Anachofanya Lissu ni uhaini

Anachofanya Lissu ni uhaini

Uhaini (kutoka neno la Kiarabu) ni pale mtu anapotenda jambo dhidi ya nchi yake. Kwa mfano, mtu anaweza kuisaidia nchi nyingine ipigane vita dhidi ya nchi yake kwa kutoa habari za siri.

Uhaini ni neno la kawaida, lakini nchi tofauti zina sheria na adhabu tofauti dhidi ya matendo ya kihaini, hata adhabu ya kifo.

Miongoni mwa wahaini maarufu duniani kuna Yuda Iskarioti, Benedict Arnold, Philippe Pétain na Vidkun Quisling.

Kwa Hisani ya Wikipedia.
Unajua tofauti ya nchi na serikali? Isome tena hiyo katiba inasemaje kuhusu nchi na inasemaje kuhusu katiba.then uje utuambie lissu amefanya nini kuhusu nchi na amefanya nini kuhusu serikal?
 
wabongo bwana shida kweli kweli ,walioapa kuilinda katiba hawailindi ila wale wafia tumbo waliopewa tu vyeo ndo wanatusumbua katiba katiba,je katiba hiyo haitambui kuwa nchi hii niya kidemocrosia inayofuata mfumo wa vyama vya siasa?sasa hiki kinachoitwa usaliti wa Lissu kinatoka wapi?je katiba inasemaje kuhusu jukumu la serikali kwa raia wake na imefanya nini kwenye swala la lissu? Hivi mkishapewa hivyo vyeo basi mnakuwa mmekuwa pia juu ya kifo? Yaani kuna uwezo fulani natamani kuwa nao kama Mungu angenipa huo uwezo hata saa moja kuna watu mngepata tabu sana
huu ndiyo UASI na UHAINI wa LISU VIDEO: Tundu Lissu ataka Rais Magufuli asusiwe kila mahali na mataifa mengine duniani - JamiiForums
 
Katika hiyo Mihimili yote tunaomba utuoneshe na uanishe hayo Matusi..

Binafsi nimesha shuhudia walio mtukana Raisi wakipandishwa Mahakamani lkn katika Makosa yao sijawahi kuona kumtukana Raisi kukawa ni Uhaini.

Sheria ya Uhaini. Na.2 ya 1970 Jedwali
SURA YA SABA

UHAINI NA MAKOSA MENGINE DHIDI YA SERIKALI
39.-(1) Mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano
(a) akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, anamuua au anajaribu kumuua Rais; au
(b) akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano anaanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano,
atakuwa na hatia ya kosa la uhaini na atawajibika kwa adhabu ya kifo.

(2) Mtu yeyote ambaye, yumo katika ndani ya Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, anajenga nia kusababisha au kuwezesha kusababishwa, au anajenga nia ya kuchochea, anashawishi, shauri au kuusia mtu yeyote au kikundi cha watu kusababisha au kuwezesha kusababishwa yoyote kati ya matendo au malengo
yafuatayo, yaani:-

(a) kifo, kumlemaza au kumjeruhi, au kufungwa au kumzuia,
Rais;

(b) kumwondoa Rais madarakani isivyo halali kutoka katika
wadhifa wake wa Urais au kumwondolea ufahari, heshima na jina la Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;

(c) kupindua kwa njia zisizo halali, Serikali ya Jamhuri ya Muungano; au

(d) kutishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
na kubainisha nia hiyo kwa kuchapisha maandishi or machapisho au kwa kitendo chochote cha siri kinachojionyesha cha hali yoyote, atakuwa na hatia ya kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifo.

(3) Mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya Muungano–

(a) aliye na mshikamno na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au anawapa msaada au hifadhi ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko;

(b) anachochea, aidha ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko, mtu yeyote aivamie Jamhuri ya Muungano kwa kutumia jeshi; au

(c) anabeba silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa amri, kwa nia ya kutumia nguvu ya kuizuia, kuilazimisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano kubadilisha vigezo au ushawishi wake, au kwa nia ya kulazimisha au kuzuia au kutishia, Serikali ya Jamhuri ya Muungano,

waulize wakandarasi waliozuia ndege nani alikuwa anasaidia kutrace asset. Hayo ndiyo makavu

Mkuu hili hauna nalo Ushahidi ,pia Suala la Ndege kukamatwa sio jambo la Siri.Unadaiwa na Mabeberu na wewe huyo huyo unaenda kuweka order ya kuundiwa Ndege kwa hao hao Mabeberu halafu unakuja hapa kulalamika ooh Mh Lissu katuchonjea!!..
 
Lete ushahidi wapi na lini Rais aliagiza Lisu apigwe Risasi.Acheni propaganda jino kwa jino

Aliyesababisha deni ni nani? na kule duniani hakuna siri za kichawi kama mnazofanya Lumumba
 
Ameuawa khashog sembuse huyo Mnyampaa aliyelia baada ya kushida kesi ya ubunge.Edward Snowden anasakwa kwa ULISU.
Sasa wewe unashangaa nini magufuli kususiwa,kwani serikali yake ndo itakuwa ya kwanza kususiwa hapa duniani? By the way hivi umewahi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania?
 
Sheria ya Uhaini. Na.2 ya 1970 Jedwali
SURA YA SABA

UHAINI NA MAKOSA MENGINE DHIDI YA SERIKALI
39.-(1) Mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano
(a) akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, anamuua au anajaribu kumuua Rais; au
(b) akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano anaanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano,
atakuwa na hatia ya kosa la uhaini na atawajibika kwa adhabu ya kifo.

(2) Mtu yeyote ambaye, yumo katika ndani ya Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, anajenga nia kusababisha au kuwezesha kusababishwa, au anajenga nia ya kuchochea, anashawishi, shauri au kuusia mtu yeyote au kikundi cha watu kusababisha au kuwezesha kusababishwa yoyote kati ya matendo au malengo
yafuatayo, yaani:-

(a) kifo, kumlemaza au kumjeruhi, au kufungwa au kumzuia,
Rais;

(b) kumwondoa Rais madarakani isivyo halali kutoka katika
wadhifa wake wa Urais au kumwondolea ufahari, heshima na jina la Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;

(c) kupindua kwa njia zisizo halali, Serikali ya Jamhuri ya Muungano; au

(d) kutishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
na kubainisha nia hiyo kwa kuchapisha maandishi or machapisho au kwa kitendo chochote cha siri kinachojionyesha cha hali yoyote, atakuwa na hatia ya kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifo.

(3) Mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya Muungano–

(a) aliye na mshikamno na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au anawapa msaada au hifadhi ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko;

(b) anachochea, aidha ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko, mtu yeyote aivamie Jamhuri ya Muungano kwa kutumia jeshi; au

(c) anabeba silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa amri, kwa nia ya kutumia nguvu ya kuizuia, kuilazimisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano kubadilisha vigezo au ushawishi wake, au kwa nia ya kulazimisha au kuzuia au kutishia, Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
atakuwa na hatia ya kosa la uhaini na atawajibika kwa adhabu ya kifo.

Nime tafuta ktk Vifungu hapa sijaona Sehemu ambayo Mh Lissu anahusika nacho moja kwa moja.Anacho fanya Mh Lissu ni kuelezea Ulimwengu juu ya lile lililomtokea na hatua zilizo chukuliwa na Serikali yake.

Ukumbuke sisi ni Binadamu na tunazo Haki za Msingi za kuishi ,haziombwi zipo tu tangu tulipo kuwa Tumboni mwa Mama zetu..Mh Lissu ana tetea Haki zetu za Msingi zinazo chukuliwa na Binadamu wengine kinyume kabisa na Utaratibu wa Sheria..
 
Aliyesababisha deni ni nani? na kule duniani hakuna siri za kichawi kama mnazofanya Lumumba
kwa hiyo wajibu wenu ni kushiriki kuikandamiza badala ya kusaidia njia bora. Je kwa busara ya mihilimi mitatu ndege haikuja? Bado mmesupataza shingo shame on you
 
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ina katiba inayotambua Rais,Bunge na mahakama. Unapotukana mihimili hii mitatu unajunja katiba inayoweka miiko na taratibu za nchi.

Katiba inamtambua rais aliyepatikana kwa kura za wananchi, unapohamasisha Rais apingwe kila kona na kususiwa huo sio UASI.

Rais hakukwapua madaraka kama unavyotaka yakwapuliwe. Ujuwe kwa katiba hii kama utakuwa Rais kwa mkono wa wafadhili wako sawa lakini kama ni katiba hii wewe ni Muasi tayari.

Bunge ni mhimili mwingine unaoubeza ambao umekulea na kukuapisha kutii katiba na sheria za nchi pia unayo kura ya kutokuwa na imani na Rais kwa nini usitumie ushawishi kikatiba kumtoa Rais madarakani.

