Anadai nikacheki damu kama haina tatizo

Anadai nikacheki damu kama haina tatizo

Joined
Oct 5, 2015
Posts
60
Reaction score
3
Habari wanajf,jaman naombeni ushauri kuhusu hili maana mpaka sasa sijaelewa anamaanisha nini..mmi nina mpenzi wangu ambaye huu sasa ni mwaka wa tatu nipo nae sasa hivi juzi kati wakat tupo chatting tu kama kawaida akanambia kuna kitu kasau kunambia nilipomuliza kitu gani akanambia niende nikacheki mkojo na damu,nilipomuuliza kwanini akanambia yeye alikutwa na uti kidogo hivo na mie niende,nikamuliza asa kama ni uti mbona ananambia nikacheki na damu akanambia nikacheki damu kama haina tatizo lolote kumuuliza kwanini kakazania kua nikacheki damu akanijibu check for advance..yani kanichanganya apa nina mawenge balaa hta kwenda kupima naogopa,jamani naomben ushauri wenu hivi atakua ana maana gani kunikazania nikacheki damu!
 
Pole dada kwa hilo,jiandae kisaikolojia kukabiliana na lolote lile mpenzi wako anamaanisha,najua inauma lakini no way out
 
Huyo kashapima amekutwa ana ngoma, sasa anatafuta jinsi ya kukufikishia taarifa ndiyo maana anakuambia hivyo, tayari yeye ameathirika.

NB: Piga moyo konde ukapime, haina maana eti kama mpenzi wako ameathirika basi na wewe umeathirika. Cha kukushauri zaidi mwombe akueleze ukweli, ikibidi ukipima ukakuta uko salama, nenda tena baada ya miezi mitatu (na katika kipindi chote hiki usifanye naye chochote labda uijue status yake kwanza).
 
huyo anaogopa kwenda kupima kwa hyo anatumia mgongo wako ukapme il na yeye apate matokeo na ina elekea amekusulati na kupga demu mwingne na anawasi wasi huyo demu amempa vidudu nenda kapme kwa usalama wa afya yko ila mwangalie huyo jamaa mara mbili mbili kuwa makini
 
huyo anaogopa kwenda kupima kwa hyo anatumia mgongo wako ukapme il na yeye apate matokeo na ina elekea amekusulati na kupga demu mwingne na anawasi wasi huyo demu amempa vidudu nenda kapme kwa usalama wa afya yko ila mwangalie huyo jamaa mara mbili mbili kuwa makini

Nashukuru kwa ushauri wako.,nitajitahidi nifanye hivyo.
 
Nenda kapime hapo hamna issue yeyote ile wala usiogope pima utapata uhakika hiyo tuu ni mikwara
 
Sa mtu ashakuambia hivo alaf unaogopa? unaogopa nin mshashiriki ngono mara kibao wew nenda kacheki ukikuta mzima shukuru mungu ila uanze pata tahadhari ukikuta mambo yameharibika anza dozi mapema kuja hapa kuomba ushauri ni jambo jema ila utapita kwenye wakati mgumu maradufu kuliko ungejibvika roho ya ujasiri na kwenda kupima direct.
 
Wewe kapime tu kwanza ujue afterall hata ikiwa vipi,afya ni yako
 
Jamaa alikusaliti toka muda mrefu sasa aliekusaliti nae hasemwi vizuri hivyo anataka ukapime ili apate majibu, nenda kapime kwanza kwa sababu naamini uko poa kabisa lakini jamaa yako pia apime baada ya hapo utachagua kusuka ama kunyoa maana amewasha taa nyekundu tayari kua makini kwani hakuna nayepata ukimwi akabaki na furaha yake ya awali
 
Kuna wakati nilikuwa kwenye mradi wa kuhamasisha upimaji wa hiari. Kauli mbiu yetu ilikuwa "Pima VVU leo, majibu ya mweza wako si majibu yako".

Katika jambo lolote ukiweza kuishinda Hofu utaweza kufanikiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom