aliyemaliza tayari umweleze kuwa hiyo siyo ajira,akufanyie kwa muda ulioupanga tu.
 
Hyo Interview kwiooooooh, kama una Interview panel wanaojua mambo ya kilimo kiasi kwamba wana uwezo wa kumuuliza mwanafunzi maswali si uwachukuwe haohao.. Acha kutufanya dhariri kiasi hichi bhana
 
Back
Top Bottom