Kama kuna kuvunja katiba kuna mahakama ya Katiba lakini umeamuakutumia shortcut. Hukumbuki shortcut itakulazimu kuja na majeshi yako, katiba yako, wanajeshi wako, usalama wako nje ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Absolutely wewe ni Muasi
Aliyetaka kumwua lissu yeye tumwiteje? Acha mizaha na maisha ya watu
Unaacha kuhoji wasojulikana unahangaika na lissu ambae Mungu amemwokoa na kifo?
Jinga sana kiwango cha standard gauge
 
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ina katiba inayotambua Rais,Bunge na mahakama. Unapotukana mihimili hii mitatu unajunja katiba inayoweka miiko na taratibu za nchi.

Katiba inamtambua rais aliyepatikana kwa kura za wananchi, unapohamasisha Rais apingwe kila kona na kususiwa huo sio UASI.

Rais hakukwapua madaraka kama unavyotaka yakwapuliwe. Ujuwe kwa katiba hii kama utakuwa Rais kwa mkono wa wafadhili wako sawa lakini kama ni katiba hii wewe ni Muasi tayari.

Bunge ni mhimili mwingine unaoubeza ambao umekulea na kukuapisha kutii katiba na sheria za nchi pia unayo kura ya kutokuwa na imani na Rais kwa nini usitumie ushawishi kikatiba kumtoa Rais madarakani.

Kama kuna kuvunja katiba kuna mahakama ya Katiba lakini umeamuakutumia shortcut. Hukumbuki shortcut itakulazimu kuja na majeshi yako, katiba yako, wanajeshi wako, usalama wako nje ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Absolutely wewe ni Muasi
Tutumie bunge la ndugai???? R u serious????.. Hili bunge la kila anapoongea mpinzan unakuta boya anainuka anadai taarifa????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lete ushahidi wapi na lini Rais aliagiza Lisu apigwe Risasi.Acheni propaganda jino kwa jino

Ili nikijibu na wewe niambie ni nani mwenye Mamlaka ya kuweza kuamuru Eneo la Viongozi liondolewe Askari Polis walio kuwa zamu.

Baada ya Tukio tuambie ni nani mwenye Mamlaka alie amuru Camera za CCTV ktk Nyumba ya Kiongozi wa Madini Bw Kalemani..

Hayo Machache niliyo ya ainisha yanaonesha Nia Ovu ya Walio panga Mauaji ya kumuua Mh Lissu ,na hayo Maswali yanazua Alama za kuuliza Sbb ya Uzito wa Suala lenyewe.
 
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ina katiba inayotambua Rais,Bunge na mahakama. Unapotukana mihimili hii mitatu unajunja katiba inayoweka miiko na taratibu za nchi.

Katiba inamtambua rais aliyepatikana kwa kura za wananchi, unapohamasisha Rais apingwe kila kona na kususiwa huo sio UASI.

Rais hakukwapua madaraka kama unavyotaka yakwapuliwe. Ujuwe kwa katiba hii kama utakuwa Rais kwa mkono wa wafadhili wako sawa lakini kama ni katiba hii wewe ni Muasi tayari.

Bunge ni mhimili mwingine unaoubeza ambao umekulea na kukuapisha kutii katiba na sheria za nchi pia unayo kura ya kutokuwa na imani na Rais kwa nini usitumie ushawishi kikatiba kumtoa Rais madarakani.

Kama kuna kuvunja katiba kuna mahakama ya Katiba lakini umeamuakutumia shortcut. Hukumbuki shortcut itakulazimu kuja na majeshi yako, katiba yako, wanajeshi wako, usalama wako nje ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Absolutely wewe ni Muasi
Ivi magufuli alishinda kweli uchaguzi wa 2015?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nime tafuta ktk Vifungu hapa sijaona Sehemu ambayo Mh Lissu anahusika nacho moja kwa moja.Anacho fanya Mh Lissu ni kuelezea Ulimwengu juu ya lile lililomtokea na hatua zilizo chukuliwa na Serikali yake.
Tundu Lissu ni Mtanzania pekee aliyekumbwa na tukio la shambulizi wa aina yake tokea tupate Uhuru!? Hao Watanzania wengine waliokumbwa na matendo ya Kihalifu hapa nchini Serikali ilichukua hatua gani!?

Ukumbuke sisi ni Binadamu na tunazo Haki za Msingi za kuishi ,haziombwi zipo tu tangu tulipo kuwa Tumboni mwa Mama zetu..Mh Lissu ana tetea Haki zetu za Msingi zinazo chukuliwa na Binadamu wengine kinyume kabisa na Utaratibu wa Sheria..
Sio binadamu tu bali hata wanyama na viumbe hai wote wana Haki za kimsingi Kuishi. Lissu hatetea Haki ya mtu yoyote ya kimsingi bali anatetea Maslahi yake binafsi na ulafi wa madaraka. Muda utaongea.
Hizo Haki "zenu" za msingi zinazochukuliwa na binadamu wengine kinyume cha na utaratibu wa Sheria ni Zipi!? Na hao binadamu wanaozichukua ni Kina nani!?
 
Habari yenyewe ni hiii ....

Mbunge wa Singida Mashariki amefanya mkutano na waandishi wa habari akimtuhumu Magufuli kwa mambo mengi na kutaka asusiwe kila mahali. Amesema mataifa ya nje yanayompa hela Magufuli yamsusie Magufuli na kutompa pesa za kuikandamiza Tanzania. Kujenga uwanja wa ndege Chato ni kama Mobutu Seseseko alivyojenga kijijini kwao.

Amesema Mwinyi na wengine wanaotaka Magufuli aongoze miaka zaidi ya 10 wanataka Magufuli awe kama rafiki zake Nkurunziza, Kagame na Joseph Kabila na kuita huo ni ujinga. Wanaoshangilia Bombardier hawajui zimenunuliwaje na Magufuli anaendesha nchi kwa misingi ya kikabila na Kifamilia, akimtolea mfano Dotto James Katibu Mkuu wizara ya fedha na Naibu wake ni watoto wa dada alikuwa afisa ngazi za chini wa TANROADS miaka 2 iliyopita na wanaambiana mjomba tununue ndege, tujenge uwanja wa ndege nyumbani na hela zinatoka. Mmoja wa wanasheria wa wizara mmoja Medad Kalemani na Naibu Waziri nishati na madini hakufukuzwa kwenye skendo ya madini iliyomuondoa Muhongo. Kuingilia uhuru wa mahakama. Anawaambia majaji kwenye mikutano ya hadhara namna ya kutoa hukumu. Sasa ni mwezi wa 8 mahakama ya Tanzania haina Jaji mkuu ina Kaimu jaji mkuu na hii haijawahi kutokea Magufuli anajiona yeye ndio dola kwenye karne ya 21.

Majaji wa mahakama kuu 4 kujiuzulu ndani ya miezi 3 haijawahi kutokea na sababu wala maelezo hayatolewi japo kuna baadhi yao walihusika na Escrow ila haijatolewa sababu Kama majaji wanalazimishwa kujiuzulu bila maelezo nani yupo salama? Vyombo vya habari vinavamiwa kwa bunduki na hakuna hatua inayochukuliwa Tunaposema udikteta ndio huu. Kazi ya kupinga udikteta sio ya CHADEMA tu, ni vyombo vya habari, wafanyakazi wa serikali viongozi wa dini. Kutumia vibaya fedha na rasilimali za taifa.

Sasa nikuulize ,unahisi hapa hakuwa na Hoja za Msingi ?

Huo Uwanja wa Ndege wa Chato Pesa zake zili hidhinishwa au kupitishwa na Bunge ?
 
Uhaini (kutoka neno la Kiarabu) ni pale mtu anapotenda jambo dhidi ya nchi yake. Kwa mfano, mtu anaweza kuisaidia nchi nyingine ipigane vita dhidi ya nchi yake kwa kutoa habari za siri.

Uhaini ni neno la kawaida, lakini nchi tofauti zina sheria na adhabu tofauti dhidi ya matendo ya kihaini, hata adhabu ya kifo.

Miongoni mwa wahaini maarufu duniani kuna Yuda Iskarioti, Benedict Arnold, Philippe Pétain na Vidkun Quisling.

Kwa Hisani ya Wikipedia.
Lissu ameisaidia nchi gani ipigane vita na Tanzania...na ametoa siri gani hizo
 
Nimegundua kipindi cha mzee kikwete na kipindi cha magu akijabadilika chochote isipokua wananchi ndo tumebadilika nadhan wote tunapenda kuiba ila atupendi kuzitumia pesa izo mbele yetu we chukua tumia kimya kimya ivi mtu leo ameondoka na 1.5 t ingekua kipindi cha kikwete ingekuaje kwel wananchi wale wale na wabunge wale leo tunatetea tunasema hesabu ziko sawa tunabushana kabs na mpiga hesabu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mbona adhabu yake ya usaliti yeye Mh. Lissu anaijua mpaka sasa, it is just the matter of time! Labda asirudi aishi huko huko mpaka azeeke akaishi kwenye nyumba za wazee.
Hahaaah mkuu kuna adhabu mnayoweza kumpa lissu kubwa zaidi ya zile risasi 38...
 
Back
Top Bottom