Anahitajika mfanyakazi wa kazi za nyumbani

Mesut90

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
537
626
Anahitajika msichana wa kazi kutoka sehemu yoyote ndani ya Tanzania.

SIFA: umri kati ya miaka 18- 25
Mshahara: 70,000 (elimu ya darasa la saba kushuka chini) au 100,000 (elimu ya o'level)
Eneo la kazi: Tanga mjini

Awe tayari kuhama mkoa ikiwa muajiri atahamia mkoa mwengine.

Malazi na chakula na matibabu madogo ni juu ya muajiri.

Ahsanteni na karibuni PM kwa mwenye uhitaji
 
Matibabu madogi na makubwa unayatofautishaje?
Mkuu naamini umeelewa.

Haya maswali mengi ili yasaidie nini??? Kwahiyo unategemea mfanyakazi huyo apate tatizo la kufeli figo halafu mimi ndio niingie gharama za kumpeleka India kwa matibabu??

Kuna mtu mmoja aliwahi sema, kuweni makini na watu wnaaouliza maswali wengine lengo Lao sio kujifunza Bali ni kuharibu tu.

Watu wa namna hiyo wapo wengi sana. Hata darasani tulikuwa na watu wanaomuuliza mwalimu maswali ili ayashindwe adhalilike tu.

Uwe na jioni njema mkuu
 
Ningeelewa ningeuliza maswali kweli?
Kwanza nimefarijika na kuona mwajiri anajali mfanyakazi Kwa matibabu hata kama ni hatua ya awali. Haujui Kuna wenzako hapa akimpa chakula na malazi mfanyakazi anaona kama anatoa ziada?

Kumbuka kwenye huu Uzi wengi wanapita. Itasaidia wengi. Mfano kwangu akiugua vipimo atafanyiwa na dawa ntanunua. Bora ungesema magonjwa ya kawaida. Ambayo kimsingi kwetu yanaangukia malaria, homa n.k.

Sijajua ugumu au ubaya wa swali langu umetokea wapi lakini kama limekua kero niwie radhi.

Cha mwisho, jikite kwenye ufanisi achana na mambo ya vigezo vya mfanyakazi Kwa hii tasnia.

Jioni njema pia
 
Sawa mkuu. Shukran sana!
 
Jamani naombeni msaada..Mwenye email ya EUROPEAN UNION TZ.
Msaada

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Mkuu hili lilikuwa ni suala la ku-Google tu.

Screenshot_20220322-100013_Chrome.jpg
 
Wameadimika sana, wengi wanaidharau hii kazi
Sio kuadimika tu, wengi wameelimika na wanauelewa,bint akishafika kidato cha nne,upeo unakuwa umefunguka ni rahisi kujiendeleza kwa certificate ya taaluma yoyote....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom